Villky_J
JF-Expert Member
- Mar 14, 2017
- 492
- 609
Habari wana jamii forum.
Kwa muda mrefu Sasa nimekuwa nikuvutiwa sana na kazi ya ushauri na unasihi jambo lilonifanya kuwa mdau mkubwa na mfatiliji wa makala, vitabu na maandiko yanayohusu Elimu ya saikolojia na unasihi. Hivyo nimejikuta napenda kukutana na watu mwenye matatizo yanahitaji ushauri.
Hivyo mara kadhaa nimekutana na watu wa aina hiyo..na kuwasaidia na kwa kiasi kikubwa nimefanikiwa kwani kuna baadhi yao wamekiri kuwa nimekuwa msaada mkubwa katika maisha yao, kwani nimeweza kuwa badilisha mtazamo wa maisha hivyo kuwafanya kuwa na furaha zaidi kuliko walivyokuwa hapo awali.
Baadhi ya watu nilikutana nao na kuwasaidia ni hawa wafuatao.
1.Yupo dada alietaka kuteketeza familia yake kwa kutaka kuweka sumu kwenye Chakula ili wanapokula wafe familia yote pamoja na yeye kutokana na wivu wa kimapenz aliokuwa nao kutokana na mumewe aliekuwa akimsaliti.
2.Yupo dada aliekuwa akiuza mwili wake (changudoa) nikamsaidia na kuacha kabisa biashara hiyo haramu na kuamua kujishughulisha na shughuli nyingine za kawaida kujipatia kipato.
3.Yupo kaka aliekata tamaa ya maisha kutokana na kifilisika mali hivyo msongo wa mawazo ulimfanya kuwa kama mtu aliechanganyikiwa. Japo ilinichukua muda mrefu lakini 75% nilimsaidia kwani alianza kurejesha tumaini na kuamini kuanguka mara moja sio mwisho wa mchezo.
4. Lakini pia yupo aliekuwa na ugomvi na wazazi wake na kutozungumza nao vizur kwa muda kama miaka 10, sababu baba yake alimfukuza nyumbani kwa kuwa alipata ujauzito akiwa angali anasoma.
Hao ni baadhi ya waathirika nilioweza kuwasaidia. Ukweli ni kwamba sina Taaluma hii, (kutoka darasani) lakini nahisi nina kitu ndani yangu. Naomba m nisaidie wadau, Je, naweza kufanya kazi hii ikiwa sina cheti na kibali kinachoniruhusu kufanya kazi hii.
Vile niko tayari kujitolea kwa mtu mtu yoyote anayefanya kazi hii ili aweze kunikutanisha na watu wenye matatizo mbalimbali lakini pia kunifunza mengi zaidi kuhusu kazi hii.
Nafikir hii ni kazi ninayoipenda zaidi kuliko kazi nyingine.