Navumilia mpaka lini tendo la ndoa??baada ya kujifungua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Navumilia mpaka lini tendo la ndoa??baada ya kujifungua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 27, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,169
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Baada ya Kujifungua....  [​IMG]
  MAMBO YA KUZINGATIA MWANAMKE BAADA YA KUJIFUNGUA MTOTO
  Wanawake wengi huwa katika wakati mgumu kufahamu ni line wanaweza kurudi kwenye maisha ya kuendelea na tendo la ndoa (sex) na waume zao baada ya kujifungua.
  Pamoja na kuwa na imani potofu zinazozuia mwanamke kujihusisha na sex baada ya kuzaa mtoto bado hakuna uthibitisho wa kitaalamu (scientific research) kuelezea ni muda gani muafaka wa kuanza sex baada ya kujifungua au hatari za kuendelea na tendo la ndoa baada ya kujifungua.
  Mke anao uhuru wa kuamua ni wakati gani anajiona yupo huru kuanza tena kushiriki katitka sex na mume wake.
  Je, ni muda gani hasa hutakiwa?
  Inapendekezwa kwamba ni kiasi cha wiki sita uterus huwa katika hali ya kawaida baada ya mtoto Kuzaliwa (vaginal birth) hiki ndicho kimekuwa ni kipimo cha wakati wote jamii nyingi duniani.
  Ingawa wapo wanawake huwa tayari kihisia na kimwili kushiriki sex na waume zao kabla ya hizo wiki sita, pia lini mwanamke aanze inatokana na complications za wakati wa kujifungua (delivery).
  Jambo la msingi ni pale anapojisikia yupo comfortable.
  Kwa wanawake wengine inachukua zaidi ya wiki sita kuwa tayari kufanya mapenzi.
  Mambo ambayo huhisiana na kuanza kwa kufanya mapenzi mapema ni maumivu kutokana na kisu wakati wa kuzaa (episiotomy), kuvuja kwa damu nyingi, kuchoka Na pia mwanamke kuwa mkavu (chini) kutokana na kiwango kidogo cha estrogens hasa baada ya kujifungua.
  Wanawake ambao kuzaa kwako kulikuwa na labour ya muda mrefu, au upasuaji au kuzaa kwa kusaidiwa (vacuum extraction, forceps or caesarean) ni vizuri kusubiri hadi wiki kati ya 8 hadi 12 au zaidi.
  Na wale ambao kuzaa kulitokana na kuchanwa (perineal tearing) wanaweza kusubiri hadi miezi kadhaa baada ya kupona kabisa.
  &&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
  Je, kuna tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa?
  Ndiyo kuna kufanya mapenzi (sex) baada ya mtoto Kuzaliwa.
  Kawaida kabla ya kujihusisha na tendo la ndoa ni vizuri kuwasiliana na daktari wako kukagua kama kumetokea healing ya kutosha kwa uterus na perineum ambayo mara nyingi huchukua wiki 6 baada ya kujifungua mtoto.
  Baada ya daktari kuwapa go ahead, basi unahitaji kuwa wazi wewe na mume wako kusema namna gani kila mmoja anajisikia kimwili na kihisia.
  Kukimbilia kuanza sex mapema kabla mmoja hajawa tayari inaweza kusababisha mambo kwenda vibaya.
  Pia hofu ya kuumizwa (hurt) kwa mke huweza kutawala ubongo na pia mtoto kulia inaweza kuwa ni kizuizi cha mahaba.
  Ukiona sex ni painful, ni vizuri kwenda polepole na Kumbuka kuhakikisha huko chini (mwanamke) yupo lubricated hata kwa kutumia KY jelly.
  Pia inabidi mke azingatie kwamba maziwa huweza kuchuluzika wakati wa tendo la ndoa.
  Hili si tatizo na si kiwango Kikubwa kuweza kuathiri uwingi wa maziwa ya mtoto.
  Mara nyingi hii hutokea miezi miwili ya kwanza kwa wanawake wengi na Baadhi huendelea hadi miezi 8 kama ananyonyesha mtoto maziwa (breasts feeding).
  Jambo la kuzingatia kwa mwanamke ni kuhakikisha baada ya kushiriki tendo la ndoa na mume wake ahakikishe anajisafisha matiti yake na mikono yake (kuzingatia usafi) kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto.
  Kumbuka “Cleanness is second to godliness”
  Tips kwa mwanamke!
  1. Usikimbilie na kuwa na haraka kwa ajili ya kuanza sex, take your time.
  2. Panga njia ya mpango wa uzazi kabla ya kujihusisha na tendo la ndoa, uwe makini unaweza kujikuta una mimba miezi miwili tu baada ya kujifungua mtoto.
  3. Ni vizuri kuwa pamoja kama wazazi hivyo panga mipango mingi zaidi kuhusiana na mtoto.
  4. Inabidi kuwa na ratiba mpya ya sex kwani si kweli kwamba kila muda kwa kwenda kulala unaweza kuwa muda mzuri wa sex hasa kutokana na mahitaji ya mtoto. So be spontaneous.
  5. Kumbuka wakati huu sex ni quality na si quantity.
  6. Zungumza kama kuna hofu na mashaka yoyote ya wewe mke kujihusisha na tendo la ndoa.
   
 2. T

  Tall JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  MAJIBU YA MASWALI YAKO UMESHAYAJIBU.HATA HIVYO CHUKUA HII.
  1. KILA KABILA LINA MILA ZAKE JUU YAHILI.FUATA MILA ZA KWENU KAMA UNAONA ZINAFAA MAANA NDIZO ZILIZOKUKUZA.
  2.RAHA YA NGONO NIKUIPATA PALE UNAPOIHITAJI.NJAA INAUMA LEO VIPI ULE CHAKULA KESHO?HATA HIVYO MKIGEUZA HAKO KAMCHEZO KATAMU NDIO KAZI,KILA SAA MPO TU MSISHANGAE KUPATA MTOTO KILA BAADA YA MIEZI TISA.
  3.KWA WANYAMA WOTE NI BINADAMU TU ANAEFANYA NGONO KAMA STAREHE.WANYAMA WENGINE NI KWA AJILI YA KUZAA TU.KWA AJILI HIYO AFYA YA MZAZI
  MARA NYINGI HUPUUZWA.
  4.MWANAMKE AKIZAA,HARAFU AKAPATA DIET/MLO SAFI,MLO MAALUM ASIFANYE KAZI YOYOTE,NA WALA ASIMEGWE.HUPENDEZA SANA,NGOZI YAKE HUWA LAINI SANA ANAMELEMETA.KWA AJILI HIYO WANAUME UZALENDO HUWASHINDA WANAAMUA KUWAMEGA. KAMA WANGEVUMILIA ZAIDI WANGEFAIDI ZADI.MTUNZE SANA MKEO BAADA YA KUJIFUNGUA ILI AWE READY KUMEGWA MAPEMA.
  Aaaah,labda ni seme hivi swala la lini mle tunda tena baada ya kupata mtoto HALINA FORMULA. inategemea na na hali na maumbile ya mtu
   
 3. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Vipi na je kama umekula kisu then baada ya wiki mbili kutoka hospitali then mme akapwata na hamu then akataka kujiexpress vipi hii style nayo inakubalika au inamadhara.
   
Loading...