Navalny atunukiwa tuzo ya juu ya haki za binadamu ya Umoja wa Ulaya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Kiongozi wa upinzani nchini Urusi aliye gerezani ambaye pia ni mkosoaji mkubwa wa rais Vladmir Putin, Alexei Navalny leo ametunukiwa tuzo ya juu kabisa inayotolewa na Umoja wa Ulaya kuhusu haki za binadamu.

Katika ishara ya wazi ya ukosoaji kwa Ikulu ya Kremlin, viongozi wa bunge la Umoja wa Ulaya wamemteua Navalny kupokea tuzo hiyo kutoka kundi lililojumuisha wagombea wengine ikiwemo rais wa zamani mpito nchini Bolivia Jeanine Anez.

Tangazo kuhusu tuzo hiyo limetolewa kupitia ukurasa wa Twitter wa Bunge la Ulaya likiwa pia na ujumbe wa kuzitaka mamlaka nchini Urusi kumuachia huru kiongozi huyo wa upinzani aliyekamatwa na kutupwa gerezani mwazoni mwa mwaka huu.

Uamuzi wa kumtunuku tuzo hiyo Navalny yumkini utadhoofisha zaidi mahusiano yaliyopwaya kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi tangu Moscow ilipoinyakua kwa nguvu rasi ya Crimea mwaka 2014 na ilipotuhumiwa kuhusika na shambulizi la sumu dhidi ya Navalny.
 
Wamemsaidia nani kupata hizo haki za binadam?

Tatizo kubwa la nchi za magharibi ni unafiki uliovuka mipaka. Navalny hajawahi kuwa mpinzani wa Putin au mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Urusi. Huyu mwanamama Jeanine wa Bolivia yeye ni dikteta kabisa aliyehusika na mapinduzi ya Evo Morales (mjamaa)na njama za kumuua akiwa kwenye ndege kabla kutorokea Mexico. Ni mwanamke aliyeua wahindi wekundu wengi sana waliokuwa wanamtaka bado Evo Morales.
 
Back
Top Bottom