SOLD: Nauza sofa set (Love seat) na L-shape jumla ya seat ni 7

Status
Not open for further replies.
Dec 31, 2021
5
5
Habari wandugu,

Nauza sofa set yenye jumla ya siti saba (7). Muundo wa sofa ni (Love seat) ambayo ni siti ya watu wawili. L-shape ambayo inaunganisha vipande vitatu. Kipande kidogo cha siti ya mtu mmoja, kipande kimoja cha siti ya watu wawili na kipande kirefu cha siti ya watu wawili.

Ni nzuri na imewekwa springs kwenye siti zake zote, ni za kisasa na zimetengenezwa kwa materials original.

Sofa hii tangu inunuliwe mwezi February mwaka 2021 haikuwahi kutumika, ilitunzwa tu mahali. Thamani yake ya dukani ni Milioni moja, nimeweka picha ya risiti hapo. Ila mimi naiuza kwa 650k. Faida kwa wafanyabiashara, wenye maduka makubwa nakupa assurance sofa hii ukiiweka dukani unaweza kuiuza mpaka 1.5M na wenye maduka ya kawaida unaweza kuiuza mpaka 1M.

Watumiaji wa kawaida ambao siyo wafanyabiashara karibuni, kwani utapata sofa kali, yenye ubora ya ghali lakini kwa bei nafuu sana.

Picha nilizopiga hapa, nimepiga zikiwa kwny chumba kilichohifadhi hizo sofa, sikuweza kuzitoa nje ili nipate picha ikizionyesha kwny mpangilio wake kama ambavyo ingeonekana kwenye sebule kutokana na kuepuka kuzikarahisha, kutoa nje na kurudisha ndani kuzipanga tena upya. Karibu uzione na uzitathmini mwenyewe, maana maneno pekee hayatoshi.

Karibuni kwa mawasiliano 0687 747 989 WhatsApp/Call.

Mali hii ni yangu na risiti ya manunuzi nitakupatia. Mimi siyo dalali na sihitaji dalali. Nahitaji mteja kwa bei ya 650,000 TSHS.
View attachment 2063814View attachment 2063815View attachment 2063816View attachment 2063817View attachment 2063818
IMG_20211230_160602.jpg
 
Hicho kitambaa kinaonyesha kama kimetumika...anyway, goodluck
Ha ha! Sawa chifu ubarikiwe. Unaruhusiwa kukagua lakini kama unafahamu sponge iliyotumika ukiibonyeza haitoi noise. Sponge mpya kwa wajuzi wa mambo ukiibonyeza kuna kitu inakueleza. By the way hata sofa zingekuwa zimetumika kweli. 650k ni very fair price kwa wanaojua vitu vizuri
 
Ha ha! Sawa chifu ubarikiwe. Unaruhusiwa kukagua lakini kama unafahamu sponge iliyotumika ukiibonyeza haitoi noise. Sponge mpya kwa wajuzi wa mambo ukiibonyeza kuna kitu inakueleza. By the way hata sofa zingekuwa zimetumika kweli. 650k ni very fair price kwa wanaojua vitu vizuri
Kweli kweli..sure
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom