Wapi linapatikana soko la chia seed kwa hapa Dar na mikoani

kimsingi hii sio dawa ni chakula na tatizo la nguvu ya kiume kuna ambayo inahitaji dawa na ambayo inahitaji kubadilisha jinsi ya kuishi (Life style changes). Jambo kuu ni kuhakikisha unapata mlo kamili ambao uko una makundi yote saba ya chakula ili mwili ukae vizuri. Mtu anaweza kutumia akaona kuwa anakuwa na nguvu kwasababu mbegu hizi zina madini mbalimbali na Omega 3 na 6 hivyo kuona kuw inamsaidia ila wataalamu wa afya watakueleza sio chakula kimoja kina vitu vyote unavyohitaji. Hi ni moja ya supplement muhimu ila tumia na vyakula vingine ili upate kuwa na afya bora. Karibuni nikuhudumie hakuna hype ni uhalisia
NAOMBA ELIMU SAHIHI KUHUSU OMEGA 3&6 NI MANENO MAGENI KWANGU
 
Omega 3 na 6 Ni mafuta muhimu yanayotakiwa kwenye mwili mwa binadamu kwa ajili ya kupunguza cholesterol mbaya mwilini na inapunguza inflamation ( Ni seme kama vimbe zinazokuwa vyanzo za magonjwa) na vilevile inakuongeze kumbukumbu na kupunguza kupata magonjwa ya Alzheimer’s. Kama unakumbuka zamani tulipokuwa wadogo tulisisitizwa sana kupata mafuta ya samaki maana nayo ina hii kitu.


NAOMBA ELIMU SAHIHI KUHUSU OMEGA 3&6 NI MANENO MAGENI KWANGU
 
Nimeona watu wengi hawafahamu chia ni nini. Naomba nifafanue.
Chia au maarufu kama chia seeds ni jamii ya mimea kama ufuta/ulezi. Zimejipatia umaarufu miaka ya hivi karibuni kwa kuwasaidia watu wanaotaka kupunguza mwili na kuboresha afya ya uzazi. Chia seeds zina uwezo mkubwa wa kuunguza mafuta mwilini, kusaidia mmeng'enyo wa chakula, kuchochea mzunguko wa damu katika mishipa. Hivyo zimeanza kushika kasi Tanzania hasa hasa katika swala zima la diet na ni biashara inayokuwa kwa kasi. Ningewashauri wale wanaotaka kuboresha afya zao katika kupunguza mwili na kuchochea mzunguko wa damu kuzitumia, hutojutia.
 
Napenda kuwataarifa wanajamii forum kuwa ninazo chia zenye ubora na ambazo zimeandaliwa kwa matumizi ya binadamu,Napatikana kwa namba hii 0622 296251.Nipigie au niwekee sms nitakujibu.Karibu tufanye biashara.Ofa kubwa ukichukua kuanzia kilo 100 nitakuuzia kwa Tsh 8,000.tu.
Namba yako haipo kabisa. Ebu toa namba inayopatikana, wateja wapo.
 
Napenda kuwataarifa wanajamii forum kuwa ninazo chia zenye ubora na ambazo zimeandaliwa kwa matumizi ya binadamu,Napatikana kwa namba hii 0622 296251.Nipigie au niwekee sms nitakujibu.Karibu tufanye biashara.Ofa kubwa ukichukua kuanzia kilo 100 nitakuuzia kwa Tsh 8,000.tu.

Hello, ni nahitaji kujua zaidi kuhusu chia seeds na upatikanaji wake!
Chia seeds zinapatikana mwaka mzima?
Kuna issue naifuatilia kuna buyer anahitaji hii bidhaa kwa wingi!
Processes za usafirishaji na vibali vya exports vimekaaje?
Tuwasiliane +8618857052304
 
Ninavyoendelea kupata repoti jinsi gani mbegu hizi zikitumia zinaweza kusaidia kupunguza uzito ndio nafurahi shuhuda nyingi zinaonyesha mtu anaweza kupunguza kilo 1.5 to 2 kwa wiki kitu ambacho ni kizuri kwa afya. Karibuni mjipatie mbegu za chia
 
Hii natumika sana katika kupunguza uzito kwasababu inaumuka sana na hivyo kumfanya mtu anayekula asisikie njaa haraka.
Hii sayansi ya "kuumuka na kumfanya mtu asisikie njaa" imekaaje? kuna mtu mwingine akishaweka kitu kwenye sahani, lazima agonge chote kiishe regadless tumbo lake "limeumuka" kwa kunywa maji, juice au chea seed.
 
Ni kwamba mbegu ya chia inauwezo wa kuumuka mpaka mara kumi yaa. na kwa kuwa inavirutubisho vinavyotakiwa kwenye mwili inamsaidia mtu ambaye hawezi kujipima msosi kuweza kula vyakula vingine kidogo. Kama inavyojulikana kuwa lifestyle ndio chanzo kikubwa cha magonjwa yasiambukiza( Non Communicable Diseases) hii ikiwa iko katika moja ya vifaa( tools) zako inaweza kukufanya upungue bila kujiumiza au kukaa na njaa sana. Watu wengi waliojitahidi kupunguza uzito wanajua kuwa wamefanya jitihada fulani ila ili ufanikiwe katika hili sio sio kuwa na diet tu unatakiwa kubadilisha mtindo wa wamaisha bila kufanya hivyo itapunguza kilo 3 leo baada ya miezi mitatu unaongeza 5. Sasa katika kubadilisha mtindo wa maisha yaani kuweka balance diet, kufanya mazoezi na kupumzika vya kutosha. Chia inakusaidia hapo kwenye kueweka balance diet ambayo hainenepeshi na vilevile inakupa kupunguza kula vyakula vingine kwa wingi ambao ndio chanzo cha watu kunenepa kula chakula kingi kuliko mwili unavyohitaji.
Napenda kusisitiza hili kuwa kula chia pekee yake hatakusaidia kama hutakubali kubadilika katika mlo ambapo utatakiwa kula milo kamili wanga kidogo( Ugali Wali, Ngano hakikisha isizidi ukubwa wa ngumi yako), Mbogamboga ( Nusu ya sahani yako), Protein 15%-20%( Maziwa, Maharage, Nyama, Samaki, Soya, Choroko, Kunde....) ya sahamani unamalizia na Matunda. Ukifuata aina hii ya mlo na mazoezi kidogo atleast mara tatu kwa wiki unaweza kuanza kwa kutembea kila siku hatua 10,000/ baada ya miezi mitatu njoo toa shukrani



Hii sayansi ya "kuumuka na kumfanya mtu asisikie njaa" imekaaje? kuna mtu mwingine akishaweka kitu kwenye sahani, lazima agonge chote kiishe regadless tumbo lake "limeumuka" kwa kunywa maji, juice au chea seed.
 
Okay ndugu nimekupata inaonekana kutakuwa na uhaba wa chakula huko mbele. Ila kwakuwa nazo tech za kulima bila udongo zimeshafika naamini tupata suluhisho tuu,

Haya fursa ndio hizo. Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa fursa kubwa katika nyanja za kiuchumi zitakuwa uzalishaji wa chakula na FinTech kwa miaka hii 5 to 10 ijayo.
 
Nauza Chia Seed kwa jumla Zipo nusu tani.
Bei kwa kilo ni shilingi 15000
Zipo Morogoro
Mawasiliano ni 0622362897/ 0673362897.
Mazungumzo yapo.
 
Nauza Chia Seed kwa jumla Zipo nusu tani.
Bei kwa kilo ni shilingi 15000
Zipo Morogoro
Mawasiliano ni 0622362897/ 0673362897.
Mazungumzo yapo.
 

Attachments

  • IMG-20190317-WA0026.jpg
    IMG-20190317-WA0026.jpg
    104.6 KB · Views: 44
Back
Top Bottom