Nauza Hisa za Vodacom, Kila moja nauza 500/=

Habari wakuu daah nilinuanua hisa bila kutafuta washauri sasa nahangaika maana hata kuuza mawakala wote wanasema Hakuna mteja nimejaribu hata kuomba wanipe kiasi chochote Hakuna majibu.

Nimeleta hapa maana nafahamu hapa kuna wadau wengi zipo Hisa 200 tu, nipo radhi kuchukua kiasi chochote kwa atakayehitaji na sifahamu kama nitakuwa sipo sahihi kimaelezo mtanilekebisha asante!

WIMICKY Tafadhali soma Elimu ya Uwekezaji wa Hisa
Dah tulkurupuka mwenyee nimetangaza kuuza lkn akuna kitu
 
uwekezaji wowote unachangamoto zake, ukilalamika hisa za voda wengine watasema za TOL, wengine za NICOL wengine za PAL pia wengine za CRDB kikubwa ni kufahamu na kufuatilia uwekezaji wowote vizuri kabla na si baada uwekezaji katika maswala ya kifedha ni ngumu zaid maana huoni moja kwa moja.

Jipeni moyo wakuu soko likikaa sawa mtapata wateja ama hisa zikapanda bei na mkaja uza kwa bei nzuri baadae
M
 
Biashara ya hisa hapa Bongo ni pasua kichwa.

Kuna wale wachaga hakina Mengi, sijui Mosha na wenzake walikuja na kampuni wakiita NICOL wakauza hisa nikanunua, yaani ilikuwa ni utapeli.

Pesa niliipoteza kwenye hiyo kampuni ya kihuni.

Sent from my HTC U12 life using JamiiForums mobile app
 
Nimekuelewa boss ila napata mashaka na ukubwa wa dividend iliyotolewa. Labda iwe ni accumulated dividend arrears for some years
Hii ya 178.57 per share wameiita special dividend. Dividend ya kawaida ni sh 12.26 per share. Mimi ni mwanahisa wa voda.
 
Kama bei ya hisa moja ni 17000 basi gawio lake sh.250 kwa hisa ni hela ndogo sana wala sio la kufurahia. Tafsiri yake ni kuwa elfu 17 inakuzalishia sh.250 kwa mwaka!
Ndio maana biashara ya hisa inatakiwa uwe na mtaji wa kutosha na pia uangalie thamani ya hisa na faida zake (Taarifa kwanza). Vodacom hisa moja TZS 770 gawio 178/ TCC hisa moja TZS 17,000/- gawio TZS 250/- . Moja kwa moja kwa mtu mwenye mtaji anae taka kununua hisa anaangalia pia gawio na sio thamani ya hisa.
 
Voda hiyo gawio la 178 mwakani halitorudia. Nahisi kuna mali/asset wameuza ndio wanalipa kiwango hicho.



Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
Naona bado ana faida kwenye soko na anaweza fanya vizuri zaidi. GB na MPESA zinalipa. Asilima kubwa ya soko la mawasiliano na mobile money analimiliki. Kadiri siku zinavyozidi kwenda watumiaji wa data wanaongezeka. Siku hizi ni bora mtu akose airtime lakin sio Data. Mpaka akina na mama wa makamo ukiinigia kwenye Daladala wapo insta, facebook, whatsapp. Kwa hiyo kama una pesa sehemu sahihi ya kuwekeza ni huko kwenye mawasiliano tu.
 
Jamani voda mbona wamesema wazi kabisa kuwa hiyo 178 sio gawio la kawaida ni special devidend which means next year tunarudi kule kule kwenye 12.26 per share
:p:p:p wacha tuone mwakani watakuja vipi.
 
Wakuu leo tarehe 13/11/2020 ilikuwa siku ya kupata mgao wa hisa zetu. Account zenu zimecheka tayari?
 
Back
Top Bottom