Nauza asali, ni mbichi na haijaongezwa chochote

Tasia, asali mbichi tunaipenda lakini bei yako imepita wastani wa bei ya soko kipindi hiki. Bila shaka wee ni mkulima na sio dalali; weka address zako hapa jamvini, tutakuja ku-bargain hapo hapo dukani kwako.

Kwa wale mnaohitaji kuanzia lita 100 na kuendelea nipeni oder zenu. Asali mbichi kwangu nauza 5,000/= kwa lita ambayo haijachujwa lakini (ghafi kutoka shambani). Hivyo utachuja na kufungasha mwenyewe huko uliko. Tukikubaliana naweza kukutumia mzigo mpaka ulipo (hasa kwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Arusha na Dar). Tatizo wananchi wanakwambia wanahitaji asali kwa wingi kumbe uwezo wao ni lita 5!!!
 
Kama unataka kubobea ktk biashara hiyo ya asali, tafuta asali ya nyuki wadogo wasiouma. Bei ya lita moja ni nzuri, lakini pia kukusanya lita moja ni kazi kubwa !!!!!.
sasa si ndo sababu inakua gali kwa sababu ni ngumu kuzalisha!
 
Kwa wale mnaohitaji kuanzia lita 100 na kuendelea nipeni oder zenu. Asali mbichi kwangu nauza 5,000/= kwa lita ambayo haijachujwa lakini (ghafi kutoka shambani). Hivyo utachuja na kufungasha mwenyewe huko uliko. Tukikubaliana naweza kukutumia mzigo mpaka ulipo (hasa kwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Arusha na Dar). Tatizo wananchi wanakwambia wanahitaji asali kwa wingi kumbe uwezo wao ni lita 5!!!

naomba contacts zako please.
 
Mkubwa tufikirie nasisi tunaotaka kwa matumizi binafsi kama mfano lita moja tu kwa mwezi!!Kama inawezekana naomba njia ya mawasiliano!!
 
Ngoja nikuletee yangu nikuuzie litre1 kwa tsh.6000/=, mana kwa hiyo bei yako ya litre1 tsh.10,000/=, itakuwa nakuachia profit tsh.4000/=. Unapatikana wapi ndugu nikuletee????..
 
Hiyo bei ya Tshs. 4,000 kwa msimu huu haiwezekani labda uuziwe Morasisi iliyochanganywa na sukari lakini siyo asali.

Kuna changamoto ya ukosefu wa takwimu na taarifa za miaka ya hivi karibuni katika sekta ya nyuki. Utakuta mara nyingi unasikia Tanzania inajisifia kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 138,000 za asali na nta tani 9,200. Lakini ukienda hukoa maporini hali ni tofauti kabisa. Miti yenye maua yenye uwezo wa kutoa mchozo imepungua na mazingira yamezidi kuharibiwa. Kwa mkoa kama Tabora, zao la Tumbaku limeua kabisa zao la asali katika uzalishaji na hata katika ubora.
Tani 138,000 ni potential production (kiwango ambacho nchi inaweza kuzalisha kama tungewekeza vya kutosha) kwa mwaka. Ila kiwango halisi ambacho tunazalisha inakadiriwa kuwa ni Tani 4860 (actual production) kwa mwaka. Nayo ni takwimu ya karibu miaka 20 iliyopita.

Jarida la Business Times, 2014. Lilireport kuwa uwezo uzalishaji umefikia Tani 8000 kwa mwaka na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Pili Africa baada ya Ethiopia katika uzalishaji wa Asali.

Kama ulivyosema kuna changamoto ya upatikanaji wa takwimu sahihi katika hii sekta hali inayochangia sana kuizorotesha. Hata hivyo, kuna jitihada zimeanza kutekelezwa kwa ajili ya kuiboresha hii sekta na kuipeleka kwenye level nyingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom