Naupinga Mtazamo wa Kiuchumi wa mzee Edward Lowassa

PharmD

New Member
Dec 18, 2017
3
4
Anaandika Bony Mmbando.

Ninaupinga mtazamo wa kiuchumi wa Mh Edward Lowassa juu ya serikali ya JPM na utengenezwaji wa Ajira nchini.

Swala la Ajira niswala ambalo ukuuaji wake unategemea Zaidi kupanuka Kwa uchumi. Kama uchumi wa jumla unapanuka ni rahisi kuzalisha Ajira kuliko ilivyo sasa uchumi wetu Kwa mujibu wa IMF unasinyaa.

Takwimu za BOT zinaeleza namna ambavyo ujazi wa fedha kwenye mzunguko zilivyoshuka kwa Zaidi ya billion 156tsh kutoka mwaka 2015-17. Hii Inamaana kwamba Uwezo wa watu kufanya matumizi umeshuka maradufu. Uwezo wa watu kufanya matumizi (Purchasing power) ukishuka unaathiri uzalishaji katika viwanda, uzalishaji Lazima Ushuke Hali itakayosababisha viwanda,makapuni, biashara za Kawaida kupunguza Watumishi Hali inayoongeza idadi ya watu wanaotafuta Ajira.

Uingizwaji wa bidhaa (importation of goods) umeshuka Sana sio kwasababu tunazalisha Zaidi, Hapana! Nikwasababu mzunguko wa fedha uko disturbed

BOT wanaeleza kuwa sekta yamanufacturing imeshuka Kwa Zaidi ya 7% maana yake tunazalisha kidogo kwasababu Uwezo wa watu kununua (purchasing power) imeshuka.

Mbali na sera ya viwanda, Uingizwaji wa vifaa vya ujenzi umeshuka sana Maana yake nikwamba hakuna ujenzi wa viwanda unaofanyika nchini, nahata kama Upo nikwa kiwango kidogo Sana. Hii Inamaana kwamba si sekta ya umma Wala binafsi inayofanya ujenzi wa viwanda nchini.

Sekta ya mabenki inakufa, kila Siku tunasikia mabenk yanafungwa, hii Inamaana mbaya Zaidi kiuchumi! Watu hawana hella zakufanya saving, wanachokipata nikidogo Sana. Non performing loans zimepanda Sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

Sekta yakilimo ambayo ndio tumaini letu, inaajiri Zaidi ya Watanzania 70% inaelekea ukingoni.... Poor ikiwa na ukuaji wa 2.3%

BoT wanaeleza kuwa ukipweshaji wa mikopo Kwa sekta binafsi umeshuka maradufu! Means sekta binafsi nayo inaelekea ukingoni!

Tunataka kutengeneza Ajira kwakutumia sekta ya umma? Tatizo la Ajira litatatuliwa Kwa sekta binafsi kuimarika... Serikali inapaswa kutengeneza mazingira ambayo ni condusive Kwa ukuaji wa sekta binafs na uzalishaji wa Ajira.
 
kiukweli lowasa alikwenda ikulu kwa maslahi binafsi. vyote alivyosifu akiwa ikulu ni dhahania tupu. kwa mfano elimu magu kafanya nini? ilhali watoto wa masikini kila siku wanaacha vyuo? je eneo la kudhibiti rushwa magu kafanya nini? ilhali wanaotoa rushwa wengine wamepandishwa vyeo? vipi eneo la ajira? ni mabomu matupu. lowasa alikuwa na yake. matatizo ya wananchi yako palepale.
 
Back
Top Bottom