Naungana na Watanzania Wenzangu Kukemea kitendo cha kihuni kilichofanywa na Paul Makonda pale Clouds

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
"Kenge hasikii Mpaka atoke damu masikioni" Wakuu nimekua Mstari wa mbele Kumtetea Paul Makonda kwa Muda mrefu hadi Leo asubuhi ambapo ambapo Ruge amethibitisha kile kilichoonekana kwenye video fupi ni kweli na Pale ni Clouds Media, nimekua Mtu wa mwisho kuondoa support yangu kwake.

Kama kijana wa Kitanzania sishabikii kitendo vya kihuni hivi Mkuu wa Mkoa wakiwa na Assault riffles kuvamia Kituo cha habari huku tuhuma zake za Vyeti zikiwa bado hazijapatiwa ufumbuzi.

Leo Rais atakua anazindua interchange za barabara pale Ubungo nahisi hotuba yake itatoa Muelekeo tuzidi Kumsikiliza he never afraid to take a step.

Nawatakia Jumatatu Njema.
 
Ni kwa masikitiko makubwa naandika maoni haya.

Nikiwa kama mmiliki vile vile wa chombo cha habari, hii clip ya mh Makonda, RC wa Dar kuvamia Studio za Clouds kwa kutumia askari wanaotakiwa kuwa walinzi wa umma, hili linasikitisha.

Hatuhitaji kwenda mbali, mambo Rwanda yalianza kama hivi hivi.

Mbaya zaidi ni utumiaji wa askari wa umma kwa matakwa binafsi, na pale walikuwa kama mamluki. Kamanda Sirro ana la kujibu hapo.

Kama mmiliki wa chombo, Makonda kulazimisha kuingia studio na kutangaziwa ya kwake, thats not only trespassing lakini ni kosa kubwa la jinai na nashangaa TCRA wako kimya hadi muda huu.

Hapa zitahitajika busara za mh Dr Magufuli kuliweka sawa hili, ama sivyo kiongozi yeyote aliye na mamlaka juu ya vyombo vya usalama, naye atataka kutangaza ya kwake kote nchini.
 
Spot on Lole.

Ikiwa hata wewe umelisemea kwa ukali hivyo basi kunna matumaini mbele ya safari.

Lakini hawa akina Ngabu wenye kutetea na kusifia kila kitu cha awamu hii, hivi kweli hawaoni madhara ya mambo haya katika mustakabali mpana wa Taifa letu? Hivi kwa nini mtu uruhusu kibri na ubinafsi vikutawale hata kwenye mambo yaliyo wazi wazi kama jua angani???
 
Ahakikishe nini sasa kwani huzifahamu sifa za udikteta? Kamishna katimiza sera ya bwana wake na atapandishwa cheo.
 
Ni kwa masikitiko makubwa naandika maonibhaya.
Nikiwa kama mmiliki vile vile wa chombo cha habari, hii clip ya mh Makonda, RC wa Dar kuvamia Studio za Clouds kwa kutumia askari wanaotakiwa kuwa walinzi wa umma, hili linasikitisha.

Hatuhitaji kwenda mbali, mambo Rwanda yalianza kama hivi hivi.

Mbaya zaidi ni utumiaji wa askari wa umma kwa matakwa binafsi, na pale walikuwa kama mamluki.
Kamanda Sirro ana la kujibu hapo.

Kama mmiliki wa chombo, Makonda kulazimisha kuingia studio na kutangaziwa ya kwake, thats not only tresspassing lakini ni kosa kubwa la jinai na nashangaa TCRA wako kimya hadi muda huu.
Hapa zitahitajika busara za mh Dr Magufuli kuliweka sawa hili, ama sivyo kiongozi yeyote aliye na mamlaka juu ya vyombo vya usalama, naye atataka kutangaza ya kwake kote nchini.
Ruge ameshakuhakikishia kuwa aliwavamia na mabunduki usiku wa saa tano kipindi cha shilawadu. sasa unataka rais akuhakikishie nini?
 
Ruge ameshakuhakikishia kuwa aliwavamia na mabunduki usiku wa saa tano kipindi cha shilawadu. sasa unataka rais akuhakikishie nini?
Soma vizuri, tumia akili na uelewe mada kwanza.
Ruge atatuhakikishia kwa vipi kuwa hili halitokei tena?
 
Habari wana JF,

Awali ya yote nieleze hisia zangu za masikitiko makubwa kwa kile kinachoendelea hapa nchini, hasa katika jiji la Dar ambalo ndiyo jicho la Tanzania.

Najiuliza maswali sipati majibu. Hivi majirani zetu wa hizi nchi jirani wanatufikiria je kuhusu vichwani mwetu Watanzania? Je, si kwamba tunaonekana kuwa ni watu wenye akili ndogo kutokana na Upumbavu huu unaondelea hapa nchini tena na wakuu wa nchi wakiushangilia? Au badala ya kujenga Tanzania ya Viwanda ndiyo tunataka kujenga Tanzania ya maSHILAWADU?

Inasikitisha sana nchi kufikia hatua Mkuu wa Mkoa anavamia kituo cha television akilazimisha eti "kipindi chake" kirushwe hewani. Kipindi cha fitina, kuchafuana na kuharibiana sifa. Bora hata kingekuwa ni kipindi chenye manufaa katika jamii. Tena mkuu huyu wa Mkoa anatumia Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la polisi. Hivi kweli ndiko tulikofika?

Watanzania sasa wanafundishwa kujadili matukio ya umbea badala ya kufundishwa kutumia akili zao ipasavyo ili kujiletea maendeleo. Nadiriki kusema haijawahi kutokea awamu yenye mambo ya kipuuzi kama hii. Kweli kwa mtu mzima mwenye majukumu ya nchi, SHILAWADU! Siamini kama ndiyo aina ya akili iliyopo hapo juu.

Nimalizie kwa kutoa wito kwa makundi mbalimbali; Wanazuoni, wanahabari na kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii, simameni pazeni sauti. Nchi inakoelekea siko. Kama ni siasa sasa hizi zitakuwa zimetoka dunia nyingine. Akili ndogo hufikiri mambo madogo.
 
Kwani nini hili halijatikoe? Kwani ndiyo ingekuwa ishara tosha kwa Raisi kwamba hawalitaki chaguo lake, kwa nini maandamano yako Mitandaoni tu na isitoshe 3/4 ya wanaolalama siyo Wana Dar, sasa kwa nini hii mismatch?

Kwanini watu wanapenda kukosoa wakati maandamano wanaweza kuanzisha wenyewe? Kwani ni kazi ya nani?
 
Wengi tunaipenda CCM, lakini lazima akili zetu zibadilike kujua kipi kizuri na kipi kibaya, kukemea yote mabaya na kusifia yote mazuri!

Nasikitika baadhi ya watu wanajali zaidi Chama badala ya kujali MAslahi ya watu walowachagua! Kwa akili za mtu wa kawaida mwenye akili timamu! sio za KUZUNGUUSHA! tokea mwanzoo ilionekana kabisa Daudi Albert Bashite AMEPITILIZA! watu wamepiga kelele sana lakini wenye dhamana walifumba macho na wakaziba masikio!

Imefika mahali Nchi inatikisika! Siri za Serikali zinavuja! watu wanavunja sheria , Mkuu wa NChi ANAKUBALI KUTUKANWA kila pande ya dunia ambapo watanzania wanafuatilia jambo hili!

HAta wale watu wasio wanasiasa nao walikuwa masikio na macho yao yapo wazi!

Hili LIWE FUNZO KWETU SOTE iwe CCM ama chama chochote kile ! SIO MPAKA WATU WAVULIWE NGUO NDIO KUGUNDUA KOSA!

Tunasubiri Kauli YA Mkuu wa nchi !
 
Nafikiri tulipofika tunahitaji Tume ya Maridhiano,kama ilivyokuwa Zanzibar,naomba viongozi wa dini mbali mbali,Retired officers walio hai akina Judge Ramadhani,Warioba na wale wenye calibre ya kutetea uhuru na haki za binadamu,tusiache Taifa likaingia kwenye giza totoro la chuki na ubaguzi,tuseme polipofika panatosha,naomba waamke sasa,chombo kimemshinda muendeshaji anahitaji msaada.

Tusije tukawa kama Mbuni tunasingizia kila siku RUSHWA na UFISADI kumbe hata walioko MADARAKANI ni wale wale wanatofautiana majina tu.
 
Hakuna vita ya madawa kulevya inayomuacha mpiganaji salama....

Wapiganaji wengi dhidi ya wauza unga hufikwa na mauti, hufungwa kwa kesi za ajabu ajabu kama kubaka, mauaji na rushwa. Wengine hutukanwa na kuchafuliwa majina kwa habari za kupika na kughushi.

Wasiojua ukubwa wa Vita ya madawa ya kulevya wanashangaa kuona masahibu anayopitia RC Paul Makonda. Hii ni kawaida ya vita hii haiwezi kumuacha salama ndugu Makonda na hili si geni kwa Tanzania na duniani.

Watanzania na wana CCM wanafaa kufurahi kuwa licha ya ukubwa wa vita aliyoianzisha Paul Christian Makonda bado yupo hai. Maharamia haya yamekosa mbinu ya kumuangamiza kilichosalia ni kumchafua na kumsingizia mambo moja baada ya lingine. Makonda ni shujaa asingelikuwa hai hadi leo.

Mungu anampigania katikati ya maharamia wanaoitafuta roho yake. Wamebaini Mungu yu pamoja naye sasa wameamua kumchafua. Wana CCM wasio jua vita hii nao wameanza kumgeuka. CHADEMA wanaongoza mashambulizi ya kukubomoa ila wewe mawe wanayokutupia yakusanye ujengee msingi imara.

Makonda simama imara, alikufa Amina Chifupa akafanyika sadaka kwa wapiganaji wajao. Hakika hutakufa bali utaishi na wanaokuchafua leo kama kawaida yao watakusafisha kesho.

Umeanzisha vita kali kwa maslahi ya Watanzania, usiogope mabomu, makombora ya matusi na kuzushiwa.

Dhahabu haing'ai pasipo kupitishwa motoni. Songa mbele Makonda. Walio upande wako ni wengi kuliko walio kinyume chako. Kusalitiwa ni sehemu ya uongozi.
 
Kijana badilika, jaribu kuangalia mambo kwa upana wake, muda mwingine ikipidi uweke mahaba ya uchama pembeni, waliokuwa wanaponda utendaji wa Makonda sio kwamba wana wivu naye, yule kijana mwenzetu tabia zake sio, watu walishaona hilo........ukichanganya na ushamba wa madaraka basi akajiona yeye ndio kila kitu.......leo watetezi wake munakuja hapa kwa kujikaza kweli maana munajua amewadhalilisha........pole sana.
 
Maandishi ukutani munashindwa kuyasoma sembuse kuyaelewa hadi jumba lidondoke ndipo muamini! Sawa, ni kweli kwa fahamu zenu wenyewe bila msaada kuelewa hamuelewi maana mu viziwi, vipofu, na wazito wa fahamu.

Basi eleweni japo kupitia sauti za kinabii. Haiwezekani umma wote uwe against mtu mmoja; ni lazima kuna jambo na huo ndio unabii wenyewe. Endeleeni kutetea watenda maovu simply "ni mwenzetu". Wanafiki wakubwa!
 
Shetani na mbwembwe zake zote lakini hawezi kumshinda Mungu,tunaamini Mungu yu pamoja na Makonda katika hili
 
Hakuna vita ya madawa kulevya inayomuacha mpiganaji salama....

Wapiganaji wengi dhidi ya wauza unga hufikwa na mauti, hufungwa kwa kesi za ajabu ajabu kama kubaka, mauaji na rushwa. Wengine hutukanwa na kuchafuliwa majina kwa habari za kupika na kughushi.

Wasiojua ukubwa wa Vita ya madawa ya kulevya wanashangaa kuona masahibu anayopitia RC Paul Makonda. Hii ni kawaida ya vita hii haiwezi kumuacha salama ndugu Makonda na hili si geni kwa Tanzania na duniani.

Watanzania na wana CCM wanafaa kufurahi kuwa licha ya ukubwa wa vita aliyoianzisha Paul Christian Makonda bado yupo hai. Maharamia haya yamekosa mbinu ya kumuangamiza kilichosalia ni kumchafua na kumsingizia mambo moja baada ya lingine. Makonda ni shujaa asingelikuwa hai hadi leo.

Mungu anampigania katikati ya maharamia wanaoitafuta roho yake. Wamebaini Mungu yu pamoja naye sasa wameamua kumchafua. Wana CCM wasio jua vita hii nao wameanza kumgeuka. CHADEMA wanaongoza mashambulizi ya kukubomoa ila wewe mawe wanayokutupia yakusanye ujengee msingi imara.

Makonda simama imara, alikufa Amina Chifupa akafanyika sadaka kwa wapiganaji wajao. Hakika hutakufa bali utaishi na wanaokuchafua leo kama kawaida yao watakusafisha kesho.

Umeanzisha vita kali kwa maslahi ya Watanzania, usiogope mabomu, makombora ya matusi na kuzushiwa.

Dhahabu haing'ai pasipo kupitishwa motoni. Songa mbele Makonda. Walio upande wako ni wengi kuliko walio kinyume chako. Kusalitiwa ni sehemu ya uongozi.
Unamuongelea Mungu gani ambaye huwa anakuwa upande wa wanyang'anyi wa vyeti na wavamizi wa vituo vya radio? Labda kama unamuongelea yule "mungu" faru Yohana asiyejaribiwa!
 
Back
Top Bottom