Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,697
- 9,048
Katika Gazeti la Mwananchi la leo amenukuliwa Mhe. Lyatonga Mrema aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu WM enzi za Utawala wa Mzee Mwinyi. Kwamba Serikali lazima iwe na mbinu mbdala za kukabiliana na hawa wauaji ikiwemo kuwekeza kwenye Intelijensia kwa kupeleka na kupandikiza watu katika maeneo hayo ili kumbaini huyu adui ni nani. Nimeipenda sana hoja hii.
Nakumbuka enzi za Baba wa Taifa Mwl.Nyerere(RIP).Tanzania ilikuwa inasifika sana kimataifa kwa Intelijensia na ilisemekana kuwa ilikuwa ni nchi ya 3 au 4 baada ya MOSSAD ya Israel, CIA&FBI za Marekani na KGB ya Urusi(enzi hizo). Ilikuwa ni vigumu sana kwa adui kupenyeza chochote kwenye anga la Tazania bila ya kubainika. Baba wa Taifa alijua kuwekeza kwenye Intelijensia ya Usalama wa Taifa. Enzi hizo Usalama wa Taifa au Mashushu ilikuwa ni Usalama hasa na siyo kamai. Ilikuwa ni vigumu sana kumjua nani ni TISS,nani shushu na kuna watu walikuwa wanapandikizwa kwene Vijiji, Majiji,Mashuleni,Vyuoni, Mashirika ya Umma wakiishi kama wanakijiji, wakisoma kama wanafunzi au wakifanya kazi kama Wafanyakazi lakini wako kazini 24 hours na usingeweza kuwatambua!!
Ungelikuta mtu ni kichaa kabisa anaokota makopo na uchafu wa kila aina jalalani karibu na shule,mji au kijiji kumbe ana kazi maalumu. Usiku mkienda kulala yeye anabadilika toka kuwa kichaa na kuanza kazi ya kupeleka taarifa za uhakika na baada ya kitambo utasikia kimenuka!!!
Hilo jambo kwa sasa halipo. Tanzania kwa sasa hatuna TISS ya enzi hizo.Tatizo la sasa ni kwamba baada ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa Vyama vingi,vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kwa maana ya Jeshi,Polisi na Usalama wa Taifa wamegeuka kuwa ni Mashushu wa KUFUATILIA VYAMA VYA UPINZANI NA VIONGOZI WAKE kuwa vinafanya nini saa ngapi na wapi!!! Yaani Wapinzani kwa Tanzania ndio wamegeuzwa kuwa maaadui nambari moja wa Serikali. Huu ni udhaifu mkubwa sana ambao ndiyo unaligharimu Taifa. Badala ya vyombo vya ulinzi na Usalama ku-concetrate na tatizo la mauaji ya kumtafuta muuaji huko Kibiti na Rufiji wao wako busy kukamata Viongozi wa Upinzani na kuwapeleka Polisi na Mahakamani au kuwapoteza kabisa kama BEN SAANANE, this absolutely non-sense. Yumkini hata hawa jamaa wanaofanya haya mauaji huko mkoa wa Pwani wanajua udhaifu wa Serikali ya CCM!!!
Bila kubadili mbinu na kufuata ushauri wa Mrema na raia wema, Rais Magufuli atabadilisha sana ma IGP na ma RPC na mauaji yataendelea tu.Hii ni aibu kwa Serikali ya CCM ni aibu kwa nchi lakini pia ni aibu kwa Rais Magufuli ambaye ni mlinzi nambari 1 wa raia wote Mpaka sasa ni jumla ya watu 48 wamepoteza maisha(Raia 35 na Askari 13). This is very shameful!!
Nawasilisha.