Naungana na kina ZITTO umri wa kugombea urais! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naungana na kina ZITTO umri wa kugombea urais!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Mar 17, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  HIVI karibuni wanasiasa vijana, Zitto Kabwe wa CHADEMA na Januari Makamba wa CCM walichokoza nyuki na kusababisha mjadala kuhusu suala la umri wa kugombea urais Tanzania. Na kutokana na kupanda kwa joto la hisia katika mjadala wenyewe, Zitto alilazimika kuandika tamko kwa vyombo vya habari kufafanua kauli yake.

  Haishangazi kwamba Zitto Kabwe na Januari Makamba, kwa mara nyingine tena, wameibua hadharani mjadala wa suala kubwa la kitaifa kuhusu jambo wanalokubaliana licha ya tofauti za vyama vyao. Itakumbukwa pia kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, wanasiasa hao walishikamana katika kupinga posho za ziada kwa wabunge.

  Lengo la safu hii si kuwajadili Kabwe na Januari. Lengo ni kujaribu kudadisi na kujifunza jambo kutoka katika mawazo yao, mitazamo yao na mikakati yao kisiasa, ikiwamo hili linalowashangaza watu wengi kwamba wabunge hawa - mmoja wa CCM na mwingine wa CHADEMA - wanaonekana kukubaliana zaidi katika masuala mazito ya kitaifa.

  Mjadala katika vijiwe mbalimbali vya elektronik na mezani ulijikita zaidi katika kulihusisha suala la umri wa rais na kuwa na busara. Kwamba ukitimiza umri wa miaka 40 uliotajwa na Katiba kwa wagombea urais lau unakuwa umekula chumvi nyingi na kupevuka kiakili. Lakini kitu kimoja ambacho hakikujitokeza ni maswali ya kutosha ya kimantiki kuhusu hoja yenyewe.

  Kwa mfano, mosi, ni nani anayesema kwamba kila mwenye umri wa miaka 40 kwenda juu ni lazima anakuwa na busara? Kwa maneno mengine je, ni kweli kuwa viongozi wote wenye umri wa miaka 40 kwenda juu wanakuwa na busara automatically? Je, huyo Chifu Mangungo wa enzi zile na hawa Mangungo wa enzi zetu, pamoja na umri wao mkubwa, wametuonyesha busara gani katika kuhakikisha wananchi wa nchi zetu wananufaika na rasilimali walizorithishwa katika ardhi yao? Je, si kweli kwamba hili la umri mkubwa na busara ni hoja tenge isiyojitosheleza wala kushawishi?

  Pili, ni nani anayesema kinachohitajika hivi sasa katika kuendesha nchi zetu katika namna itakayotuhakikishia kujinusuru, kujihifadhi, kujiendeleza, kujistawisha na kujilinda kwa kutumia akili zetu wenyewe ni busara tu za kiongozi wa juu mwenye umri wa miaka 40 au zaidi?

  Kwa maneno mengine busara tu zinatosha kumfanya kiongozi awe na maono, dira, kipaji na uwezo wa kuonyesha njia? Kwani nchi zetu hazipaswi kuwa zinaongozwa kwa Katiba, sheria, kanuni na miongozo mingine inayomlazimisha kiongozi yeyote – bila kujali umri – asitumie utashi na hisia binafsi tu katika kuongoza taifa?

  Na je, endapo rais ataongozwa na Katiba, sheria, kanuni na miongozo mingine ya kitaasisi iliyopo itawezekanaje basi akatenda yale yatakayofanya nakisi ya busara aliyo nayo – eti kutokana na umri mdogo - ikaathiri utendaji wake?
  Tatu, je ni utafiti gani uliofanyika na kuhitimisha kwamba busara huwaingia binadamu wote wanapofikia umri wa miaka 40 tu na zaidi? Kwa maneno mengine ni nani anayedhani kwamba vijana wote ambao hawajafikia umri huu wa kirasimu uliowekwa katika Katiba hawawezi kuwa na busara?

  Lakini je, nchi yetu haina mifano hai inayoweza kutusaidia kujifunza kitu katika mijadala huu? Wengi wa viongozi walioongoza mapambano ya kudai uhuru wa nchi yetu na hata kushika madaraka ya uongozi, ikiwamo urais, hawakuwa wamefikisha miaka 40 wakati tunapata uhuru. Na je, si kweli kwamba dhamira, ujasiri na kuthubutu kwa vijana wale katika kulitetea taifa, watu wake na rasilimali zake haviwezi kulinganishwa na kitu kingine chochote vikiwamo vingi vyenye miaka zaidi ya 40 tunavyovijua leo?

  Lakini pia katika miaka ya karibuni nchi hii haijashuhudia wanasiasa vijana wa kike na wa kiume ambao hawakuwa wamefikia umri wa miaka 40 lakini walipochaguliwa kuwawakilisha wananchi kule bungeni wakadhihirisha, bila chembe ya shaka, uzalendo wao, ukali wa akili, umakini, busara na kuthubutu ambavyo haviwezi kulinganishwa na kitu kingine chochote vikiwamo vingi vyenye miaka zaidi ya 40 tunavyovijua leo?

  Na wakati mwingine – na hili nalisema si kwa kukosa adabu – je, wananchi hawakushuhudia wawakilishi wengi tu wa wananchi wenye umri wa zaidi ya miaka 40 wakisinzia na kukoroma bungeni kwa muda mrefu tu bila hata kuchangia hoja sana sana wakiamka kushabikia mambo yenye maslahi binafsi kwa kugonga meza?

  Ni dhahiri kwamba katika nchi zetu za kusini mwa Jangwa la Sahara suala la umri linaweza kuwajengea watu imani potofu endapo litatazamwa kwa jicho la kimazoea. Katika nchi zetu hizi wanaweza kuwapo watu wazima kwa kigezo cha miaka tu, lakini wakichunguzwa kisayansi ikabainika kuwa bado umri wao kiakili ni mdogo sana.

  Kwa mfano, hapa nchini kwetu karibu asilimia 40 ya watoto wenye umri wa miaka mitano kwenda chini wanakuwa na utapiamlo. Kwa maneno mengine watoto wale wanakuwa wamekosa lishe muhimu kwa makuzi ya akili zao na miili yao. Na ni hoja ya kimantiki tu kwamba ni kutokana na tatizo hili kubwa wapo watu wetu ambao wanaweza kufikia miaka 40 ya kuwepo duniani, lakini ukipiga hesabu ya lishe waliyoipata kwa miaka yote hiyo unakuta inalingana na ya kijana wa miaka 18 aliyelelewa vizuri na kula chakula bora tangu utotoni.

  Hivyo basi, kwa umri wa kuhesabu mtu anakuwa na miaka 40 na zaidi lakini umri wa kufikiri – ambao ndio unaosemekana kubeba busara - anakuwa mdogo kwa vile akili zake zilivia kutokana na utapiamlo.

  Kwa mantiki hii basi watu wanaweza tu kuamini kwamba umri wa miaka 40 ni kigezo cha kiakili cha kuamua ni nani anaweza kuwa rais makini wa nchi lakini bado wakajikuta wakishindwa kumpata kiongozi mwenye busara – walizokuwa wakizitafuta katika umri – kwa vile watampata mwenye miaka mingi ya kutosha lakini iliyoathiriwa na utapiamlo.

  Dunia tunayoishi leo inatulazimu sote kwenda mbali zaidi na haya mapokeo tuliyochukua kutoka kwa wengine bila hata kuyahoji ili kutafuta uhalali wake kwa maslahi yetu. Ni kweli kama taifa tunapaswa kukishukuru kizazi kilichoongoza mapambano ya kuwang'oa wakoloni na kujaribu kujenga misingi ya utu na misingi ya sisi kujiendeleza wenyewe.

  Kilitekeleza wajibu wake wa wakati. Lakini wakati huo huo, kizazi kipya hakina budi - kama alivyosema mwanafalsafa na mwanaharakati wa ukombozi wa Afrika Frantz Fanon - kufanya jitihada za makusudi za kuutambua wajibu wake na kuutekeleza.

  Zitto na Januari wanawakilisha kizazi ambacho, kinajaribu kuainisha jukumu lake la wakati, kinajaribu kubaini ni yapi malengo ya taifa hili kwa miaka 50 na zaidi ijayo ili kiweze kutengeneza dira makini na mikakati ya kutimiza ili kufika huko salama.

  Katika dunia ya sasa taifa hili halihitaji tena wanasiasa wanaoangalia malengo ya miaka mitano tu mbele na kuweka mikakati ya namna ya wao kuwa madarakani huku wakizingatia tu umri wao wa kuishi.

  Kama alivyowahi kusema Rais mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, kila zama na kitabu chake. Waliozichukulia kiwepesi kauli za Zitto na Januari kuhusu umri wa urais wanapaswa pia kutambua kuwa wakati ni ukuta na kwamba hizi ni zama tofauti kabisa na jana na hata kitabu kinachotumika sasa si cha karatasi tena bali ni iPad.

  Na ni dhahiri pia kuwa lipo kundi kubwa la vijana ambao wamekulia katika mfumo tofauti, fikra tofauti na mazingira tofauti. Wana matamanio tofauti, maono tofauti, ni wabunifu na wanatafuta majawabu ya matatizo yao kwa akili zao na mikono yao. Ni vijana walio na njia – na nyanja – mbalimbali za kuwasiliana na wenzao nchini na nje ya nchi katika kujaribu kuelewa na kutafuta suluhisho la matatizo yanayowakabili. Wanayo maswali mengi ambayo hayawezi kujibiwa na kizazi cha jana kwa sababu wanazungumza lugha tofauti.

  Nahitimisha kuwa katika nchi zetu hizi hizi tumeshuhudia watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 ambao wana akili kali kama wembe, wana maono na dira ya kukomboa jamii zetu kiuhuru, kifikra na kiuchumi, wanavyo vipaji wanavyovitumia kusaidia wengine, wanao uzalendo usiotiliwa shaka na wana uthubutu kama wa simba.

  Lakini pia tumewaona vijana wenye umri chini ya miaka 40 wenye sifa kama hizo hapo juu na mara nyingi wakiwa na nguvu za ziada zitokanazo na damu changa na uelewa mkubwa zaidi wa dunia ya sasa, teknolojia yake na ushindani wake. Kwa mantiki hii umri mkubwa peke yake unakosa nguvu za kuwa kigezo muhimu na makini katika kumpata rais bora wa nchi yetu.

  Tatizo ambalo linapaswa kuwa kiini cha mjadala huu ni jinsi ya kuwapata Watanzania wenye sifa hizo hapo juu - bila kujali kama wamefikia miaka 40 au ni vijana kama Halima Mdee - ili watuongoze katika namna ambayo kila mmoja wetu, na sote kama jamii, tunaweza kufikia ndoto zetu.

  NUKUU:urais 2015 ni zamu ya vijana - JK

  Nawasilisha kimtindo!
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tuambie kile kilicho 'behind the scene' hadi ushabikie fikra hizi duni za JK,Zitto na wengineo.
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,681
  Trophy Points: 280
  umri uliotajwa katiba ya sasa naunga mkono! 40yrs ni umri muafaka.kwanza huwa siangalii umri na uongozi! Mfano ktk hao vijana nani hata sasa ni zaidi ya Salim.A.Salim na Dr Slaa? Miaka 40 unakuwa umepevuka bwana!
   
 4. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,681
  Trophy Points: 280
  Hata huyu Zitto umri wake unavyosogea unaona anavyokomaa! Mikiki ya Urais si mzaha wakuu,kuwa Amri Jeshi ina maana kubwa sana lazima uwe umepitia vitu fulani ktk maisha na hata kuishi na binadamu wenzako kwa muda mrefu unajifunza kitu.Zipo nafasi hata ukiwa na miaka 28 unaweza kufanya kama una karama ya uongozi lakini si Urais! Tusitafute justification eti kuna watu wenye umri huo hawana busara! Hapa tunajadili mtu mwenye sifa zote za uongozi alafu walau akafikisha 40 yrs atakuwa amekomaa zaidi.tunapojadili umri wa mtu kugombea Urais tujue tunazungumzia mtu mwenye sifa muhimu za uongozi alafu kuanzia hapo tupime na umri!! 40 years is very reasonable age kwa nchi yetu na mazingira yake plus mfumo wa elimu yetu!
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,681
  Trophy Points: 280
  Mkuu maneno ya JK ni vita tu ya kisiasa! Mbona yeye kawa Rais? Wakati anagombea alikuwa kijana? Kwahiyo Membe kwa mfano ni kijana kama akina Zitto na Kafulila aliokuwa anawajaza ujinga for political enger?
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,681
  Trophy Points: 280
  Ndio maana kwenye Uspika tuliambiwa sasa zamu ya wanawake fursa sawa kwa wote! Unapendelea mtu alafu unasema fursa sawa!! Wanasiasa wetu wengi wamejaa njaa si ya kuleta maendeleo bali ile ya tumboni haswa!
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwa sababu mimi sio mzee kama wewe,nimechoka kutawaliwa na vijana nataka na sisi vijana tugombee nafasi hiyo ya juu ili tulete mabadiliko ya kweli,tunakuja na mawzo mbadala wazee mtupishe tutaandamana nchi nzima ikibidi tena bila kujali itikadi za vyamakudai umri upunguzwe
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,681
  Trophy Points: 280
  Mawazo mbadala yanaletwa na umri wa mtu au uwezo wa mtu?
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sipingi hoja ya kuwapa nafasi vijana kwenye safu ya uongozi, lakini sikubaliani kabisa na tabia ya vijana kuwa madalali wa 'wazee'. Hii hoja ya ujana kwenye urais ni mkakati wa mtu. Tumesikia ajira kwa vijana, sasa tunasikia rais kijana! Mwaka 2005 tuliimbiwa sana mashairi ya ujana sasa yametukuta! Leo anatoka mtu huko na kutuimbia mashairi yale yale kama sio kutufanya sisi watanzania mazuzu ni nini?

  Urais uende kwa mtu mwenye nia, uwezo na uthubutu wa kupambana na uporaji wa rasilimali za nchi hii. Awe na umri wa miaka 20 au 90, au hata 120 cha muhimu ni uwezo wake katika kupambana na matatizo na wala sio umri. Sitta anafanya mambo makubwa huko Zambia na umri wake tunaujua. Binafsi I prefer Zitto wa 2007 kuliko huyu wa 2012. Makamba sina hata la kusema! Sorry folks!
   
 10. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kwanini uziite fikra duni kaka hebu fafanua....!!!!


   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo busara za Mtanzania zinakuja pale anapokuwa amefikisha umri wa miaka 40? Je,akina Mkapa -KIWIRA,ANBEN,EPA,MEREMETA na Akina JK-DOWANS,RICHMOND walikuwa wamepevuka pia ? Hizi busara za ANBEN,KIWIRA,RICHMOND ndizo zinazopatikana unapokuwa umefikisha miaka 40? Vipi akina Hussein Mwinyi -IPTL?
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Binafsi mimi ni kijana sana lakini nadhani muda uliopo kwenye katiba ya nchi miaka 40 ni muafaka kwa sasa.
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,681
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio tunapokosea mkuu wangu,kwahiyo kesho Zitto akiwa Rais alafu akaharibu tushushe umri hadi miaka 18? Miaka 40 naamini si pabaya kwa mtu mwenye sifa ya uongozi kuwa Rais! Narudia tena kwa mtu mwenye sifa ya uongozi!! Mimi pia kijana na naona ninavyojifunza na kukomaa umri unavyokwenda! Tusitumie failures kujustify kupinga jambo lilokuwa jema mkuu wangu!
   
 14. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni nini katika kipengele hicho cha katiba mpaka washupalie hili?, Je nchi haina watu wanaofaa kuwa Rais wenye umri huo? kiukweli mi sioni kama hoja hii ni ya msingi hata kidogo kwani sioni kinachopungua!,

  Japo unasema lengo sio kuwajadili kina zito na Makamba Jr, lakini ni muhimu kuwajadili kwani malengo yao ya kugombea yanafahamika, kwa hiyo hili ni la mtazamo wa kibinafsi zaidi kuliko wa kitaifa kwa maana ya faida ya kizazi kijacho.
   
 15. Ambrose Nshala

  Ambrose Nshala Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazo la umri muafaka wa kura Rais wa nchi mimi naliangalia kwa tofauti kidogo. Kwanza kabisa naamini Tanzania inahitaji Rais shupavu, mwenye uelewa mzuri wa masuala ya kiuchumi na kisiasa na mwenye uthubuti wa kufanya maamuzi yenye lengo la kuwanufaisha wengi hata kama maswahiba wake wachache hawatafurahi.

  Tunataka Rais wenye uwezo na busara ya kupambana na changamoto zisizo tabirika na kufanya maamuzi muafaka.

  Tunahitaji Rais ambaye anajua ana dhamana ya kuwalinda na kusimamia ustawi wa jamii nzima na sio kuwa kibaraka wa wachache.

  Na kwa kutazama historia fupi ya uongozi wa Tanzania na kwa mapana zaidi katika historia ya jamii mbali mbali ulimwenguni kote, tumeona kuwa viongozi shupavu wamekuwa wakitokana na lika mbali mbali, vijana, watu wa makamo na wenye umri mkubwa.

  Kwa ufupi naweza sema umri sio kigezo cha uongozi bora. Kama kijana anaona anauwezo wa kuwa Rais wa nchi..na atuonyeshe kama anaweza. Kama mwanamke anataka kuwa Rais basi atuonyeshe....kama mzee anaweza naye aje mbele na atuonyeshe. Kinachohitajika kwetu sisi ni UWEZO NA SIO UMRI.

  Katiba mpya iondoe kigezo hicho....kama mtu anaweza kupiga kura basi aweze pia kupigiwa kura kwa nafasi yoyote. Kama anauwezo na ameonyesha, na kama wapigakura wataridhika...basi atashinda!!!

  UMRI wala JINSIA SIO KIGEZO......TUNATAKA UWEZO.

  Naomba kuwasilisha.
   
Loading...