Naunga mkono wazo la Uzalendo lililotolewa na Rais kuwa umesomeshwa na Serikali basi nenda kawatumikie Wananchi

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
UKISOMESHWA NA SERIKALI,NENDA KAWATUMIKIE WATANZANIA.

Leo 19:10hrs 30/01/2021

Serikali inakupa full sponsorship ya utofauti exceptional for unique medical courses mfano areas of specialization kama Neurosurgery, Kidney Transplant,Heart surgery,kwa gharama kubwa kama Mtumishi wao unamaliza masomo baada ya masomo unaamua kuhamia hospital binafsi bila kujali pesa nyingi za walipa kodi zilizowekezwa kwako,hospital za Serikali kupata huduma Daktari bingwa gharama ni chini ila huko kwenye private hospital kupata huduma ya Daktari bingwa gharama ni kubwa kweli na ndio wanapopata pesa ya kukuongezea kukulipa vizuri ewe Daktari Bingwa uliyekimbia hospital ya Umma na kwenda hospitali binafsi ukisaka maslahi,lakini fahamu kwamba unawadhulumu Watanzania waliokusomesha kwa kodi zao,

Mwenye hospital binafsi anamfanya bidhaa Daktari bingwa aliyesomeshwa na Serikali anapandisha bei kwenye hospital yake dhidi ya watanzania ambao pesa zao za kodi ndio zimesomesha huyo Daktari,kwa ufupi huyo mwenye private hospital anakuwa ameigeuza "Public Asset" kuwa "private asset" kwa maslahi yake binafsi,huku ni kutowatendea haki Watanzania,Hivyo naunga mkono maelezo na maelekezo ya Mh Rais kuwa huyo mwenye private hospital asomeshe specialist wake kisha aweke gharama kubwa kuonana na wagonjwa badala mtindo wa sasa unamchukua specialist aliyesomeshwa na Serikali kisha unaweka gharama kubwa kuonana na wagonjwa ambao ndio hao hao waliomsomesha huyo specialist kwa gharama kubwa kupitia kodi zao akiwa Mtumishi wa Serikali,

China wakati wanaendelea hiyo option ya kufanya kazi hospitali ya binafsi haikuwepo kabisa wakati umesomeshwa na Serikali haikuwepo hata sasa haipo,Hii inatakiwa iwahusu wanafunzi wote wanaosomeshwa au kupewa mikopo na Serikali,Wanafunzi wote wanaosomeshwa na Serikali waandikiwe mikataba ya kufanya kazi Serikalini hata kama ni kazi za ualimu,hivi sasa sekta nyingi za binafsi hapa Tanzania zinasomesha Wanafunzi kwa mkataba na wakimaliza wanaitwa Graduate Trainee na wanawajibika kwenye kampuni hiyo iliyomsomesha kwa mujibu wa mkataba wake,

Marekani pamoja na uhuru wanaousema na maendeleo yao,lakini huwezi kusomeshwa na Serikali halafu uende kufanya kazi kwa mtu binafsi kisa anakulipa pesa nyingi,hiyo haipo,Pengine kazi za kawaida tu kama kuendesha lori,hata kazi hiyo nayo kuna baadhi ya kampuni zikikulipia mafunzo na kupata leseni yake wanakulazimisha kwa mkataba ufanye nao kazi uendeshe malori yao kwa mshahara wao kwa muda fulani kama miaka miwili au zaidi,kwa hiyo ndugu zangu hakuna cha bure,upatapo fursa ya kusomeshwa na Serikali basi tambua ya kwamba umechagua fungu la kuwa Mzalendo kwa nchi yako daima,

General Medical doctors wenye degree moja wa kawaida hawana biashara kubwa,Wenye private hospital wanataka madaktari Bingwa waliosomeshwa kwa gharama kubwa na kuwageuza bidhaa za Ulanguzi,Mh Rais anaongelea madaktari bingwa waliosomeshwa na Serikali kwa gharama kubwa sana,Mfano wale wa Kidney Transplant pale Muhimbili ni wapya ukianzisha hospitali binafsi kisha unafanya Kidney Transplant bei kubwa sana unawachukua wote wa pale Muhimbili maana utakuwa na uwezo wa kuwalipa sababu bei zako kwa wagonjwa ni kubwa,Sasa Ulanguzi uko hapa,wakati hospital za Umma wanatoa huduma,hospital binafsi wao wanafanya biashara,hivyo ni ngumu kumshinda Mfanyabiashara anaweza kuchukua madaktari Bingwa wote kisha huduma zikawa bei juu hao,

Hospital binafsi ni Wafanyabiashara kama wafanyabiashara wengine,wanaangaika biashara zaidi,wapo wengi si Tabora tu wengi wenye uwezo wa public hospital watapata wapi huduma pale hospital binafsi inapomchukua mtaalam wa Serikali aliyepewa full government sponsorship akiwa Mtumishi wa Serikali ili aje awape huduma Wananchi wa kawaida wa Tabora kumbuka hospital binafsi anamchukua baada ya uwekezaji wa Serikali kwa gharama kubwa kisha anawalangua Watanzania kuwatibu kwa bei kubwa,hapa ndio penye tatizo Serikali isomeshe kwa gharama kubwa kwa ajili ya Wananchi halafu mlanguzi hospital binafsi amchukue kwa biashara yake binafsi,

Ndugu zangu hivi tunafikiri Serikali inashindwa kuongeza gharama ili ziwe kubwa kama hospitali binafsi!!?? Serikali inajua ina Wananchi wenye uchumi tofauti lakini wote wanatakiwa kupata huduma za madaktari Bingwa ndio maana inawasomesha watumishi wake kwa gharama kubwa sana kupitia kodi za Watanzania ili Daktari Bingwa aje kuwatumikia Watanzania wote,Kwenye health sector kumuona specialist kuna gharama sana kuanzia consultation hadi treatment kuna special cost unalipa, Serikali inaamua kusomesha Madaktari Bingwa ili waje watoe huduma ya afya bure ama kwa pesa kidogo,Sasa Serikali inatumia gharama kubwa kumtengeneza specialist wa Neurosurgery au Kidney Transplant kisha wewe unamlangua kwenye hospital binafsi kwa gharama kubwa dhidi ya walipa kodi waliomsomesha!!?

Nimalizie kwa kuunga mkono wazo la Uzalendo lililotolewa na Mh Rais kuwa umesomeshwa na Serikali basi nenda kawatumikie Wananchi,sio kununuliwa na hospitali binafsi halafu hospital binafsi inapandisha bei na kusema tunae Daktari Bingwa hapa wakati kasomeshwa na Serikali kwa ajili ya Watanzania, Serikali inasomesha Madaktari Bingwa ikiwa na lengo zuri,ili kila Hospitali iwe na madaktari bingwa wa fani nane,fani hizo ni pamoja na Daktari bingwa magonjwa ya uzazi na wanawake , Watoto, magonjwa ya ndani, upasuaji, upasuaji wa mifupa,daktari wa huduma za dharura na magonjwa ya ajali.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Mbona haieleweki, tunaomba mwongozo wa huyo daktari ili ieleweke kosa lipo wap...? Ni specialist au ni Dr wa kawaida ? Mkataba wake na serikali ukoje kiutumishi ?

Alipoamua kufata maslah pengine aliondoka kinyemela au alifika Kwa mwajiri anamwambia anaquit job? Huo mkataba na serikali kuna vipengele serikali imekiuka na kumfanya Dr ajiondokee zake ? Ni lazima Dr afanyie kazi hospital ya serikali tuuu?

Kama ni mkopo wa serikali alikuwa analipa kama kawaida au Alisitisha kulipa baada ya kutimkia private?

Haya maswali tukiyaelewa tutatoa hukumu vizur , Ila inavyoonekana kuna chance ndogo Sana Kwa Dr kuenenda kinyume na Serikali hii ya kibabe ..navyoonekana 90% ni makosa ya serikali yaliyomfanya ajiondokee.
 
Naunga mkono hoja kama hutaki kubanwa na masharti ya serikali mzazi wako akulipie uwe free anytime kuacha kazi na kwenda kokote sababu investment ya serikali kwenye elimu yako ni zero

Ushauri wangu kwa wazazi hasa wanaosmesha sekondari private hata iwepo opportunity ya mikopo asilimia 100 msikubali watoto wawe free mbele ya safari kufanya kazi sekta binafsi au serikali na wawe free kuacha kazi anytime kutafuta green pastures sababu serikali haikuchangia chochote elimu ya mtoto
 
Kwani ukiwa hospital binafsi unawatumikia wanyarwanda?

unajua sana kujipendekeza kwa wanaume, na ndiyo maana ukapewa kura mbili.

Mpaka unakufa hutapata teuzi, nakuapia kwa Mungu.
Naungana na mengi ya JPM ila kwa hili nasema hapana maana hizo hospitali na hata mashule yalianzishwa ku complement juhudi za serikali. Hivyo daktari akiwa private anawatumikia watanzania. Tungalihoji iwapo kama angevuka mipaka ya nchi
 
Back
Top Bottom