Naunga mkono Watoto wa vigogo kupewa ubunge na teuzi CCM. Kinachotakiwa ni Watu watoke CCM wakaunge Juhudi Upinzani na siyo kinyume chake!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,854
141,792
CCM imeliongoza taifa hili kwa zaidi ya miaka 60 kuanzia enzi za Tanu na ASP hadi sasa.

Ni ujinga kusema mtu anatoka upinzani kuja kuunga juhudi CCM kwa sababu CCM imekuwepo miaka nenda rudi na ni ile ile, waliounga juhudi ilikuwa ni wakati wa kudai Uhuru kutoka kwa mkoloni mweupe yaani mwingereza.

Waliounga Juhudi wakati huo ndio hao watoto wao leo wanakula mema ya nchi, sasa kuna nongwa gani?

Nimemkubali sana Dr Slaa aliposema tangu ajiuzulu ukatibu mkuu wa Chadema hajajiunga na chama kingine cha siasa.

Huo ndio msimamo wa kweli

Juhudi xa CCM zilikuwa ni kutuletea Uhuru na walishafanikisha.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa hiyo aliteuliwa kuwa balozi akiwa Hana chama, je na wewe unakubaliana naye? Siyo kwamba aliambiwa atupe nyavu bahari, amfuate yeye?
 
CCM imeliongoza taifa hili kwa zaidi ya miaka 60 kuanzia enzi za Tanu na ASP hadi sasa.

Ni ujinga kusema mtu anatoka upinzani kuja kuunga juhudi CCM kwa sababu CCM imekuwepo miaka nenda rudi na ni ile ile, waliounga juhudi ilikuwa ni wakati wa kudai Uhuru kutoka kwa mkoloni mweupe yaani mwingereza.

Waliounga Juhudi wakati huo ndio hao watoto wao leo wanakula mema ya nchi, sasa kuna nongwa gani?

Nimemkubali sana Dr Slaa aliposema tangu ajiuzulu ukatibu mkuu wa Chadema hajajiunga na chama kingine cha siasa.

Huo ndio msimamo wa kweli

Juhudi xa CCM zilikuwa ni kutuletea Uhuru na walishafanikisha.

Maendeleo hayana vyama!
Dr Slaa ni mwanachama wa vyama viwili ccm na Chadema, na kadi zote mbili anazo, anawalaghai watu wajinga na wasiojielewa.

Hata Simon Sirro leo atakwambia hana chama akistaafu usishangae anagombea ubunge kwa tiketi ya ccm na kadi yake ni ya mwaka 1977.
 
Back
Top Bottom