Naunga mkono vyombo vya habari kunyimwa haki ya kuripoti matukio ya vyama vya upinzani

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,326
Hata ningekua mimi ndio kiongozi wa nchi hii aliye malizamuda wake wa kipindi cha kwanza halafu nione wananchi wasivyo na shukrani, kqa kuwshabikia vyama vya upinzani, ningezima kabisa TV na mitandao ya jamii.

1. Nimejenga SGR
2. Nijenga hospitali na vituo vya afya bora
3. Nimejenga uwanja wa ndege nyumbani kwangu Tocha..
4. Nimepiga kampeni pekee yangu kwa miaka mitano
5. Nimenunua ndege ambazo pia zimesaidia kuleta tiba ya corona toka madagasca..

Haya yote eti watanzania wanajifanya hawayaoni..

Kwa halinilivyo jingezima hadi TBC maana huu ni utomvu wa nidhamu na unatakiwa kukemewa kwa nguvu zote.

Hivyo Watanzania tuelewe na tuzikubali sababu ambazo zinaganya kiongozi achukue maamuzi haya kwa sababu inauma sana.

Ni sawa na demu umemsomesha kisha anakuja pigwa mimba na bodaboda..

Inauma
 
Mwenyewe anatakiwa kutambua na kuzisifu kwanza kazi ambazo tumezifanya.. anataka kusema miaka mitano hatuja fanya kitu?
Hofu ya nini?
Kwanini mnamuogopa Lissu?
Kwanini mkisikia jina la Lissu mnakosa raha, mnaumia, mna tetemeka?
 
Ila kweli tunamuonea jamaa lakini Kibinadamu hata kama ungekuwa ni wewe ungezima vyote. Umefanya yote hayo lakini bado wananchi wanamshabikia Lissu ambaye kwanza licha ya kutofanya jambo lolote lakini oia hakuwepo nchini.

Mnyonge mnyongeni......
 
Nadhani kilichojenga ni fedha za wananchi kupitia kodi zao na si pesa ya mtu binafsi toka mfukoni mwake...lakini je vp na deni la taifa kuzidi kupaa?

Jr
Haa kumbe ni fedha zetu za kodi kwakutumia akili zangu za kuvukia barabara nikajua Bunge kazi yake ni kutunga sheria tu haipitishi bajeti ya serikali, maana huwa nawasikia mawaziri wote wakimtaja Rais kutoa fedha kila nikisikiliza kwenye vyombovya habari kumbe huwa wanajitoa ufahamu?
 
Halafu wewe juzi nimekuona kwenye bombadier una piga self..
Sasa Upigiwe kura na Stiegersgorge, standard gauge , flyover, Madaraja na bombadier ndio zikupigie kura wewe si ndio umeona za muhimu kuliko watanzania?
 
Back
Top Bottom