Naunga mkono Uwanja wa Ndege wa Chato. Una justification, utakuwa kama Ggabolite au Yamoussoukro. Watalii watamiminika!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Wanabodi,

Tangu kupatikana kwa taarifa ya kutelekezwa kujengwa kwa uwanja wa ndege wa Bukoba, eneo la Omukajunguti na badala yake sasa uwanja huo unajengwa Chato, kumetokea pingamizi kadhaa kupinga kujengwa kwa uwanja huo Chato kwa kutumia costs benefits index, hivyo mimi naunga mkono ujenzi wa uwanja huo wa ndege wa Chato, una Justification fulani! Mji wa Chato, baadae unaweza kuja kuwa mji wa Ggabolite, au Yamoussoukro, watalii watamiminika kula raha Chato na kushuhudia miundombinu ya kupendeza, hivyo naunga mkono uwanja wa ndege wa maana ujengwe tuu Chato.

Justification why not Omukajunguti
Imetolewa justification kwa nini uwanja wa ndege wa Bukoba, haujengi tena eneo la Omukajunguti kwa maelezo kuwa eneo hilo ni swamp area! Excuse hii ni very lame excuse, kama watu wanaweza kujenga hadi baharini kwa land reclamation, what is swamp area kama mjenzi anajua anachokifanya ikiwemo kufanya elevation na kuweka vizuri water flows? Watu waende Holland wakaone nchi iko under sea level, watu wamefanya land reclamation na wamejenga. Kinachotakiwa ni kujenga good water flows tuu, hivyo argument ya swamp area doesn't hold water! Ile hoja ya kuogopa kulipa fidia wageni wengi, ni childish, assence ya fidia sio land bali ni development done on that land. Kama kuna mgeni mmemuacha hadi amejenga, then anastahili fidia. Hivyo hoja ya fidia nayo ni hoja tuu ya nguvu lakini haina nguvu ya hoja.

Justification Why Chato International Airport
Japo sijabahatika kuzisikia hoja kwa nini ni Chato International Airport, lakini mimi nimebahatika kufika Chato ile ya jamaa yangu fulani akiwa waziri, ndio alikuwa akimiliki the best hotel in town ya Chato ile. Kuna wakati nilikuwa na assignment ya mwezi mzima Biharamulo, lakini niliishi Chato, nikapanga kwenye hiyo the best hotel in Chato, ni hotel ya vijumba jumba vya detached suites.

Kama Akiwa Waziri Tuu Alishusha The Best in Chato, Sasa Hivi Alivyo, Atashusha nini?
Nimeteremka tena Chato ya sasa, na kiukweli Chato inabadilika kwa speed ya umeme, au speed ya ajabu, vitu vinaota kama uyoga!, na kuna kitu moja kimeshuka kwa kupanda juu kama mbingu!, hii kitu ni kitu ya ukweli, sii mchezo!. Sakafu tuu ni marble na granite, sofa za rooms ni pure leather!, hadi Free WiFi ya 4G mjini Chato!, kwa mambo kama haya na kwa mwendo kama huu wajameni, uwanja wa kimataifa Chato ni halali na unastahili!. Kama haya tunayoyaona ni ya hii miaka mawili tuu, then kufikia miaka 10, Chato itakuwaje?. Mimi naamini Chato itakuwa an international city kama Ggabolite ya Mabotu Sesse Seko au Yamasoukro ya, Félix Houphouët-Boigny.

Utalii Sio Natural God Given Only, Hata Man Made
Wengi wanadhani vivutio vya utalii ni lazima viwe natural God given only, kama mbuga za wanyama, milima, mito na mabonde tuu, sii wengi wanajua kuwa tourism attractions zinaweza kuwa man kama mambo ya kale, au made kwa kujenga miundombinu ya kufa mtu ya kuvutia watalii, kuna mji wa Sun City South Africa, au kuna mamia ya watalii wanamiminika kushuhudia a Catholic minor basilica dedicated to Our Lady of Peace in Yamoussoukro, the administrative capital of Côte d'Ivoire (Ivory Coast). Disney Land ni manmade, kuna watu wanakwenda Egypt kushuhudia Pyramids, watu wanakwenda Paris just to see ile Eiffel Tower. Watu wanakwenda London kuona the London Bridge, Italy kuona the Lening Tower of Pisa, watu wanakwenda Iraq kuangalia the Hanging Garden of Babylon, etc etc, nasi tuta create kitu, watalii wanamiminika tuu Chato. Mfano tukijenga zoo na kuwaweka the big five, tumemaliza.

Kwa Nini Wanabeza Chato?
Hivyo kuna wengi wanabeza uwanja wa Chato. kwa kijicho tuu cha wivu, wana moyo wa kwanini na sio wivu wa maendeleo, the real and true charity, begins at home, mimi naunga mkono 100% kwa 100%, kama umejaaliwa uwezo, anza kwanza kujenga kwako, ndipo ukajenge na kwa wengine. Pia kuna uwezekano hata huu uwanja wa Chato, wanao beza ni wasiojua kutazama mbali, kwa sisi tuliofika Chato, na kuona vitu vinavyopanda, na hii ni miaka miwili tuu, then amini usiamini, baada ya miaka 10, watu watakuwa wanamiminika Chato, kuliko Mikumi!

Naunga Mkono Uwanja wa Chato, Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, Walifanya Makosa?

Hivyo naunga mkono ujenzi wa uwanja wa Chato. Kiukweli Nyerere alifanya makosa kuhusu Butiama, Mwinyi akafanya makosa kuhusu kwao, Mkapa alifanya makosa kuhusu kwao, Kikwete amefanya makosa Msoga, Magufuli asifanye kabisa makosa Chato, miundombinu ya kuifikia Chato ikikamilika, kitu cha kuitumia miundombinu hiyo kitaibuka.

Chato oye!.
Mungu ibariki Tanzania.
Jumapili Njema.
Paskali
cc. britanicca
 
Hahaha kweli sio watu wengi wanaifahamu fasihi. Ili uelewe unapaswa kuwa na uelewa kuhusiana na hadithi zinazojulikana kama Istiara. Tofauti na hapo utakuwa kama wakoloni walioichapisha riwaya za Kusadikika au Kufikirika bila kujua kuwa hayo yasemwamyo humo ni kuhusu wao wenyewe. Wakampa hadi tuzo mwandishi. Sitashangaa CCM pia ikimpa tuzo mwandishi huyu kwa kuwasifia!
 
Kuweka rekodi sawa, Mkapa hakufanya makosa kuhusu kwao, alijenga daraja la Mto Rufiji.

Ila Paskali nimekuelewa sana kwenye bandiko lako, imenikumbusha novel moja maarufu iitwayo " The Beautyful Ones Are Not Yet Born " iliyoandikwa na Mwanafasihi nguli kutoka Ghana Ayi Kwei Armah
 
Back
Top Bottom