Naunga mkono tarehe 3/10/2011, KUVAA NGUO NYEUSI

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Samahani pengine hii imeshakuwepo humu ndani ya JF ila mimi nimepokea sms tano sasa kuhusu
kuvaa nguo nyeusi mnamo tarehe 3 wa 10 mwaka huu.

SMS inasema kuwa ni kupinga au kuiambia serikali kuwa tunapinga MGAO WA UMEME, RUSHWA, UFISADI nk.
Nimefurahi sana na nadhani hapo hakuna mabomu ka ya Arusha.

Nawasihi ata wale wasio na nguo nyeusi wavae vifua wazi kwakuwa sisi ni weusi labda wachache tu na waliojichubua.

Tujulishane kwa wingi na tutende kwa vitendo. Tupambane tutashinda.

ARUTACONTINUER
 
Nitavaa pia. Shati na suruali nyeusi tayari ninazo, natafuta kufuli nyeusi tii.
 
Mctake kuwaharibia maisha wadogo zenu wa form IV..tar 3 oct ndio wanaanza necta hvo hawataruhusiwa kufanya mtihan na nguo nyeuc..na hata kuvaa nguo nyeuc czan km n suluhisho kwa kuwa serikal inafahamu kuwa 2mechoka na matatzo ya umeme...suluhsho n kuumiza kichwa chako cha kutafuta solutn zen peleka kwa ngeleja km wazo n zuri na linatekelezeka 2takuwa 2mekomboka co kuvaa miguo mieuc km wafiwa afu kichwan ZERO hamna haja
 
Naunga mkono,lakini suala la kubaki kifua wazi kwa wale ambao hawana nguo nyeusi sikubaliani na wewe!
 
Naunga mkono hoja ila kuhusiana na kuingilia na siku wadogo zetu wanaanza paper ya form four itakuwaje?
 
Nimeipata ktk sms pia. Siku hiyo itakuwa pimajoto ya kutufahamisha mwamko wa waliochoshwa na maovu ya serikali yetu wakati tunatafakari hatua zaidi kwa ajili ya cku zijazo. Panga pangua mabadiliko ni lazima. Kikombe cha uovu cha mafisadi kimefurika. Hasira ya mola iko juu yao. Usemi wa kiitalia wa Vox Populi Vox Dei utakuwa kweli.Niseme na Mtikila-Saa ya ukombozi ni sasa.
 
Labda niulize kwanini wamechagua tarehe 3? Mi naona mbali sana maana sasahivi hali inazidi kuwa tete hali ni mbaya zaidi kwanini tusiamue hata kesho? Mi nimeanza leo kabisa kuvaa nyeusi maana nyumbani kwangu walinirudishia umeme masaa 4 tu tena usiku wakati nimelala halafu wakauchukua tena. Wiki iliyopita tulipigwa changa la macho tulivyodanganywa adha itapungua badala yake ndio imezidi
 
Ukianza kesho mtakuwa 10 tu na tukio halitakuwa na mshiko. Kwanza linatangazwa kwa sms na email. Tunahitaji watu wengi wapate habari ili washiriki. Nilipopata sms nilidhani mzaha. Nimeikuta humu nimeona umma wanamaanisha.
 
Ukianza kesho mtakuwa 10 tu na tukio halitakuwa na mshiko. Kwanza linatangazwa kwa sms na email. Tunahitaji watu wengi wapate habari ili washiriki. Nilipopata sms nilidhani mzaha. Nimeikuta humu nimeona umma wanamaanisha.

Haya itabidi siku hiyo nivae tena, maana mwenzenu nimechoka kweli kweli na hii nchi umefika wakati wa kufanya maamuzi wala tusiogope maana tunapelekeshwa ovyo na wachache
 
Thanks kwa taarifa, shati jeusi ninalo nasubiri tu tarehe. Na nashauri utaratibu huu ungekuwa wa kudumu namaanisha itafutwe siku labda tuseme kila jumamosi ya kwanza ya mwezi kufanya protest hii
 
Mi nitavaa full black na bendera ndogo ya Tanganyika nitachomeka mfuko wa shati ining'inie, hapo vp?
 
nawaambia mafisadi, watawala wabovu. MENE MENE TEKEL PERSIN (ufalme/utawala wenu umepimwa na umeonekana umepungua). WALAHI mmeanza kuporomoka. OLE wenu. Maana hamwezi kushindana na nguvu ya Umma, FFU haitambi mbele ya Umma, hata Dr. Bana alitamka hilo.Ni nani atakayewaokoa ninyi na wanenu? Angalieni wana wa Gadaffi!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom