May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,818
Mimi ni miongozi wa Wazazi nisiyefurahishwa kabisa na namna tunavyowachosha Watoto wetu kwa ratiba ngumu wakati mwingine kuliko hata tulizonazo sisi Watu wazima.
Kuhusu likizo nadhani twaweza kuja na namna nyingine ya kwenda na Watoto wetu hawa bila kuendelea kuwaumiza...maana pia kama lengo kuu ni kuwapa Watoto muda wa kukaa na Wazazi tujiulize ni Wazazi wangapi wanapatikana nyumbani zama hizi? sanasana Watoto hawa huishia kushinda tu na kina Dada wa Kazi au Kaka wa kazi.
Au la watashinda kutwa nzima wakiangalia TV hapo kwao au kushinda kwa majirani...au kutumia simu zitakazopatikana kwenye maeneo yao bila Msimamizi...hivyo bila ya shaka shuleni bado kutabaki kama sehemu salama zaidi kwa uangalizi kuliko hata nyumbani.
Kwa kipindi hiki cha likizo Watoto waruhusiwe kwenda hata shule zilizopo jirani na wanapoishi, ila kwa wale ambao bado watamudu kutumia usafiri kuzifikia shule zao ni sawa. Watoto watoke nymbani saa nne na warudi saa tisa. kwangu ni kheri kuliko wakishinda nyumbani siku nzima.
Kwa namna ile ile wanavyolipia tuition Watoto wahudhurie mashuleni na wafundishwe stadi za maisha za kawaida tu zisizowapa stress, mafundisho kama ya kiimani, michezo, kuimba n.k. kabla ya kurudi nyumbani na kushiriki kazi ndogondogo za nyumbani.