Naunga mkono Mohamed Dewji kuishukuru serikali na vyombo vyake vya usalama!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,060
22,755
Wakati mwingine tuwe tunatumia akili kidogo, Mohamed Dewji kawashukuru waliomteka kwa kuamua kumuachia usiku wa manane wakati tuliokuwa tukisikitika, tuliokuwa tukiomba, tuliokuwa tukiliaa na tuliokuwa tukipiga makelele tumelala. Mohamed Dewji hana muda wa kuwashukuru binadamu wanyonge kama sisi tulioumbwa kwa udongo.

Sala zetu, vilio vyetu na makelele yetu hayakuweza kufanikisha kupatikana kwa Ben Saanane, Azory na ndugu zetu lukuki waliopotea...iweje kwa Mohamed Dewji? Maombi yetu, masikitiko yetu na vilio vyetu havikuwezesha kupatikana kwa wauaji waliommiminia risasi zisizo na hesabu Mbunge wa Singida Mh. Tundu Antiphas Lissu kwa nia ya kumuua.

Mohamed Dewji hana haja ya kutushukuru wala asithubutu kutushukuru, awashukuru watekaji wenye roho nzuri waliomuonea huruma hadi kapatikana mzima wa afya bila hata kuhitaji uchunguzi wa afya yake, nashauri familia yake iwape hao watekaji zile trilioni kama asante...Kweli Tanzania ni zaidi ya tunavyoijua, pole sana Mohamed Dewji!
 
Wakati mwingine tuwe tunatumia akili kidogo, Mohamed Dewji kawashukuru waliomteka kwa kuamua kumuachia usiku wa manane wakati tuliokuwa tukisikitika, tuliokuwa tukiomba, tuliokuwa tukiliaa na tuliokuwa tukipiga makelele tumelala. Mohamed Dewji hana muda wa kuwashukuru binadamu wanyonge kama sisi tulioumbwa kwa udongo.

Sala zetu, vilio vyetu na makelele yetu hayakuweza kufanikisha kupatikana kwa Ben Saanane, Azory na ndugu zetu lukuki waliopotea...iweje kwa Mohamed Dewji? Maombi yetu, masikitiko yetu na vilio vyetu havikuwezesha kupatikana kwa waliommiminia risasi zisizo na hesabu aliyekuwa Mbunge wa Singida Mh. Tundu Antiphas Lissu.

Mohamed Dewji hana haja ya kutushukuru wala asithubutu kutushukuru, awashukuru watekaji wenye roho nzuri waliomuonea huruma hadi kapatikana mzima wa afya bila hata kuhitaji uchunguzi wa afya yake, nashauri familia yake iwape hao watekaji zile trilioni kama asante...Kweli Tanzania ni zaidi ya tunavyoijua, pole sana Mohamed Dewji!
Aiseee hatari sana
 
Muungwana ni vitendo, amefanya vyema kushukuru kwani hata neno la Mungu linasema shukuruni kwa kila jambo!
 
Bongo bwana eti waliokuteka wanakuachia siraha zote hizo na wewe huwafanyi kitu unawaangalia tuu huku wakikimbia kwa miguu maana gari lao ni moja tu Surf waliyokua wanazunguka nayo na siraha ndani ya Jiji la dar es salaam...

Baadae wakataka kulichoma moto gari wakashindwa..hakuna kitu rahisi kama kuchoma moto gari ila hao watekaji walishindwa...
 
Nilijua, hii heading ni 'bait'! Hivi kweli 'mtekwaji' hakutushukuru sisi wengine tuliokuwa tunamuombea arudishwe salama?
====
Hizi tuhuma unazoshusha kwa wahusika ni nzito. Ujitahidi ushahidi wako uutunze sehemu salama. Ili ushahidi huo utakapohitajika kusiwepo na kisingizio cha 'niliuweka hapa nadhani kuna aliyenifanyia fitina'.
 
Maombi yetu, masikitiko yetu na vilio vyetu havikuwezesha kupatikana kwa waliommiminia risasi zisizo na hesabu aliyekuwa Mbunge wa Singida Mh. Tundu Antiphas Lissu.

Mkuu Mag3
Asante kwa tafakuri.

Nafikiri mh. Lissu yungali mbunge wa Singida.
 
Kilicho nishangaza ni hao Watu wa mungu kutelekeza bunduki zao sita.
M
Naamini hatutatekwa tena.
Wamempokea BWANA.
 
Tanzania Yetu
Hata hivyo iIngelipendeza kama angetutaja japo kwa mbali sisi tusio na uwezo lakini tumemlilia sana asipatwe na yale ya akina Ben Saanane! Hata hivyo tunamsamehe kwani tunajua watekaji na watesi wetu Tanzania wana bima ya kutoonekana, kutotambulika na kutojulikana.
 
Tafadhali sana, tambueni kuwa Mo kalazimishwa kuongea, hakuwa amejiandaa, na alichoongea huenda ni maelekezo ya majambazi yaliyomteka. Inategemea katendewa nini huko alikokuwa, mimi naamini bado alikuwa kwenye hofu kubwa na hali ya kutoamini kama kweli kaachiwa au kaambiwa Haya nenda ili akianza kutembea amiminiwe mawe ya AK47 pamoja na zile bastola. Jifanye wewe ndio uko katika hali hiyo halafu uone kivuli kinafanana na wale, unadhani utaweza toa neno kwa mpangilio unaoutaka wewe sasa hivi? Kwa ufupi, kwangu mimi Mo nisawa na amefufuka. Lakini pia si tunaambiwa tutende mema na tuondoke zetu, tusingoje shukrani? Sasa wewe ulimuombea ili akisalimika aje akukushukuru? Au unataka sehemu ya ile B.
 
Back
Top Bottom