Naunga mkono jitihada za kuondoa 'Elimu ya Mwendokasi' Tanzania

ZINDAGI

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
1,116
1,422
Napenda kuunga mkono na ku- support jitihada zinazochukuliwa na waziri wa elimu katika kurudisha heshima ya elimu ya Tanzania-Maana majoho yalizidi mtaani kwa elimu za miezi mitatu.

Kusema ukweli ilifika wakati heshima ya Graduate candidate ilikua haina maana yeyote ile mtaani, kwani watu wengi ambao hawakutaka kufuata njia halali ya elimu waliweza kupata credit na vyeti kwa muda mfupi sana na kuanza kuvitumia katika kuombea kazi.

Athari zake zikawa kubwa sana, kwani tumeshuhudia tangu zoezi hili lianze “wataalam” wengi wameanza kuachia ngazi ama kwa hiari yao, au wengine wamenyakwa kwa kukosa sifa za elimu zao, fikiria miaka kadhaa iliyopita, hawa ndio walikua planner, consultant, executer, na approval wa miradi yetu, Je leo utashangaa unachokiona ?

1.Bara bara imejengwa miezi miwili tuu imeharibika tayari

2.Madaraja chini ya kiwango,

3. Miradi ya maji isiyokamilika

4. Miradi ya umeme isiyokamilika

5.Mikataba isiyoeleweka

6.Mashine zilizochini ya kiwango vile.

7, Poor Standard

8. etc etc you name it

Binadam ni wajanja sana, wizara ijipange jinsi ya kutafuta njia bora zaidi ya kufanya uhakiki huu kwa kwenda mbali zaidi, kwani tumeshaona baadhi ya watu wanaanza ku-report polisi na kutangaza kwenye magazeti vyeti vimepotea, je siku zote walikua wapi?

Jambo la pili, ni kuvifuatilia vyeti vya watu waliovipata nje ya nchi, nina uhakika baadhi ya nchi hata zilizoendelea zina vyuo vingi vya mwendo kasi na vyeti vyake ndio hivyo wanavitumia hapa pia, hatuna uhakika na ubora wa elimu yake

Jambo la tatu, online degree, hizi pia ni za kuziangalia sana, kwani nyingi either watu wamefanyiwa au hazina ubora pia.

Tunataka wataalam na wasomi wa kweli, naamini nyote mtakaoathirika na zoezi hili, uwezo mnao, jipangeni kufuata taratibu za stahiki,ili mrudi katika game mkiwa mmeiva.

Mwisho naomba tumsaidie mheshimiwa waziri kuonyesha wapi walipo watu hawa, tafadhali tupia mchango wako hapa.
 
[QUOTE="AMMARITO, post: 16929562, member: 342588"

Kusema ukweli ilifika wakati heshima ya Graduate candidate ilikua haina maana yeyote ile mtaani, kwani watu wengi ambao hawakutaka kufuata njia halali ya elimu waliweza kupata credit na vyeti kwa muda mfupi sana na kuanza kuvitumia katika kuombea kazi.

Hapo kwenye bold sijakuelewa unamaanisha nini. Who is graduate candidate? What does the word stand for?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom