Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,379
3,882
1623416538230.png

Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.

Sasa moja kwa moja kwenye mada husika,tangu huyu Mama aingie madarakani nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mwenendo wake,ingawa kweli ni mapema sana kuanza kumtolea hukumu,lakini nachelea kusema huyu Mama HATUFAI hata kidogo especially kwa wale tunaotaka kuona Tanzania inapiga hatua za kweli za kimaendeleo na sio siasa,

Kwa sasa nisingependa kuongea mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba HAJUI Taifa hili linataka nini ili kujikomboa,anaonekana ni mtu wa KUFURAHISHA watu tu,bila kujali hii inchi inaathirika au inafaidika vp na anachokifanya,nauona mtindo wa utawala wa Kikwete ukijirudia kwa kasi sana nchini,

Ni dhahiri mpaka sasa huyu Mama anafanya mambo kwa kupangiwa au kuchukuliwa na upepo tu wa kwenye mitandao ya kijamii lakini yeye binafsi hana mipamgo na maono yoyote ya kueleweka juu ya Tanzania.
 
Huyo ndiye Rais wa nchi hiyo cheap popularity inaingiaje?

Mkitaka msitake yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi na ndiye aliyeachiwa hatamu ya uongozi, mbona aliyepita kuna miradi aliiwacha hivyo hivyo?

Tuwe na subira, kwani yeye hajatoka upinzani ni kiongozi wa CCM ileile na ilani ileile kinachotofautiana ni utendaji tu. Ukizingua unazinguliwa.
 
Sasa kama Samia ana cheap popurality sijui Magufuli alikuwa na nini? Maana yeye alimulikwa na Kamera hata akienda kumuomba Mungu wake.

Tulia mzee dawa ikuingie. Mlisema maendeleo ya Tanzania yamecheleweshwa na wapinzani sasa kuanza kijiji, kitongoji mpaka taifa ni CCM tupu.

Usiangalie idadi ya kurasa angalia utekelezaji.
 
Wee ukianza kutongoza Mwanamke kumuoa unaanza kumshawishi kwa kutaja furaha za ndoa au changamoto?

Sasa hivi tuna changamoto kubwa ya kurudisha Uwekezaji na njia bora ni kuwaaminisha mazingira kuwa yameboreshwa sio kuanza kuwapa maangalizo
 
137 Reactions
Reply
Back
Top Bottom