N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,824
- 9,521
Mhariri wa gazeti la Mwananchi leo Septemba 17 2016 anasema madereva wanaosafiri nchi zenye machafuko kama huko DRC wasindikizwe kwa sababu hali huko si salama, na visa vinavyosimuliwa ni vichache.
- Anasema madereva wengi wanaosaforosha mizigo kwenda DRC husimulia kuporwa, kupigwa na mizigo wanayosafirisha kuibiwa.
- Wanasema pamoja na kusafiri kwa misururu bado wanatendewa jinai
- Haya yanajiri wakati kukiwa na kongamano la kuboresha biashara baina ya nchi ya Tanzania na DRC, sasa suala la usalama kuwa nyuma kama ajenda kiongozi hakutawezesha kukuza biashara.
- MHARIRI anamalizia kwa kushauri kuwa uwekwe utaratibu kwa serikali ya DRC na Tanzania zikubaliane kuwe na utaratibu wa askari wa DRC kuwasindikiza madereva wetu mara wanapoingiza matairi ya malori yao DRC ili ukuaji wa biashara usizorote.