Naumwa, nataka kuandika wosia, wananishauri niache eti ni uchuro

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,108
2,000
Wakuu, nina umwa sana wapendwa. Ninasumbuliwa na uric acid. magoti yako hoi.

Nilitaka kuandika wosia,kwa ajili ya mali zangu kidogo nilizo nazo.

Mashoga zangu kama sio mashosti zangu wame nionya kuwa kamwe, katu nisithubutu kufanya hivyo kwa kuwa ni dalili mbaya (uchuro).

Wenye nia njema na mimi naombeni ushauri wenu.
Watu wame book hadi makaburi na si uchuro. We andika tu.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,503
2,000
Tatizo we are so materialistic tunasahau wosia wenye value zaidi ni busara zilikufanya upate hicho ulichonacho..., thus wape hao waliokuzunguka hizo nasaha (hata baba mmoja aliyerudi toka safari aliwaachia watoto wake, kwa mtazamo wake wapi ni pa kupata mali).. kwake yeye ilikuwa ni shambani

Binafsi sina kitu na wosia wangu huwa natoa kila dakika kwa mwenye masikio (kwa matazamo wangu) hence hata hapa ninapoandika nakuachia wosia..., Waachie hao wanakuzunguka busara na hekima na bila kusahau makosa uliyoyafanya ili wasiyarudie.., kama una mali nyingi usingoje kufa waingize kwenye hizo biashara wakati upo hai ili ujue nani anafaa wapi na ana uwezo gani wa kuweza kuendeleza, pili kama kuna mali kama nyumba moja n.k. badala ya kumpa huyu au yule unaweza ukasema ni ya familia na hakuna kuuzwa unless otherwise ina-make a loss, ila kinachopatikana kwenye nyumba ile either wagawane au iwasomeshe watoto wao (i.e. wajukuu zako) kama wakiona vipi wakatafute za kwao..

Karne hii mitoto haina busara wazee wakifa full kupoteza muda kugombania mali badala ya kutafuta.., unachowaachia hakiwaunganishi bali kinawatengenisha, hivyo kama ni Tycoon unaweza ukatengeneza Trust ili hizo mali ziendelee kusimamiwa na proffessionals na ndugu zako wanakula faida (kama hawana uwezo wa kuziendeleza)
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,792
2,000
Pole sana mkuu.

High level of Uric acid katika damu inatokana na matumizi makubwa ya Pombe na pia kula nyama nyingi.

Kunywa maji mengi na kupunguza vitu tajwa hapo juu,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom