Naumwa, nataka kuandika wosia, wananishauri niache eti ni uchuro

Wakuu, nina umwa sana wapendwa. Ninasumbuliwa na uric acid. magoti yako hoi.

Nilitaka kuandika wosia,kwa ajili ya mali zangu kidogo nilizo nazo.

Mashoga zangu kama sio mashosti zangu wame nionya kuwa kamwe, katu nisithubutu kufanya hivyo kwa kuwa ni dalili mbaya (uchuro).

Wenye nia njema na mimi naombeni ushauri wenu.

Pole sana kwa kuumwa mkuu,Mungu akufanyie wepesi.
 
Mwalimu wangu alinifundisha hata ukiwa na raptop tu wewe andika, Siku huongei tena Yale maandishi yataongea kwa niaba
 
Wakuu, nina umwa sana wapendwa. Ninasumbuliwa na uric acid. magoti yako hoi.

Nilitaka kuandika wosia,kwa ajili ya mali zangu kidogo nilizo nazo.

Mashoga zangu kama sio mashosti zangu wame nionya kuwa kamwe, katu nisithubutu kufanya hivyo kwa kuwa ni dalili mbaya (uchuro).

Wenye nia njema na mimi naombeni ushauri wenu.
RIP in advance, just in case.

Wosia andika tu hata kama hauugui. Unaweza gongwa na boda au Isamilo Express wosia ukatusaidia kubana matumizi ya kwenda mahakamani
 
Mwanamke anakuwaje na watoto nje ya ndoa?
Andika Haraka sana ,hasa kama una watoto nje ya ndoa,maana wakati wa kurithi watasumbuliwa na warithi halali.
Na kama una taka baadhi ya mali zako zitolewe sadaka ,bora ueleze mapema ,kwani warithi watagawana kila kitu bila ya kukuwekezea hata kwenye charity yoyote ile kwa faia yako huko wendako.
Wahi Kutowa Shahada kabla hujafa. Na uweke wasia kuwa Maiti yakoisije chomwa Moto kama wafanyavyo Huko ulaya na India kwa mapagani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom