Naumwa, nataka kuandika wosia, wananishauri niache eti ni uchuro

Pole sana jamani dear!

Andika wosia wako mwaya, tena umechelewa sana mimi kila mwezi nabadilishaga wosia wangu!!

Hamna uchuro hapo ni kujiandaa kuwaacha vizuri wale tuwapendao!!
Kwanini una badilisha kila mwezi?
 
Wakuu, nina umwa sana wapendwa. Ninasumbuliwa na uric acid. magoti yako hoi.

Nilitaka kuandika wosia,kwa ajili ya mali zangu kidogo nilizo nazo.

Mashoga zangu kama sio mashosti zangu wame nionya kuwa kamwe, katu nisithubutu kufanya hivyo kwa kuwa ni dalili mbaya (uchuro).

Wenye nia njema na mimi naombeni ushauri wenu.
Nafikiri watanzania huwa hawajifunzi na mambo yanayoendelea lakini tunapenda umbea na baadae mambo yanaenda.

Kabla ya kuandika wosia, hebu jiulize tu, ni watu wangapi wamefariki wakiacha Mali na tunashuhudia katika media na hata kesi au umbea umbea kwenye magazeti hayo, ambavyo mtu akifariki kaacha mali na ndugu zake ndo wa kwanza kukimbilia Mali za ndugu yao na kuacha mke na watoto wakiteseka?
Pia ni mara ngapi ndugu hufikia kupigana, kuchomana kisu hadi undugu kuisha kisa Mali? Na haya yapo katika jamii? Kabla hujafa, ukiona haya, je wewe ukifa hayawez kuwafikia watoto wako? Je unajuaje ndugu zako watakuwa wakarimu kwa watoto wako au watatenda haki kwa watoto wako?
Au hatujifunzi kitu hapo? Au tunaangalia na kusoma katika magazeti na kusambaza umbea kuhusu mambo ya wengine na siku imeisha?

Wosia ni tamko la mtu ambae anatoa kabla ya kifo chako akitaja Mali zake na jinsi zitakavyogawiwa kwa warithi aliowachagua kwa jinsi apendavyo. Pia ipo jinsi ya kuandika wosia maana wanaopewa mali au warithi hawaruhusiwi kujua kuhusu mgawanyo wa Mali hizo maana hapo ndo kimbembe kinaweza kuanzia hapo au hata ukauawa na mmoja wa warithi ili ufe mapema na yeye aanze kutesa kwa zamu kwa Mali alizoachiwa.

MNAKUMBUKA WIMBO WA "TUTATOANA ROHO YARABI , KWA MALI ALIZOACHA BABA?"
Kuhusu uchuro, huo ndo ujinga wa watanzania tulioachiwa na mababu zetu kutokn na kutokujua kusoma. Mungu ndo anajua siku ambayo atakuchukua na si vinginevyo.
Ila kwenye kuandika wosia ni uchuro na wengineo husema unawez kufa mapema, lakini mtu akinunua gari, akipanda ndege, mbona hawasemi ni uchuro wakati ndege zinaanguka na kuwaka moto, magari yanapata ajali lakini hatusemi kumiliki gari ni uchuro? Tena hasa hasa kwa pikipiki dar ambao kila kukicha huchomwa visu na kuibiwa pikipiki au kugongwa na magari makubwa? Aisee
Ila chaguo ni lako brother
 
Wakuu, nina umwa sana wapendwa. Ninasumbuliwa na uric acid. magoti yako hoi.

Nilitaka kuandika wosia,kwa ajili ya mali zangu kidogo nilizo nazo.

Mashoga zangu kama sio mashosti zangu wame nionya kuwa kamwe, katu nisithubutu kufanya hivyo kwa kuwa ni dalili mbaya (uchuro).

Wenye nia njema na mimi naombeni ushauri wenu.
Kunywa supu ya bamia na mabamia yatakusaidia kurekebisha matatizo yako .
 
Pole sana jamani dear!

Andika wosia wako mwaya, tena umechelewa sana mimi kila mwezi nabadilishaga wosia wangu!!

Hamna uchuro hapo ni kujiandaa kuwaacha vizuri wale tuwapendao!!
Hapa nmekaa nawaza hua unabadilisha kila mwezi kwamba mali zimeongezeka au unabadilisha marina ya warithi 😄
 
Wakuu, nina umwa sana wapendwa. Ninasumbuliwa na uric acid. magoti yako hoi.

Nilitaka kuandika wosia,kwa ajili ya mali zangu kidogo nilizo nazo.

Mashoga zangu kama sio mashosti zangu wame nionya kuwa kamwe, katu nisithubutu kufanya hivyo kwa kuwa ni dalili mbaya (uchuro).

Wenye nia njema na mimi naombeni ushauri wenu.
wosia unaelekeze urithi wa Mali za mwendazake utatwaliwa na Nani, urithi unnasimamiwa na sheria ya Mila, sheria ya kiserikali, sheria za Dini ,kwa sheria ya dini hata usipoandika wosia'uislamu"mgawanyo umeanishwa. kwa ile inayosimamiwa na sheria zingine wosia ni lazima uandikwe na mtu mwenye akili timamu, kuwe na ushahidi na kuwe na warithi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom