Naulizia wale wanaharakati wa kupinga malipo ya chenji ya Rada

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
413
Nimekuwa najiuliza walikopotelea wale wanaharakati wa kupinga serikali kurejeshewa malipo ya chenji ya Rada. Wanaharakati hawa na mafisadi wa uhuru na heshima ya nchi yetu kupanga matumizi ya fedha za walipa kodi wetu walikuwa katika pilika pilika za kukusanya saini za wanaowaunga mkono ili wazitumie kama kigezo cha kuweka kauzibe.

Wakati hatujapewa taarifa za matunda ya harakati zao, tulilolisikia ni kwamba BAE wamesalimu amri na sasa Watanzania kupitia serikali waliyoiweka madarakani kwa ridhaa yao, watapanga matumizi ya fedha hizi kwa manufaa yao na kwa uadilifu unaohitajika.

Tukio hili limeonyesha kwamba wazungu siyo watu wanaoshabikia tu harakati ambazo zinaweza kuwaweka katika doa la kidiplomasia. Lakini limethibitisha kwamba hizi zilikuwa ni harakati zinazofanywa na watu ambao hawajui wanachokifanya na walikuwa wanataka kuwapumbaza watanzania ili fedha za jasho lao ziingie kwenye mifuko ya wajanja kupitia kinachoitwa NGOs.
 
Back
Top Bottom