Aziz Ki Mayele
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 899
- 1,954
Nimeingia wengi wanapopa- refer kama 'Mjini' mida ya saa moja unusu hivi nikitokea mkoani, kwa ufupi mi ni Mgeni mjini hapa ni mara yangu ya tatu au nne kufika japo leo sina mwenyeji kama zile safari za awali, na hua simalizi siku tatu narudi mkoani kwetu.
Baada ya ku-park virago vyangu lodge "recommended by a friend" huko wanapopaita Kimara [sitaitaja kwa jina wanawake wa dar wasije nifata mpaka chumbani] kisha kupata maji na chakula nikaamua kufanyia kazi hiki nachosikiaga kua Dar ya usiku inamandhari nzuri kuliko ya mchana. Nikaamua kupanda Daladala kutoka kituo kimoja kwenda kingine, [Unspecified Destination] ili mradi tu nione madhari, gari ikifika mwisho naanza root nyingine
Sasa nilipopanda gari root ya kwanza nimekaa na mdada akaanza kuniongelesha ongelesha, kwa kweli nimeona ananisumbua kwa sababu alikua ananipotezea concentration ya kuona hayo mandhari yasemwayo. Mara aanze kunionyesha vitu kwenye simu yake dheni akaniuliza nashuka kituo gani nikamwambia kinachofuata, cha ajabu nilipokausha kushuka nae hajashuka anaendelea kunipigisha tuu stori. Nimejifanya kupokea simu nikashuka nikapumua nikapanda gari nyingine ili niendelee na mission yangu. Ajabu ni kwamba kaja dada mwingine nae anafanya yale yale
Nimepanda gari zaidi ya nne mambo ni yale yale, sasa niko njiani kurudi lodge nikalale tuu maana wameniharibia kabisa makusudio yangu.
Sasa wanawake wa Dar nawauliza MNA nini, mbona wanawake wa mkoani hawako hivi?