Nauliza tu: Kwanini wenye nyumba wana usumbufu hivi?

Mkuu nakushauri upgrade kidogo, najua umepanga chumba cha 50k, na choo mnachangia, Sasa tafuta chumba cha 80 to 150k hutaona usumbufu huu wa kipuuzi.
 
Kupangishwa na mijitu mieusi tabu tupu, heri upangishwe na white atakuvumilia kwa kila hali.
 
Mwenye nyumba wangu hana uswahili hivyo. Kwanza kodi inaisha naanza kumtegeshea akirudi usiku nimpe maana bila hivo anaweza zidisha hata mwezi hajanidai.
Anaishi nyumba ya pembeni, anaenda kazini mapema na kurudi usiku. Mimi mwenyewe sio mkorofi.
mtaa gani huo na mimi nije?
 
inategemeana na mtu maeneo na mikoa usukuman wenye nyumba wastarabu sana we utapata wap mwenye nyumba anakuambia mwanangu korona hii imeyumbisha sana maisha jkusanye ukipata leta hata ya mwez mmoja mmoja mpka hali itakapo kaa sawa
inasemekana kwamba wasukuma ni wastaarabu sana
 
Ukipanga nyumba zingatia mkataba...kwenye mkataba deal sana na terms na conditions halafu ishi nazo..utalipishwa vipi kitu ambacho hakipo kwenye mkataba...zingatia terms and conditions unapopanga utajua upange au usipange hiyo nyumba...la sivyo utapanga jehanam Siku moja ufanywe fursa.
 
Swala LA maji haina noma,we mkishatajiwa bill ,nenda kwenye mita chukua mita namba,piga simu Dawasco bule uliza bill ya maji ya mwezi katika mita yenu,12000 mnapigwa,wenye nyumba wengi huisi wapangaji hawana akili,siku waambie mwezi huu takataka utalipa Wewe,na uwafuate wenye gari kivyako waulize garama ya taka kisha lipa,hapo atakuwa ashajua janja ya nyani,Mimi upande Wa Dawasco alinifanyanyia hivyo
 
Hivi kwanini nyumba za kupanga ambazo wenye nyumba nao wanaishi humo zinakuwa na usumbufu sana. Wenye nyumba wanasumbua kinoma noma yani.

Mfano nyumba ninayokaa nimehamia mwezi wa tano, lakini dah natamani kuhama sema ninmeshalipa miezi sita. Yaani kuna vigharama vya ajab ajabu mpaka najiuliza huyu mzee ana shughul gan na hizi pesa.

Maana nimehamia tu nikaambiwa chemba imejaa wapangaji tujichange 36k tuite gari livute maji taka. Mimi nikagoma kwasababu hata mwezi sina nikasema chemba ikijaa tena nitatoa hii ya sasa sihusiki. Mwenye nyumba akanijia juu kinoma kuwa mimi mkorofi.

Kingine kila tarehe 1 na tar 15 kuna watu wanakuja kusafisha hapo nje kwenye vitofali vya chini sijui wanaviitaje jina lake inabid kila mpangaji achangie elf tatu ili hao mabwana walipwe.

Yaani nyumba hii ina mambo kibao yaani.

Bili ya maji jana imekuja elf 12 kila mmoja achangie na mimi hata sina mazoezi ya maji maana sifui wala kupika kwasababu sio mtu wa kushinda home kazi zangu ni za porini huko, utalii.

Nikirud nakaa week nasepa tena. Nguo huwa napeleka sehem zinafuliwa then nazifuata matumizi yangu ya maji ni kuoga tu na usafi wa ndan basi.

Je, huko kwenu jaman hali ikoje?

Wenye nyumba wenu wana habari gan huko maana dah.
Ndugu unapopanga hakikisha kunakuwa na mkataba ,na uoneshe wajibu wa mwenye nyumba na haki zake na wajibu wako na haki zako kwenye nyumba unayopanga ,ukiona poa pangs vinginevyo sepa.
 
Inategemea na mwenye nyumba, mi wangu huwa wanakaa mpk wanajenga zao ndio wanahama maana sina usumbufu wa ajabu. Mm na mpangaji tunakutana kwenye bili ya maji tu. Vingine kila mtu na kwake.

Mpangaji wa kwanza alikaa hapa miaka nane, na sasa yuko mwingine ana mwaka na miezi 4.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom