Nauliza tu: Kwanini wenye nyumba wana usumbufu hivi?

thebogo055

Member
Jun 22, 2020
19
100
Hivi kwanini nyumba za kupanga ambazo wenye nyumba nao wanaishi humo zinakuwa na usumbufu sana. Wenye nyumba wanasumbua kinoma noma yani.

Mfano nyumba ninayokaa nimehamia mwezi wa tano, lakini dah natamani kuhama sema ninmeshalipa miezi sita. Yaani kuna vigharama vya ajab ajabu mpaka najiuliza huyu mzee ana shughul gan na hizi pesa.

Maana nimehamia tu nikaambiwa chemba imejaa wapangaji tujichange 36k tuite gari livute maji taka. Mimi nikagoma kwasababu hata mwezi sina nikasema chemba ikijaa tena nitatoa hii ya sasa sihusiki. Mwenye nyumba akanijia juu kinoma kuwa mimi mkorofi.

Kingine kila tarehe 1 na tar 15 kuna watu wanakuja kusafisha hapo nje kwenye vitofali vya chini sijui wanaviitaje jina lake inabid kila mpangaji achangie elf tatu ili hao mabwana walipwe.

Yaani nyumba hii ina mambo kibao yaani.

Bili ya maji jana imekuja elf 12 kila mmoja achangie na mimi hata sina mazoezi ya maji maana sifui wala kupika kwasababu sio mtu wa kushinda home kazi zangu ni za porini huko, utalii.

Nikirud nakaa week nasepa tena. Nguo huwa napeleka sehem zinafuliwa then nazifuata matumizi yangu ya maji ni kuoga tu na usafi wa ndan basi.

Je, huko kwenu jaman hali ikoje?

Wenye nyumba wenu wana habari gan huko maana dah.
 

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
1,628
2,000
Pale kwangu yule mama ni mtu wa kuweka cha juu yaani ndoo ya maji ni shilingi 100 yeye anafanya 200, umeme inabidi ilipwe 10.000 yeye kafanya 15.000 na ni sheria. Usafi hatufanya wanafanya wanae ila kila mwezi hela ya usafi ni 5000. Kwenye taka sasa Ndio shida.
 

Mnyenz

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
1,234
2,000
Mkuu, amini nakuambia wewe ndio una shida.

Kama uliusoma vizuri mkataba na ukakubali yote basi wewe una shida.

Kama wewe unasema maji hutumii zaidi ya kuoga basi wewe una shida.
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
16,919
2,000
thebogo055,

Ukishakaa nyumba changanyikeni kubaliana na yote, kwanini usitafute nyumba ambayo utaka peke yako ofcourse utasema ni ghari sana lakini ili kuepukana na hizo kero hiyo ndiyo solution.
 

jerrybanks

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
2,343
2,000
Pale kwangu yule mama ni mtu wa kuweka cha juu yaani ndoo ya maji ni shilingi 100 yeye anafanya 200, umeme inabidi ilipwe 10.000 yeye kafanya 15.000 na ni sheria. Usafi hatufanya wanafanya wanae ila kila mwezi hela ya usafi ni 5000. Kwenye taka sasa Ndio shida.
Mimi usafi ilikuwa 10, maji 10, umeme 20, taka kwa mwezi 5000
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
16,919
2,000
Pale kwangu yule mama ni mtu wa kuweka cha juu yaani ndoo ya maji ni shilingi 100 yeye anafanya 200, umeme inabidi ilipwe 10.000 yeye kafanya 15.000 na ni sheria. Usafi hatufanya wanafanya wanae ila kila mwezi hela ya usafi ni 5000. Kwenye taka sasa Ndio shida.
Wenye nyumba hasa uwakute wale warithi ndiyo wenye nyumba utafurahi ndugu.
 

joshua_ok

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
13,052
2,000
We jamaa Mkorofi hufai kuishi na binadamu Ni Bora unahamishia makazi yako huko porini kwa wenzako
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
16,919
2,000
thebogo055,

Swala la maji kwanini usichangie? Kutumia au kutotumia maji inamhusije mwenye nyumba? Ni wewe mwenyewe hutumii hujakatazwa kutotumia maji, sasa lipa bili za maji acha makelele, ukishakua na jamii mnayokaa pamoja kila kitu ni vya kuchangiana.
 

kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,857
2,000
Inaonekana wewe mkorofi Sana. Kwahiyo unataka kila chumba kiwekewe mita ya maji? Halafu pia unataka kila mpangaji amegewe kipande chake chakudumu cha kufanya usafi? Hebu kutafakari wewe kwanza inaonekana mtata mtata hivi.

Vipi ungeishi zile nyumba mother house anakugongea mlango anaomba umpakulie mboga akale na wanawe? Jenga yako au kakae kwa shemeji. Puuzi moja wewe.
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
16,919
2,000
thebogo055,

Mkataba unasemaje wewe kama mpangaji majukumu yako ni yapi? Umesaini hakuna pakukimbilia usafi wa mazingira unataka usichangishwe wakati muda mwingi umesema hukai nyumbani? Nani hakufanyiea usafi bure.
 

njoo kwetu

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
556
1,000
Panga chumba kuanzia laki. Uone kama utapata usumbufu kama huo.

Vya bei poa vina gharama
 

mama hepache

Senior Member
Dec 22, 2018
132
250
Hivi kwanini nyumba za kupanga ambazo wenye nyumba nao wanaishi humo zinakuwa na usumbufu sana.. wenye nyumba wanasumbua kinoma noma yani.

Mfano nyumba ninayokaa nimehamia mwezi wa tano, lakini dah natamani kuhama sema ninmeshalipa miezi sita...
Huyo mwenyewe nyumba atakuwa anawafilisi. Kazi kweli kweli.
 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
2,805
2,000
Mwenye nyumba wangu hana uswahili hivyo. Kwanza kodi inaisha naanza kumtegeshea akirudi usiku nimpe maana bila hivo anaweza zidisha hata mwezi hajanidai.

Anaishi nyumba ya pembeni, anaenda kazini mapema na kurudi usiku. Mimi mwenyewe sio mkorofi.
 

Mbeba Lawama

Senior Member
Oct 12, 2015
132
500
Inategemeana na mtu maeneo na mikoa usukuman wenye nyumba wastarabu sana we utapata wap mwenye nyumba anakuambia mwanangu korona hii imeyumbisha sana maisha jkusanye ukipata leta hata ya mwez mmoja mmoja mpka hali itakapo kaa sawa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom