Nauliza tu je matukio mengine ni false flags?

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,627
2,000
False Flags ni Matukio ya Serikali au kikundi fulani Kujishambulia yenyewe ili wamsingizie adui wao wa nje au wa ndani kuwa yeye ndiye aliyefanya hayo. Kwa nia ya Kumpiga, au kumtengengenezea chuki kwa Wananchi au dunia. Au kutafuta justification ya kutumia nguvu kubwa kisiasa bila kulaumiwa na dunia, kwa upande wa matukio ya ndani.

Mifano ipo mingi sana Kwa upande wa Kimataifa, eg Zambia ulipokaribia Uchaguzi nafikiri ni 1994, Na Kaunda akataka Kugombea, Basi Chiluba akaandaa Igizo la jaribio la kujipindua Mwenyewe Kisha akamkamata Kaunda!

Wakati UKAWA walipotangaza UKUTA, Polisi walikuwa wakiranda randa mitaani wakiwa na RPG utadhani ni Alshabab, Mara ikatokea Mauaji ya kiajabuajabu ya Askari Wanne katika Bank! Wakasingiziwa UKUTA! Muda Kidogo Akauawa Askari huko Vikindu Kiajabu ajabu hivyo hivyo! Akina Mbowe wakasoma Mchezo Wakasitisha Maandamano ya UKUTA.

Haya Mauaji ya Kibiti nayo Nilisikia Mmoja akisema, "Iweje wanauawa ni CCM Tu?" Sasa kiukweli mimi sijui kama hawa ni Wahalifu wa Namna Gani, lakini inawezekana Kabisa ni False Flag ya kuandaa jambo fulani. Kwanini ni Polisi hasa ndio Wanaouwawa Matukio haya? Na mbona mpaka leo Waliowaua Wale Polisi Wanne pale Bank na Yule wa Vikindu hawajakamatwa?
 
xav bero

JF-Expert Member
Nov 24, 2016
5,148
2,000
Nani alisema ukuta,,au kijiwen kwenu ndio mnasema hayo? Sijawah kusikia serikali ikisema ni chama fulan asilan
 
Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,227
2,000
Kama ni kweli theory yako then as a nation we're absolutely phacked up.

God help us. Am scared!
 
Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
14,912
2,000
Kuna Jambo Zito Nilitaka Kukiandika Ila Ndugu Zangu Wameniambia

Aya Mambo Niyaache Ivi Ivi Niyasikie Tuu
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,608
2,000
False Flags ni Matukio ya Serikali au kikundi fulani Kujishambulia yenyewe ili wamsingizie adui wao wa nje au wa ndani kuwa yeye ndiye aliyefanya hayo. Kwa nia ya Kumpiga, au kumtengengenezea chuki kwa Wananchi au dunia. Au kutafuta justification ya kutumia nguvu kubwa kisiasa bila kulaumiwa na dunia, kwa upande wa matukio ya ndani.

Mifano ipo mingi sana Kwa upande wa Kimataifa, eg Zambia ulipokaribia Uchaguzi nafikiri ni 1994, Na Kaunda akataka Kugombea, Basi Chiluba akaandaa Igizo la jaribio la kujipindua Mwenyewe Kisha akamkamata Kaunda!

Wakati UKAWA walipotangaza UKUTA, Polisi walikuwa wakiranda randa mitaani wakiwa na RPG utadhani ni Alshabab, Mara ikatokea Mauaji ya kiajabuajabu ya Askari Wanne katika Bank! Wakasingiziwa UKUTA! Muda Kidogo Akauawa Askari huko Vikindu Kiajabu ajabu hivyo hivyo! Akina Mbowe wakasoma Mchezo Wakasitisha Maandamano ya UKUTA.

Haya Mauaji ya Kibiti nayo Nilisikia Mmoja akisema, "Iweje wanauawa ni CCM Tu?" Sasa kiukweli mimi sijui kama hawa ni Wahalifu wa Namna Gani, lakini inawezekana Kabisa ni False Flag ya kuandaa jambo fulani. Kwanini ni Polisi hasa ndio Wanaouwawa Matukio haya? Na mbona mpaka leo Waliowaua Wale Polisi Wanne pale Bank na Yule wa Vikindu hawajakamatwa?

Sema ulitaka utuambie kwamba leo umejifunza neno ,,false flag" na sasa unataka kututambia, haya hongera kwa hilo!
 
TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,627
2,000
Nani alisema ukuta,,au kijiwen kwenu ndio mnasema hayo? Sijawah kusikia serikali ikisema ni chama fulan asilan

Wale Askari Wanne walipouwawa Mkuu wa Mafunzo Wa Polisi alisema haya! Mimi sio Taahira wa Mitaani

Kiherehere

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,808
2,000
mimi ni mmoja wa watu waliolichukulia hili jambo kwa muda mrefu kama ulivyoleta mleta mada!! Ni kama maujaji ya Polisi stakishari...ilikua ni diversion ya kukatwa kwa Lowasa...vingi vinaokea, hapa ili tu kuondoa au kujenga jambo linaloweza kuja kufanyika baadae.

Hili la kibiti...ni mpango wa nguvu kwa ajili ya uchaguzi 2020......leon liko Kibiti....litahama....ikifika 2020...utasikia tu kipindi cha kampeni, "intelijensia ya polisi" itakuwa juu hasa kwa kampeni za upinzani...LAZIMA WAFUNGWE GAVANA!!

Pili, kusema wauaji wananua viongozi wa CCM tu!! ni mpango wa anaesuka jambo hili.......na kulitangaza kwa nguvu kuaminisha watu....UKWELI TUNAUJUA, SASA WATAMUUA KIONGOZI WA UPINZANI YUPI WAKATI PWANI YOTE INATAWALIWA NA maCCM??

Waelezeni hawa....nchi hii haina akili ya kijasusi ya maana, kushawishi waelewa...mipango na akili ya Bashite!!

Kwao ni Collateral damage
 
ARIUS MZUSHI

JF-Expert Member
Jun 18, 2017
272
250
Kuna Jambo Zito Nilitaka Kukiandika Ila Ndugu Zangu Wameniambia

Aya Mambo Niyaache Ivi Ivi Niyasikie Tuu

Ni vizuri ukaliandika, yamkini likaleta uponyaji kule Kibiti maana unaweza kusubiri mwingine aseme afu asiseme na hali ikaendelea kuwa mbaya kila uchao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom