Nauliza tu hivi OCD wa Hai na RPC wa Kilimanjaro kwanini hawakumkamata Sabaya wakati akifanya uhalifu uliomfunga jela?

Katika muundo wa kiutawala hao wana usalama wote wasingeweza kumtia nguvuni Sabaya bila order ya juu kutoka kwenye mamlaka ya uteuzi wake

Na si kwamba hawakujua bali waliyajua na pengine waliyaripoti lakn no order no arrest

Na sio tu Sabaya, hata akiwa Waziri Mkuu, waziri, Katibu mkuu, wakurugenzi na wengne wenye wadhifa ya kuteuliwa na Rais hawawezi kutiwa nguvuni ikiwa wamefanya uhalifu bila idhini au order ya mwenye mamlaka ya uteuzi wake

Pia Rais anadili na mambo mengi sana sana ya nchi tena yale makubwa makubwa, hvyo sio kila taarifa humfikia yeye na kungoja maamuzi yake bali zingine huishia ngazi za kati either kwa Waziri Mkuu, Katibu mkuu kiongozi nk kulingana na chain of command ya kiutawala
Kwa hiyo unasemaje hapa?
 
Kwa OCD asingeweza maana Sabaya alikuwa ni boss wake ila kwa RPC sijajua protocol zipoje
 
Na hata hii kesi ya Mbowe na wenzake, hakuna askari polisi wa Kilimanjaro au Moshi. Hii kesi unaiona ina mkono wa Sabaya. Hata ukiangalia mashahidi wa Jamhuri wako connected na Sabaya (mfano Kaaya ambaye alikua akifanya kazi za nyumbani kwa Sabaya). Ukamataji wa watuhumiwa wa kesi ya Mbowe haujahusisha askari polisi wa Kilimanjaro au Moshi, Sabaya hakuwa nao vizuri hawa askari wa Kilimanjaro. Huyo Kingai aliyekuwa RCO wa Arusha na Mahita aliyekua ofisi ya OC - CID Arusha, wote hao ni team Sabaya, ndiyo maana waliweza kutumika katika operation bila hata kumhusisha askari hata mmoja wa Kilimanjaro wakati ukamataji ulifanyika Moshi Kilimanjaro.
Washirika wake katika ushetani pamoja na Clouds TV, wamemtosa General Lengai Ole Sabaya. Alichobakiza ni kutubu na kumrudia Mungu. “Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao.” (2Nyakati 7: 14). AMEN
 
Najaribu kujiuliza Aliyekuwa MKUU wa WILAYA ya HAI Bw.SABAYA alifanya Matukio ya UHALIFU ndani ya HAI Na Nje ya HAI
WILAYA ya HAI ina OCD na MKOA una RPC Je ni kwanini VIONGOZI hao Hakuna Sehemu yoyote Wanaonekana Kumchukulia Hatua za KUMKAMATA Bw.SABAYA mpaka pale Mh.RAIS SAMIA Alipomsimamisha KAZI na Kuagiza UCHUNGUZI Ufanyike na ndipo ALIPOKAMATWA.

Je, ule UHALIFU ulikuwa na BARAKA za OCD wa HAI na RPC wa Kilimanjaro?

Na Kwanini kwa Kutokumkamata Bw. SABAYA Wakati Akitenda UHALIFU Wasichukuliwe Nao HATUA?
Hakuna uwajibikaji kabisa katika utumishi wa umma na viongozi wa chama na serikali.
Hapo ndio umuhimu wa Katiba ya wananchi unapokuwa inevitable.
 
Najaribu kujiuliza Aliyekuwa MKUU wa WILAYA ya HAI Bw.SABAYA alifanya Matukio ya UHALIFU ndani ya HAI Na Nje ya HAI
WILAYA ya HAI ina OCD na MKOA una RPC Je ni kwanini VIONGOZI hao Hakuna Sehemu yoyote Wanaonekana Kumchukulia Hatua za KUMKAMATA Bw.SABAYA mpaka pale Mh.RAIS SAMIA Alipomsimamisha KAZI na Kuagiza UCHUNGUZI Ufanyike na ndipo ALIPOKAMATWA.

Je, ule UHALIFU ulikuwa na BARAKA za OCD wa HAI na RPC wa Kilimanjaro?

Na Kwanini kwa Kutokumkamata Bw. SABAYA Wakati Akitenda UHALIFU Wasichukuliwe Nao HATUA?
SABAYA UMKAMATEJE, ULIKUWA UNAPOTEZA KAZI TOKA UTAWALA WA MKOLONI
 
Back
Top Bottom