Nauliza tu hivi OCD wa Hai na RPC wa Kilimanjaro kwanini hawakumkamata Sabaya wakati akifanya uhalifu uliomfunga jela?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,879
Najaribu kujiuliza Aliyekuwa MKUU wa WILAYA ya HAI Bw.SABAYA alifanya Matukio ya UHALIFU ndani ya HAI Na Nje ya HAI
WILAYA ya HAI ina OCD na MKOA una RPC Je ni kwanini VIONGOZI hao Hakuna Sehemu yoyote Wanaonekana Kumchukulia Hatua za KUMKAMATA Bw.SABAYA mpaka pale Mh.RAIS SAMIA Alipomsimamisha KAZI na Kuagiza UCHUNGUZI Ufanyike na ndipo ALIPOKAMATWA.

Je, ule UHALIFU ulikuwa na BARAKA za OCD wa HAI na RPC wa Kilimanjaro?

Na Kwanini kwa Kutokumkamata Bw. SABAYA Wakati Akitenda UHALIFU Wasichukuliwe Nao HATUA?
 
RPC alikuwa against hila za Sabaya.

Ndiyo maana Sabaya alipowasingizia wafanyabiashara wa mabasi ya mikoani kuharibu reli, RPC alifanya uchunguzi na akakanusha kwamba si kweli (tukio la kijasiri sana hili kwa nyakati zile za Magu).

Ndiyo maana Sabaya alifanya uhalifu sana Chuga sababu ya kuwa na akina Kingaiii ambao wanamuunga mkono unyama wake.
 
Watakwambia aliyafanya hayo kwa usiri na hawakupata taarifa kutoka vyanzo vyao kwa wakati muafaka.

SASA WAULIZE HIVI;
Kwa nini alipofanya uhalifu wa kuharibu Mali za watu mchana kweupe hawakumkamata?Kwa mfano:kuharibu mashamba ya Mbowe.

HALAFU
Linganisha majibu.
 
M/kiti kamati ya ulinzi,
Mteule wa Rais.

RPC na OCD ni wateule wa IGP
RC Mwigwira alifahamu sana na alionya lakini hakuwa na nguvu.

Muundo wa mamlaka unamfanya mmoja kuwa Alpha na Omega.
Hoja ya katiba bora na siyo katiba mpya ni yamsingi ili asiwepo wakuumizwa kwa kauli toka juu
 
Sabaya alikuwa akifanyia ujambazi wake aArusha, huku akilindwa na wezi wenzake oc cid Arumeru na kina Kingai na Mahita.
 
RPC alikuwa against hila za Sabaya.

Ndiyo maana Sabaya alipowasingizia wafanyabiashara wa mabasi ya mikoani kuharibu reli, RPC alifanya uchunguzi na akakanusha kwamba si kweli (tukio la kijasiri sana hili kwa nyakati zile za Magu).

Ndiyo maana Sabaya alifanya uhalifu sana Chuga sababu ya kuwa na akina Kingaiii ambao wanamuunga mkono unyama wake.
Na hata hii kesi ya Mbowe na wenzake, hakuna askari polisi wa Kilimanjaro au Moshi. Hii kesi unaiona ina mkono wa Sabaya. Hata ukiangalia mashahidi wa Jamhuri wako connected na Sabaya (mfano Kaaya ambaye alikua akifanya kazi za nyumbani kwa Sabaya). Ukamataji wa watuhumiwa wa kesi ya Mbowe haujahusisha askari polisi wa Kilimanjaro au Moshi, Sabaya hakuwa nao vizuri hawa askari wa Kilimanjaro. Huyo Kingai aliyekuwa RCO wa Arusha na Mahita aliyekua ofisi ya OC - CID Arusha, wote hao ni team Sabaya, ndiyo maana waliweza kutumika katika operation bila hata kumhusisha askari hata mmoja wa Kilimanjaro wakati ukamataji ulifanyika Moshi Kilimanjaro.
 
Katika awamu ya 5 (awamu ya kijambazi) Sabaya alikuwa kama Nungunungu(hakamatiki)
Na yule Mwendazake angekuwepo, wala asingefunguliwa hiyo kesi. Na bila shaka, leo hii angekuwa ni MKUU WA MKOA! Hata yule MUSIBA, hizo kesi alizohukumiwa kulipa mabilioni ya fedha, zingekuwa zishatupiliwa mbali.
Hayo, ndiyo tuliyoyaona. Sina shaka kulikuwa kuna MAOVU mengi sana yakifanyika, ambayo hatuyafahamu! Namuomba
Mwenye Enzi Mungu amuweke JPM mahali panapofanana na MATENDO yake!
 
Najaribu kujiuliza Aliyekuwa MKUU wa WILAYA ya HAI Bw.SABAYA alifanya Matukio ya UHALIFU ndani ya HAI Na Nje ya HAI
WILAYA ya HAI ina OCD na MKOA una RPC Je ni kwanini VIONGOZI hao Hakuna Sehemu yoyote Wanaonekana Kumchukulia Hatua za KUMKAMATA Bw.SABAYA mpaka pale Mh.RAIS SAMIA Alipomsimamisha KAZI na Kuagiza UCHUNGUZI Ufanyike na ndipo ALIPOKAMATWA
Je ule UHALIFU ulikuwa na BARAKA za OCD wa HAI na RPC wa Kilimanjaro?
Na Kwanini kwa Kutokumkamata Bw. SABAYA Wakati Akitenda UHALIFU Wasichukuliwe Nao HATUA
 
Sabaya na tabia yake vs kesi ya Mbowe, kichefuchefu mashahidi wasi na uhusiano na mhalifu, kama aliweza kubambikia tuhuma ya mataruma wenye mabasi, anaweza fanya lolote!
 
Hai penyewe hapana askali wa upelelezi ambapo magaidi walijichimbia.
Hotel ya Aish haina viongozi wa serikali za mtaa?
Hiyo hotel haijapekuliwa isijekuwa imehifadhi mabomu ikawa madhara kwa wageni.
Huu mtandao wa ugaidi uchunguzwe upya nje ya akina Kingai.
Eti kikulacho kinguoni mwako
 
Na yule Mwendazake angekuwepo, wala asingefunguliwa hiyo kesi. Na bila shaka, leo hii angekuwa ni MKUU WA MKOA! Hata yule MUSIBA, hizo kesi alizohukumiwa kulipa mabilioni ya fedha, zingekuwa zishatupiliwa mbali.
Hayo, ndiyo tuliyoyaona. Sina shaka kulikuwa kuna MAOVU mengi sana yakifanyika, ambayo hatuyafahamu! Namuomba
Mwenye Enzi Mungu amuweke JPM mahali panapofanana na MATENDO yake!
Uyo mwendazake apelekewe moto kw matendo yake ya kufuga majambazi kama sabaya
 
Najaribu kujiuliza Aliyekuwa MKUU wa WILAYA ya HAI Bw.SABAYA alifanya Matukio ya UHALIFU ndani ya HAI Na Nje ya HAI
WILAYA ya HAI ina OCD na MKOA una RPC Je ni kwanini VIONGOZI hao Hakuna Sehemu yoyote Wanaonekana Kumchukulia Hatua za KUMKAMATA Bw.SABAYA mpaka pale Mh.RAIS SAMIA Alipomsimamisha KAZI na Kuagiza UCHUNGUZI Ufanyike na ndipo ALIPOKAMATWA
Je ule UHALIFU ulikuwa na BARAKA za OCD wa HAI na RPC wa Kilimanjaro?
Na Kwanini kwa Kutokumkamata Bw. SABAYA Wakati Akitenda UHALIFU Wasichukuliwe Nao HATUA?

Katika muundo wa kiutawala hao wana usalama wote wasingeweza kumtia nguvuni Sabaya bila order ya juu kutoka kwenye mamlaka ya uteuzi wake

Na si kwamba hawakujua bali waliyajua na pengine waliyaripoti lakn no order no arrest

Na sio tu Sabaya, hata akiwa Waziri Mkuu, waziri, Katibu mkuu, wakurugenzi na wengne wenye wadhifa ya kuteuliwa na Rais hawawezi kutiwa nguvuni ikiwa wamefanya uhalifu bila idhini au order ya mwenye mamlaka ya uteuzi wake

Pia Rais anadili na mambo mengi sana sana ya nchi tena yale makubwa makubwa, hvyo sio kila taarifa humfikia yeye na kungoja maamuzi yake bali zingine huishia ngazi za kati either kwa Waziri Mkuu, Katibu mkuu kiongozi nk kulingana na chain of command ya kiutawala
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom