Nauliza tu: Hivi Mbunge Jason Rweikiza huwa bubu?

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,958
7,512
Kama ni hasara basi kuna maeneo wana hasara kweli kweli. Ukiwa mbunge na ukawa bungeni ni tofauti unapokuwa kanisani/msikitini ukiwa na viongozi wa dini. Huko unahitaji kuwa mpole, mtulivu na kujichunga lakini bungeni ni kinyume chake. Huku kupaza sauti, kusema, kuongea, kuuliza na kubisha ndo mahala pake, huku si kanisani.

Mkiwa na mbunge anayekaa bungeni mithiri ya kanisani basi mmepatwa kama jua, na tunaweza tukaiita CONSTITUENT ECLIPSE. Mna hasara mara zote. Watakatifu na mabubu bungeni si saizi yao. Waende kanisani na kunakowafaa wao, bungeni waachieni wapiganaji, wapambanaji na wajenga hoja kwasababu kazi ya siasa ni ushawishi na sahivi (enzi za JPM), siasa zimehamia bungeni. Ukishindwa kufanya huko basi we jihesabu unapotea tu.

Haiwezekani bunge linaanza zaidi ya wiki na sasa miezi uko pale mithiri ya walioko madhabauni. Siasa za zamani za kutembeza pesa hovyo zimekwisha sasa, kwamba utatumia pesa kuwarubuni watu ili urudi bungeni. Ni kati ya wabunge wasioweza kujenga hoja, kusimamia jimbo lako na kuwaweka mbele watu wako. Nikisema wengine mko huko kwa ajiri ya kukinda shughuli zenu naamini sitakosea na wewe ni mmoja wa hao. Jipange, jitume na usikae kama mgeni jamvini. Mara hii kazi unayo mzee wetu
 
Akiongea pumba utamwanzishia uzii Mhe.. Kaongea pumba kajinyamazia bado unamsema
 
Bukoba vijijini mmepata hasara, mnaacha kuchagua wenye uwezo mnachagua wenye pesa.
Mkuu wananchi wananunua bidhaa iliyoko sokoni. Siku zote ukimwondoa marehemu S. Kinyondo hili jimbo halijawahi kuletewa bidhaa ya maana si kupitia CCM wala upinzani. Wanaopelekewa wachague ndo hawa akina Rweikiza na baada ya kuonekana yupo yupo tu akapewa ukatibu wa wabunge. Huyu ni hasara kwa jimbo na wanastahili mbadala ili akapumzike
 
Kwa Rweikiza muhimu kwake pesa kelele sio sehemu yake ya maisha hivyo hamtamsikia na 2020 atalipoti mjengoni, wahaya jifunzeni
 
Kati ya wabunge waliyowahi kuongoza jimbo la Bukoba vijijini ambaye hajafanya chochote ni uyo,tetemeko la ardhi lilitokea katika jimbo lake lakini hakuna kitu alichowasaidi 2020 hasahau kabisa
 
Mkuu kwa ujumla wabunge wengi ni vilazaz hatari, uwezo mdogo sana!
Binafsi mie naona kwa taifa kama letu kuwa na wabunge ni hasara kuliko faida, output yao ni ndogo sana ukilinganisha na tunachowalipa (kodi zetu maskini wa Mungu)!!!!
 
Kama ni hasara basi kuna maeneo wana hasara kweli kweli. Ukiwa mbunge na ukawa bungeni ni tofauti unapokuwa kanisani/msikitini ukiwa na viongozi wa dini. Huko unahitaji kuwa mpole, mtulivu na kujichunga lakini bungeni ni kinyume chake. Huku kupaza sauti, kusema, kuongea, kuuliza na kubisha ndo mahala pake, huku si kanisani.

Mkiwa na mbunge anayekaa bungeni mithiri ya kanisani basi mmepatwa kama jua, na tunaweza tukaiita CONSTITUENT ECLIPSE. Mna hasara mara zote. Watakatifu na mabubu bungeni si saizi yao. Waende kanisani na kunakowafaa wao, bungeni waachieni wapiganaji, wapambanaji na wajenga hoja kwasababu kazi ya siasa ni ushawishi na sahivi (enzi za JPM), siasa zimehamia bungeni. Ukishindwa kufanya huko basi we jihesabu unapotea tu.

Haiwezekani bunge linaanza zaidi ya wiki na sasa miezi uko pale mithiri ya walioko madhabauni. Siasa za zamani za kutembeza pesa hovyo zimekwisha sasa, kwamba utatumia pesa kuwarubuni watu ili urudi bungeni. Ni kati ya wabunge wasioweza kujenga hoja, kusimamia jimbo lako na kuwaweka mbele watu wako. Nikisema wengine mko huko kwa ajiri ya kukinda shughuli zenu naamini sitakosea na wewe ni mmoja wa hao. Jipange, jitume na usikae kama mgeni jamvini. Mara hii kazi unayo mzee wetu
Wewe si ndo mtetezi wake?
 
Mkuu, usimuongezee mzigo wa kuongea huyo Mheshimiwa. Yeye ni Katibu wa Wabunge wa CCM. Hilo linamtosha. Hayo ya kuchangia na kuuliza kuhusu Jimbo lake yatangoja kwanza. Upo?
Shule zake ziko dhofuli hali,Mkuu wa Shule ya St Anne Marie hana profession yyte,ni dogo aliyemaliza hapo 2013.
 
Nauliza tu: Hivi Mbunge Jason Rweikiza huwa bubu?
Ni bubu sababu wanaomchaguwa nawo ni bubu, wanaomchaguwa wangelalamika kuchachamaa sidhani kama angekuwa bubu, mmemuendekeza kabisa, sasa anakula hela za bunge kwa mrija na amani...hela za bure kabisa..
 
ASIWE MLOPOKAJI KAMA TUNDU LISSU ; USO UMEJAA AIBU ; JITU ZIMA OVYO .
 
Back
Top Bottom