Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
WanaJF; Naomba tulijadili hili.
Hivi ni sawa kwa jeshi letu la polisi kutumia silaha za kivita (military) katika shughuli za kiraia? hapa nina maana ya sub machine gun (SMG), silaha ambayo ilitengenezwa maalum kwa vita.
Hii silaha inatumia magazine yenye risasi 30 na ni vigumu kwa mtumiaji kuweza kupiga risasi moja kwani usipoangalia ukianza kuminya tu trigger, zaidi ya tatu au nne zinatoka.
Mwanajeshi mmoja kaniambia kwamba katika mafunzo yao ya silaha, hupewa mtihani wa kuminya trigger ili silaha itoe risasi chache zaidi -- ni kazi kubwa kweli kweli, aliniambia.
Sasa hawa polisi wetu hutumia sana SMG katika shughuli za kiraia na huenda ndiyo sababu raia wengi wasio na hatia wanakufa. Huenda silaha hii huwapa usongo sana au mdadi polisi anayetumia na hivyo kujikuta anamimina risasi nyingi katika makundi ya watu bila kukusudia.
naona ingefaa polisi wasitumie SMG, na badala yake watumie zile rifle za kawaida kama vile Mark 4 au nyinginezo -- bolt action rifles.
Hizi huwa na clip ya risasi 5 au 10 na inatoka moja moja tu, yaani kila ukipiga lazima u-cock kwa kutoa ganda la risasi na kuingiza ingine kwenye chamber. Hii kazi inachukuwa kama sekunde 5 au sita hivi.
Nawasilisha.