Nauliza: Ni lini JK katika hotuba zake alizungumzia wizi/ufisadi kwa kuukemea kwa ukali?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233



Ni lini, na katika mkutano au hafla gani tangu aupate urais Kikwete aliujia juu ufisadi kwa kuulani kwa nguvu zake zote kama ni kansa inayoitafuna taifa na kutishia amani ya nchi hii?

Mimi nataka kujua ni lini alifanya hivyo na ikiwezekana mwenye ushahidi hata wa clip au text ya maneno husika ayaweke hapa. Naona tumekuwa wepesi kumsema huyo swahiba wake EL kuhusu ukimya wa namna hiyo hiyo.


Najua kuna baadhi yenu, hasa wale wanaoitetea CCM kwa njia ya upofu mtasema "hana haja ya kuzungumzia ufisadi – kwani yeye ni mtu wa vitendo."

Binafsi nalikumbuka tukio moja – mapema mwezi Agosti 2008 pale ilipoonekana hakuwa na budi bali kusema angalau kitu kidogo kuhusu ufisadi/wizi wa EPA. Aliingia Bungeni lakini ishu ya EPa ilikuja mwisho kabisa kama dakika 20 za hotuba yake ya karibu masaa mawili ambayo aliongea mambo mengine na iliwafanya wasikilizaji/watazamaji wa hotuba hiyo kuanza kuwaza kwamba hata EPA hataizungumzia.

Lakini hata hivyo hiyo ishu ya EPA ilimpa tabu sana – kwanza alianza kwa kusema eti hizo hela hazikuwa za serikali bali ni hela za Tz zilizowekwa BoT na watu/makampuni binafsi kwa ajili kulipa bidhaa wangeziagiza kutoka nje. Ilikuwa ni enzi ya strict Imports and exchange control – miaka ya themanini. Sawa, hazikuwa za serikali in strict sense of the word, lakini zilikuwa mkononi mwa serikali (BoT) kama mtunzaji (custodian) kwa hiyo hazikupaswa kuibiwa.

Pili haikuwa kweli kabisa kwamba hazikuwa hela za serikali kwani miongoni mwa wawekaji hizo hela yalikuwemo mashirika ya umma yaliyokuwa yakifanya biashara ya uagizaji toka nje kama vile STC, State Motor Corp, Dabco, etc etc – enzi hizo.

Halafu katika speech yake JK alitaja EPA kama mara tatu tu na alikwepa kabisa, au hakuwa na ubavu wa kutaja maneno "wizi", "kuiba," "kuibiwa," au "ziliibiwa" na badala yake aliishia tu kusema "walilipwa", "walipokea," "walichukuwa" etc akimaananisha kilichotokea.

Alionekana ni mtu wa ajabu kabisa kwamba hao jamaa ambao hayo mabilioni ya EPA yalihamia katika umiliki wao bila ya wao kustahili "kuchukuwa", "kupewa" au ‘kulipwa" - wanaitajwe? Hakika ni wezi tu, lakini JK ilimwia vigumu kutaja neno halisi la watu wanaofanya hivyo!

Lakini cha ajabu ni kwamba pamoja na kutokuwa na ujasiri wa kuwaita "wajamaa wale ni wezi, Lakini aliweza hapo hapo Bungeni kujinyakulia mamlaka ya ‘prosecutor' na jaji kwa pamoja na kuwahukumu, tena kwa njia ya kushangaza kabisa – yaani kuwataka warejeshe hela au watinge mahakamani. Utaratibu huu sijui aliutoa katika vitabu gani! Na juu ya ajabu ya ajabu wanasheria wetu (wakiwemo majaji) walikaa kimya tu.



Lakini huu ni mfano mmoja tu ambapo JK angalau aliweza kuzungumzia wizi/ufisadi katika serikali yake na swali langu labakia pale pale.

Nawasilisha.




 
Nami huwa najiulkiza hivyo hivyo. Ni swali la msingi kabisa ulilouliza. na I fear akiingia EL, Tanzania itapiga miaka 20 bila ya hatua zozote kutoka juu kabisa kuutokomeza ufisadi.
 
We,Thubutu yake aanzie wapi kukemea hayo.Hawezi huyu mwenyekiti wa magamba,ye mwenyewe kila siku analalamika kuwa katika chama chake kuna rushwa halafu hachukui hatua yoyote ile utafikiri hana mamlaka.
 
siku zote kuuliza si ujinga bali wewe unaye mwita mwenzako mjinga ni ndiyo huna akili
take care anda think before saying
huna jipya
 
Katika list of shame, jina lake lilitajwa Mwembe Yanga na kamwe hakukanusha. Hivyo ni dhahiri kuwa hawezi kukemea ufisadi maana nae YUMO. Dawa yake ni kwamba ajiandae kujibu atokapo madarakani.
 
Huyu mjamaa hawezi kuzungumzia ufisadi- anachoweza ni kupiga picha ya pamoja na watu kama akina Ray C wenye kuitangaza Tanzania vibaya!
 
Muasisi wa Ufisadi kwa vipi atakemea ufisadi,au umesahau the famous Fisadis mtandao,Rostam Azizi, Edward Lowasa,Jakaya Mrisho Kikwete,Zakhia Meghiji,Daudi Bilali,Jeetul Patel,Yusuphu Manji , constructor wa ufisadi vipi ajikemee labda sayari ya dunia itakapogeuka
 
Mimi zaidi humuona kwenye picha mbalimbali za matukio kama vile kuwashika mikono watoto wa mitani,kukaa kwenye mkeka karibu na mama mlemavu, kupungia wananchi kwenye mikutano,kugongea mikono wananchi,kupiga picha na timu ya taifa, kupiga picha na hashim sabeet, na watu wengine wengi maarufu....kwa kifupi ni mtu wa matukio!!! Zaidi ya hapo anapenda kutabasamu.
 
Mbona zipo kesi za ufisadi mahakamani?

Kwani kuzungumzia kwa ukali ndio suluhisho?
 
Mbona zipo kesi za ufisadi mahakamani?

Kwani kuzungumzia kwa ukali ndio suluhisho?
Kesi yeyote ambayo inamwacha Kikwete ni uonevu rafiki yake Lowassa anasema KIkwete ndie alikuwa ananufaika na milioni 150 kila siku kwa mradi wa Richmond aka Dowans je amepelekwa mahakamani kwa wizi huo mkubwa
 
Back
Top Bottom