Nauliza: Ni lini JK katika hotuba zake alizungumzia wizi/ufisadi kwa kuukemea kwa ukali?


Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,402
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,402 0Ni lini, na katika mkutano au hafla gani tangu aupate urais Kikwete aliujia juu ufisadi kwa kuulani kwa nguvu zake zote kama ni kansa inayoitafuna taifa na kutishia amani ya nchi hii?

Mimi nataka kujua ni lini alifanya hivyo na ikiwezekana mwenye ushahidi hata wa clip au text ya maneno husika ayaweke hapa. Naona tumekuwa wepesi kumsema huyo swahiba wake EL kuhusu ukimya wa namna hiyo hiyo.


Najua kuna baadhi yenu, hasa wale wanaoitetea CCM kwa njia ya upofu mtasema "hana haja ya kuzungumzia ufisadi – kwani yeye ni mtu wa vitendo."

Binafsi nalikumbuka tukio moja – mapema mwezi Agosti 2008 pale ilipoonekana hakuwa na budi bali kusema angalau kitu kidogo kuhusu ufisadi/wizi wa EPA. Aliingia Bungeni lakini ishu ya EPa ilikuja mwisho kabisa kama dakika 20 za hotuba yake ya karibu masaa mawili ambayo aliongea mambo mengine na iliwafanya wasikilizaji/watazamaji wa hotuba hiyo kuanza kuwaza kwamba hata EPA hataizungumzia.

Lakini hata hivyo hiyo ishu ya EPA ilimpa tabu sana – kwanza alianza kwa kusema eti hizo hela hazikuwa za serikali bali ni hela za Tz zilizowekwa BoT na watu/makampuni binafsi kwa ajili kulipa bidhaa wangeziagiza kutoka nje. Ilikuwa ni enzi ya strict Imports and exchange control – miaka ya themanini. Sawa, hazikuwa za serikali in strict sense of the word, lakini zilikuwa mkononi mwa serikali (BoT) kama mtunzaji (custodian) kwa hiyo hazikupaswa kuibiwa.

Pili haikuwa kweli kabisa kwamba hazikuwa hela za serikali kwani miongoni mwa wawekaji hizo hela yalikuwemo mashirika ya umma yaliyokuwa yakifanya biashara ya uagizaji toka nje kama vile STC, State Motor Corp, Dabco, etc etc – enzi hizo.

Halafu katika speech yake JK alitaja EPA kama mara tatu tu na alikwepa kabisa, au hakuwa na ubavu wa kutaja maneno "wizi", "kuiba," "kuibiwa," au "ziliibiwa" na badala yake aliishia tu kusema "walilipwa", "walipokea," "walichukuwa" etc akimaananisha kilichotokea.

Alionekana ni mtu wa ajabu kabisa kwamba hao jamaa ambao hayo mabilioni ya EPA yalihamia katika umiliki wao bila ya wao kustahili "kuchukuwa", "kupewa" au ‘kulipwa" - wanaitajwe? Hakika ni wezi tu, lakini JK ilimwia vigumu kutaja neno halisi la watu wanaofanya hivyo!

Lakini cha ajabu ni kwamba pamoja na kutokuwa na ujasiri wa kuwaita "wajamaa wale ni wezi, Lakini aliweza hapo hapo Bungeni kujinyakulia mamlaka ya ‘prosecutor' na jaji kwa pamoja na kuwahukumu, tena kwa njia ya kushangaza kabisa – yaani kuwataka warejeshe hela au watinge mahakamani. Utaratibu huu sijui aliutoa katika vitabu gani! Na juu ya ajabu ya ajabu wanasheria wetu (wakiwemo majaji) walikaa kimya tu.Lakini huu ni mfano mmoja tu ambapo JK angalau aliweza kuzungumzia wizi/ufisadi katika serikali yake na swali langu labakia pale pale.

Nawasilisha.
 
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,402
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,402 0
Nami huwa najiulkiza hivyo hivyo. Ni swali la msingi kabisa ulilouliza. na I fear akiingia EL, Tanzania itapiga miaka 20 bila ya hatua zozote kutoka juu kabisa kuutokomeza ufisadi.
 
Femsor The Activist

Femsor The Activist

Senior Member
Joined
Oct 1, 2012
Messages
193
Points
225
Femsor The Activist

Femsor The Activist

Senior Member
Joined Oct 1, 2012
193 225
We,Thubutu yake aanzie wapi kukemea hayo.Hawezi huyu mwenyekiti wa magamba,ye mwenyewe kila siku analalamika kuwa katika chama chake kuna rushwa halafu hachukui hatua yoyote ile utafikiri hana mamlaka.
 
M

Mercyless

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
653
Points
195
M

Mercyless

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
653 195
Acha ujinga wewe, kamwe mtu mwenye akili timamu hawezi kuukata mti alioukalia!!
 
B

blue arrow

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
271
Points
0
B

blue arrow

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
271 0
siku zote kuuliza si ujinga bali wewe unaye mwita mwenzako mjinga ni ndiyo huna akili
take care anda think before saying
huna jipya
 
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Messages
9,255
Points
2,000
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined May 1, 2009
9,255 2,000
Chama legelege huzaa Serikali legelege - "Julius Nyerere"
 
Masaningala

Masaningala

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
543
Points
225
Masaningala

Masaningala

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
543 225
Katika list of shame, jina lake lilitajwa Mwembe Yanga na kamwe hakukanusha. Hivyo ni dhahiri kuwa hawezi kukemea ufisadi maana nae YUMO. Dawa yake ni kwamba ajiandae kujibu atokapo madarakani.
 
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,402
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,402 0
Huyu mjamaa hawezi kuzungumzia ufisadi- anachoweza ni kupiga picha ya pamoja na watu kama akina Ray C wenye kuitangaza Tanzania vibaya!
 
L

Lwesye

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Messages
5,296
Points
0
L

Lwesye

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2012
5,296 0
Muasisi wa Ufisadi kwa vipi atakemea ufisadi,au umesahau the famous Fisadis mtandao,Rostam Azizi, Edward Lowasa,Jakaya Mrisho Kikwete,Zakhia Meghiji,Daudi Bilali,Jeetul Patel,Yusuphu Manji , constructor wa ufisadi vipi ajikemee labda sayari ya dunia itakapogeuka
 
M

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2010
Messages
2,511
Points
0
M

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2010
2,511 0
Mimi zaidi humuona kwenye picha mbalimbali za matukio kama vile kuwashika mikono watoto wa mitani,kukaa kwenye mkeka karibu na mama mlemavu, kupungia wananchi kwenye mikutano,kugongea mikono wananchi,kupiga picha na timu ya taifa, kupiga picha na hashim sabeet, na watu wengine wengi maarufu....kwa kifupi ni mtu wa matukio!!! Zaidi ya hapo anapenda kutabasamu.
 
Mchaga

Mchaga

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
1,381
Points
1,195
Mchaga

Mchaga

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
1,381 1,195
Mbona zipo kesi za ufisadi mahakamani?

Kwani kuzungumzia kwa ukali ndio suluhisho?
 
L

Lwesye

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Messages
5,296
Points
0
L

Lwesye

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2012
5,296 0
Mbona zipo kesi za ufisadi mahakamani?

Kwani kuzungumzia kwa ukali ndio suluhisho?
Kesi yeyote ambayo inamwacha Kikwete ni uonevu rafiki yake Lowassa anasema KIkwete ndie alikuwa ananufaika na milioni 150 kila siku kwa mradi wa Richmond aka Dowans je amepelekwa mahakamani kwa wizi huo mkubwa
 

Forum statistics

Threads 1,285,560
Members 494,675
Posts 30,866,859
Top