Nauliza kwa waliopata mkopo

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,842
8,231
Wapendwa nimepigiwa simu kutoka mkoani na jirani yangu,kijana wake kapata nafasi ya kujiunga Mzumbe University,na pia amebahatika kupata mkopo lakini sasa amemwambia mzazi wake kuwa inatakiwa alipe 700,000 kutoka mfukoni mwake kama registration fee kabla ya Sept 30,sasa nilichoulizwa na huyo mzazi mwenzangu ni kuwa si hela ya mkopo ndio inalipia kila kitu?nami nimeshindwa kumpa jibu kwa kuwa sifahamu,naomba mwenye kufahamu anijulishe ,tumeangalia kwenye hizo form za kujiunga hatujaona sehemu iliyosema inatkiwa hiyo 700,000. mwenye kujua tafadhali atuhabarishe .Asente
 
ndiyo, pesa ya mkopo inalipia ADA yake kwa asilimia kadhaa kwa baadhi ya watu na wengine wanalipiwa yote xa kwa kesi hiyo ni kweli inawezekana kijana wake hakulipiwa pesa yote na bodi (manake hakupata 100%) ndo mana inabidi ajiongeze mwenyewe
 
Asante du huyu jirani yangu sasa hii itakuwa sawa na kiwete kupanda mlima Kilimanjaro
 
unatakiwa utuambie amepata mkopo kwa aslilimia ngapi?????kuna hela unapewa bodi ya mikopo lakini mzumbe unatakiwa ulipe hela ya matibabu, hela ya serikali ya wanafunzi -MUSO, caution money, hela ya malazi, na asilimia yako unayotakiwa ulipe kama mzazi/mlezi, NI INBOX NAMBA YAKo kama unamwswali zaidi
 
Lazma uangalie kuwa kapewa asilimia ngapi. Kuna hela ambayo mwanafunzi analipa mwenyewe kama matibabu, mtihani, tahadhari n.k. Kuna uwezekano hajapewa 100% hivyo kuna kiasi anachopaswa kujilipia. Pitia site ya tcu ucheki kapewa kiasi gani ili urudi hapa upewe jibu sahihi.
 
Kama milioni 3 na elfu hamsini kama sijakosea hivi anaenda BSc Economics
 
Hapa nkweli kabisa. Lazima alipe fedha za usajili kwanza. Akishajisajili chuoni ndio anaweza kupata huo mkopo. Na kama atakua amepata 100% atarudishiwa hizo fedha endapo akidai.
 
Back
Top Bottom