Nauliza kwa nini Agakhan Foundation wanapewa misamaha ya kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nauliza kwa nini Agakhan Foundation wanapewa misamaha ya kodi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by anney, Aug 20, 2012.

 1. a

  anney Senior Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF napenda kufahamu kwa nini taasisi ya Agakhan inapewa misamaha ya kodi hapa nchini kwetu. Nina uliza kwa sababu huduma za Agakhan mfano hospital za Agakhan ni ghali kuliko hospitali zote hapa nchini. Mfano mtoto mdogo wa wiki moja ukimpeleka Agakhan ili alazawe lazima uweke deposit ya laki tano za Tanzania ndiyo apewe huduma ya matibabu. Kumwona daktari ni elfu Ths 40,000-70,000. Shule za Agakhan ada zake nazo zipo juu kulinginishwa shule zingine za binafsi. Je kwanini wapate misamaha ya kodi? Je wanastahili kupewa misamaha ya kodi?
   
 2. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unatafuta ugomvi na akina Pengo wewe! ukianzia huko utakuja kuishia kwa nini Serikali inalipa Kanisa mabilioni ya pesa kwa mwaka halafu bado gharama zao ni za juu sana huku wakipewa misamaha ya kodi, na mwisho wa siku faida inayopatikana katika hizo Hospitali inakwenda Kanisani.
  Unafikiri akina Pengo watakuachia hivihivi uwatilie kitumbua chao mchanga?
   
 3. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mkuu nahisi unakimbia mada. Alichouliza ni uhalali wa kupewa msamaha halafu gharama zao zikawa juu. Nadhani ulipaswa kutaja hospitali gani za hao akina Pengo zenye garama kama au kuliko agakhani ili nazo tuzijadili.
   
 4. Nkwesa Makambo

  Nkwesa Makambo JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 4,765
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ni mjadala mzuri tu,kama umeona hata kanisa lina misamaha lakini gharama ziko juu ni bora ungeongeza idadi ya taasisi za kuhoji uhalali wa misamaha ya kodi wakati zaniajiendesha kibiashara zaidi...
  Ni hoja nzuri ijadiliwe kwa uwazi pasipo kuleta jazba za kidini.
  Binafsi nashindwa kuelewa un NON-PROFIT ORG wa taasisi za AGHA KHAN,kwa kweli wanachuma sana zaidi ya taasisi zingine za kibiashara,ni wakati kuafaka wa serikali kuweka utaratibu wa namna ya kuhakikisha misamaha ya kodi inawanufaisha watanzania kupitia taasisi zinazopata hiyo misamaha.
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Side naona unataka kutupotezea
  Ili suala ata Mbatia aliuliza kwa bunge last time,regence hawana exemption but wanalipa kodi kubwa tuu na gharama zao ni sawa na agha khan
  Ila kwa serikali hii sishangai bse kuna viwanda vinatumia gesi but hawajashusha bei ya bidhaa zao na serikali haifanayi follow up
  So the same to this watu wana exemption but hakuna unafuu wa huduma which make the exemption usesless kwa mwananchi wa kawaida
   
 6. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,980
  Likes Received: 20,368
  Trophy Points: 280
  Hujui unachokisema, Pengo ndo AF, fungua akili yako mkuu. Nachojua RC (na mashirika yao inc. Benedectine) wanamiliki baadhi ya hospital kubwa ikiwemo BMH, Ndanda Mission, Ligula, Peramiho na hizi zote zinatoa huduma kwa bei ya kawaida kabisa na tena zinahudumia jamii kubwa na si matajiri mfano wa AF.

  Makanisa mengine yenye hizi Hospital na bado zinatoza huduma za 'kawaida' ni pamoja na AIC Makongoro, na Kolandoto, KCMC, kutaja machache.
  Na pia hospital za BAKWATA zinatoa huduma kwa bei ya kawaida na ndiyo maana mtoa mada anahoji inakuwaje AghaKhan hospitals zinatoza gharama kubwa wakati anahisi zinapata msamaha kama hospitali nilizojaribu kuainisha hapo juu.

  EID MUBARAK
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Sio mpaka gharama ziwazidi Agakhan hata hospital zingine wanapewa misamaha ya kodi lakini gharama zao zipo juu mfano Bugando Hospital, KCMC Hospital.
   
 8. peri

  peri JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kuna haja ya kuangalia upya misamaha ya kodi hasa kwa taasisi za kidini, wengi hawaitumii ipasavyo.
  Wanafanya biashara badal ya kuhudumia jamii.
   
 9. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  ni kweli Mbatia aliuliza bungeni lakini hoja yake haikujibiwa.Huduma za Agakhani zimelenga daraja la juu la watanzania hivyo kuwepo kwao hakuwasaidii wananchi wa kawaida ambao ni wengi Tanzania.Hindu mandal wanalipa kodi hizo hospital nyingine unazozungumzia za makanisa huduma zake ni za kawaida na hazibagui watu kwa vigezo vya kipato au dini tuna haki ya kujua nini kinaendelea kuhusu kodi zetu na wapi wanapata kiburi cha kupandisha gharama wakati wana msamaha wa kodi
   
 10. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nikifikiria kuwa Kanisa la Pengo lilikuwana mwakilishi wakati wa kusaini ile "MoH" na kwa vile yeye ndiye kinara ndio maana nikamtaja.
  Mkuu! ili kuurahisisha huu mjadala tungeangalia ni kiasi gani cha ruzuku inayopata mahospitali yote ya Kanisa kisha tuioanishe na ruzuku inayopata AghaKhan. Tuangalie pia ruzuku za gharama za ukarabati, elimu kwa wafanyakazi tuoanishe.
  Halafu tuangalie gharama za matibabu kati ya hospitali moja ya Aghakhan na KCMC au Bugando tuoanishe, hii nafikiri itakuwa njia rahisi ya kuwa na munakasha wenye tija au unafikiri kuna njia nyingine rahisi zaidi ya hii kuuendesha huu mjadala?
  Nakumbuka kuna mchangiaji hapa aliye oanisha gharama za kumtibu mgonjwa wake KCMC na India jibu ikawa India ni rahisi zaidi kuliko KCMC, hii ilimlazimu kumpeleka mgonjwa wake India! huyu ni mlipa kodi ambaye kiasi cha kodi yake kinakwenda kama "ruzuku" KCMC na ameshindwa kumtibu mgonjwa wake pale! Serikali pia inapoteza pale pesa ya huyu mlipa kodi inapokwenda kutumika nje ya nchi badala ya kuuingiza katika mzunguko wa pesa nchini.
  Miaka kadhaa iliyopita gharama tu za kujiandikisha Bugando Hospital ilikuwa ni elfu Ishirini!
  MoH inabidi ifutwe pesa za ruzuku zirudishwe (mkataba hauna ridhaa ya walipa kodi) wasioweza kurudisha Hospitali zao ziuzwe ili kufidia na Serikali ichukuwe its own responsibility.
   
 11. a

  adolay JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Alie toa mfano Wa aghakan kidogo ametoa walau pa kuanzia na kusherehesha hoja yake kwa data, anasema kulaza mtoto mdogo walau uanze na deposit tsh. 500,000/=, kumuoana dkr at least uwe na tsh. 40,000 - 70,000.

  Na nyie mnaomension kcmc na .... Tupen data msilete majibu ya kisiasa, lengo tujue nan anadanganya nan anasema ukweli, na taasis zipi zinatuibia misamaha ya kod zetu kwa kututoza zaid.

  Tuache majibu ya jujuu, kisiasa na yenye mtazamo wa kidin.
   
 12. Zux de

  Zux de JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hivi na wewe kumbe uelewa wako bado ni mdogo. Unaweza ukalinganisha gharama ya huduma zitolewazo na bungano na zile za aghakhan.
   
 13. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ameshindwa kutuonyesha KCMC au Bugando gharama zao ni kiasi gani!
  Tukipata tuangalie idadi ya pesa ambazo KCMC inaingiza kutoka Serikalini (Ruzuku,ukarabati, msamaha wa kodi n.k)na Aghakhan nayo inaingiza kiasi gani ili tujumlishe. simple
   
 14. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Dawa ni taasisi za kidini zote zinzofanya biashara zilipe kodi kama ilivyo msumbiji!!Agha Khan wa Bank Diamond Trust,Wana magazeti mwananchi,citizen,wana shule mzizima pia mwingira ana ban efatha,mashamba ya mazao ya biashara!Nadhani mwaka ujao wa fedha waziri atamke juu ya hizi taasisi kulipa kodi
   
 15. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  jibu zur analo nape!
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kuna watu msipomtaja pengo au katoliki hamwezi kupumua eeeh?


   
 17. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Sawa...sasa tuseme eg 1- ECG Bugando ni Tsh..... na Aga Khan ni Tsh......, 2-CT SCAN Bugando ni Tsh.... na Aga Khan ni Tsh...., tulinganishe na kupata jibu zuri
   
 18. F

  Fortune Samuel Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeupenda huu mjadala wanaJF. Badala ya kuangalia Agakhan, ni vizuri tukaangalia mbali zaidi. Hata katika huduma ya elimu, kwamfano, ada anayolipa mwanafunzi wa Tumaini Dar kwa kozi za kawaida za Arts mwaka mmoja inakaribia ada anayolipa mwanafunzi wa UDSM kwa miaka miwili na nusu. Pia ni zaidi ya ada ya SAUT kwa tabribani 1mn kwa mwaka. Hivi, misamaha hii inafanya kazi gani?
   
 19. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu lengo ni kupata suluhisho la maana hivyo sioni tabu yoyote ile ikiwa kila kitu kitawekwa mezani ili kitusaidie katika mjadala wetu huu!
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Nyie ndo mnalichafua jamvi nakuonekana kuwa ni la vilaza. Mada umeielewa au umeamua kutumia moyo wako kuchangia badala ya kutumia kichwa?

  Tupe mchanganuo wa ughari wa huduma zao basi mkuu. Kuongea tuuuu kila mtu anaweza kuongea. Kuthibitisha anachokiongea mtu ndo kutafanya hoja yake kuwa na nguvu!
   
Loading...