Nauliza kuhusu talaka na kugawana mali kisheria

pitapitapita

Member
Nov 2, 2010
10
0
mie nimeachana na mke wangu, lakini wakatu tuanakutana miaka 8 iliyopita nilikuwa na nyumba na shamba kubwa tu, baada ya mambo kutokwenda vizuri, tuliamua kuachana. huyu mama tulionana bomani. sasa alikwenda mahakamani kudai haki yake na mahakama ikaamuru kila kitu kiuzwe na angawiwe asilimia 20%.
1. je vile vitu alivyonikuta nayo vinaingiaje hapa katakia mgawo?
2. je hii asilimia 20% iliyotolewa ni sheria gani inasema hiyo

tafadhali ndugu zangu nisaidieni
 
subiri uchaguzi uishe nitachangia, ila angalia muda wa rufaa usipitilize bila kukata rufaa!
 
Pole pita pita muachie tu wife bwana miaka minane uliyokaa nayo si haba mgawie akaanze maisha..
Je mna watoto nae?
 
Mie nilizani 50%, wanawake mara nyingi sana uzurumiwa na kulaghaiwa kimapato na wanaume zao. Kama ulienda kuoa mke mwengine ukamuini mkeo je? kama ulikua na wanawake wengine pembeni ukiwaonga maela je? Je hizo mali zitarudi zisabiwe hapo?
 
Wanaume inabidi tuwe macho na ikibidi tuachane na taratibu hizi za kufunga ndoa.
 
tafuta msaada wa kishria kwa wanasheria maana naona wote wanaokujibu hakuna anayejua sheria za ndoa. Au hata ktk website google pengine utazipata
 
mie nimeachana na mke wangu, lakini wakatu tuanakutana miaka 8 iliyopita nilikuwa na nyumba na shamba kubwa tu, baada ya mambo kutokwenda vizuri, tuliamua kuachana. huyu mama tulionana bomani. sasa alikwenda mahakamani kudai haki yake na mahakama ikaamuru kila kitu kiuzwe na angawiwe asilimia 20%.
1. je vile vitu alivyonikuta nayo vinaingiaje hapa katakia mgawo?
2. je hii asilimia 20% iliyotolewa ni sheria gani inasema hiyo

tafadhali ndugu zangu nisaidieni
Office hii hatushughuliki na mambo ya sheria hapa ni malavidavi toka nje zunguka nyuma utakuta mlango umeandikwa Jukwaa la sheria huko nikila kitu unachotaka kuuliza watakusaidia hata katiba yakuoa!!karibu tena kwa issue za malavidavi!:bowl:
 
Pole pita pita muachie tu wife bwana miaka minane uliyokaa nayo si haba mgawie akaanze maisha..
Je mna watoto nae?

pitapitapita, hapa kuna ushauri mzuri sana kwako. kuishi miaka 8 si mchezo. talaka si uadui. kama mna watoto itapendeza sana hata ukimwongezea mgao zaidi ya uliotolewa na mahakama kwa manufaa ya watoto na yeye pia. usikate mawasiliano wala kuacha kutembelea watoto kama mahakama imeamuru wakae na mama yao.

mimi nilitaliki miaka miwili iliyopita na tulikuwa na watoto wawili wakati huo ambao walikuwa wadogo sana na mahakama iliagiza waishi na mama yao na mimi nipeleke matunzo kila mwezi, sikuwahi kukosa kuzidisha hela ya mtunzo ya kila mwezi hata mara moja. krismass ya kwanza baada ya talaka nilimpelekea zawadi na kumpa hela ya sikukuu. hapo sikuamrishwa na mahakama na kila nikimkumbuka huwa namtumia hela kidogo kwa m-pesa na huwa anafurahi kuzipokea. baadaye nilipa kiwanja changu kimoja kilichokuwa tabata na nilikinunua baada ya talaka na sasa naendelea kumjengea nyumba na karibu inaisha.

tangu talaka itolewe mi ndiye namlipia kodi ya nyumba pale anapoishi na mahakama haikuniamuru kufanya hivyo, nafanya kwa mapenzi yangu tu kwake na kwa watoto wetu. nimepanga nikimaliza kumjengea hiyo nyumba nitamnunulia gari na ndipo nitaanza kujenga yangu. lengo ni kumthibitishia kuwa nilimpenda kwa dhati na kuwakinga watoto na athari zozote za talaka.

wewe unashindwa nini kumwchia 20%? nakushauri kama uwezo wako kimaisha ni mzuri kupita wake, endelea kumtunza hadi akatae mwenyewe. na kama mna watoto mgawie hata 70% ya mali uliyonayo na Mungu atakubariki utapata zaidi.

ubarikiwe sana
 
Nyie mliotaliki tuna waanzishia jukwaa lenu ilimwaelimishe wengine wenye nia hiyo!!MoD pls
 
ok mimi sijajua hakuna sheria inayolinda divorce Tanzania .. kwa sababu nchi nyingi huwa watu wanaenda 50/50 baada ya kuachana haijali mmeoana kwa muda gani.. ndo maana watu wenye mali sana wanachukuaga prenuptial agreement ...
 
Miaka nane Kaka si mchezo!!! Mungu hapendi talaka. Ni kosa gani hilo lisilosamehewa jamani? Talaka si nzuri. Kuishi na mtu ambaye si ndug u yako ni kazi kubwa sana kwanza mtatofautiana tabia na vingine vingi tu hapa kitu cha msingi ni UVUMILIVU!! Kama umeweza kukaa nae miaka nane unashindwa nini kuendelea nae au ndo ushapata mwingine unamuona hafai? Au yeye kapata mwingine zaidi yako? so anakuwa na kiburi hata ukimpatia talaka hana wasiwasi? Hili jambo zito sana usiliongelee kirahisi tu kuwa unampa talaka itakugharimu kaka yangu kaa chini na ufikirie mara mbili mbili kuachana si kuzuri kwa kipindi chote mlichokaa mie sikushauri kabisa kiukweli. Unless unasababu ambazo wewe mwenyewe unazijua kuwa una mwingine na yeye ana mwingine lakini kama ni makosa ya kawaida tu SAMEHEANENI!!! Watu wanazaa nje ya ndoa na maisha yanaendelea bwana
 
Wandugu asante sana kwa yote.
ila, safari imeshaanza sirudi nyuma, asanteni kwa yote nitafanyia kazi la kila mmoja, na kupata shulihisho.
kakakiiza, nitapita vile vile mlango wa pili.
 
wandugu asante sana kwa yote.
Ila, safari imeshaanza sirudi nyuma, asanteni kwa yote nitafanyia kazi la kila mmoja, na kupata shulihisho.
Kakakiiza, nitapita vile vile mlango wa pili.

kuna maisha pia hata baada ya talaka, wengine tumeishazoea na tunapumua sasa!! Manake ndoa ilikuwa kazi kwelikweli
 
Alitakiwa apate 50%, nadhani atakata rufaa muda si mrefu!
 
pitapitapita, hapa kuna ushauri mzuri sana kwako. kuishi miaka 8 si mchezo. talaka si uadui. kama mna watoto itapendeza sana hata ukimwongezea mgao zaidi ya uliotolewa na mahakama kwa manufaa ya watoto na yeye pia. usikate mawasiliano wala kuacha kutembelea watoto kama mahakama imeamuru wakae na mama yao.

mimi nilitaliki miaka miwili iliyopita na tulikuwa na watoto wawili wakati huo ambao walikuwa wadogo sana na mahakama iliagiza waishi na mama yao na mimi nipeleke matunzo kila mwezi, sikuwahi kukosa kuzidisha hela ya mtunzo ya kila mwezi hata mara moja. krismass ya kwanza baada ya talaka nilimpelekea zawadi na kumpa hela ya sikukuu. hapo sikuamrishwa na mahakama na kila nikimkumbuka huwa namtumia hela kidogo kwa m-pesa na huwa anafurahi kuzipokea. baadaye nilipa kiwanja changu kimoja kilichokuwa tabata na nilikinunua baada ya talaka na sasa naendelea kumjengea nyumba na karibu inaisha.

tangu talaka itolewe mi ndiye namlipia kodi ya nyumba pale anapoishi na mahakama haikuniamuru kufanya hivyo, nafanya kwa mapenzi yangu tu kwake na kwa watoto wetu. nimepanga nikimaliza kumjengea hiyo nyumba nitamnunulia gari na ndipo nitaanza kujenga yangu. lengo ni kumthibitishia kuwa nilimpenda kwa dhati na kuwakinga watoto na athari zozote za talaka.

wewe unashindwa nini kumwchia 20%? nakushauri kama uwezo wako kimaisha ni mzuri kupita wake, endelea kumtunza hadi akatae mwenyewe. na kama mna watoto mgawie hata 70% ya mali uliyonayo na Mungu atakubariki utapata zaidi.

ubarikiwe sana

Acha kumpumbaza mwenzio na unafiki wako
 
Back
Top Bottom