Nauliza hospital ya Muhimbili wodi ya watoto (makuti ) ni yanani?

jike la simba

JF-Expert Member
Jan 3, 2017
494
347
Habari wanajamvi!
Nilienda juzi kumuangalia mpendwa wangu wodi ya watoto inaitwa makuti, nilipofika pale nikamtuma mtu aniitie mpendwa wangu nje maana awaruhusu kuingia ndani wodini kunakisehemu maalumu chakukutana na wapendwa wetu . Nae akaja na tukazungumzo na kujuliana hali ya mtoto. lakini kilichonishangaza katika mazungumzo yake akawa analalamika huduma hafifu na bili kubwa ya kitanda na matibabu kwa yeye alie kaa siku 3 vipimo vyote Vya mtoto takribani tsh 161,000. Nikajiuliza Sera ya nchi si wanasema watoto kuanzia mwaka 1 adi 5 huduma bure nikajaribu kumuulizia mwingine akaniambia Mimi nadaiwa laki 5 mumewe kamwambia akae atamgomboa siku akipata pesa .sikuchoka nikajaribu kuuliza zaidi nikaambiwa kuna mama alienda kulalamika adi kwa mkuu Wa mkoa lakini akajibiwa akalipe tu! Aina namna dhuuuu nikaona bora nilete huku kwenye jukwaa nipate kujua zaidi hospitar ya Muhimbili wodi ya watoto MAKUTI NI YANANI?
 
Pale muhimbili kuna huduma za namna mbili....
1. Rufaa
Hawa ni wale wagonjwa waliokwenda pale kwa rufaa kutoka hospitali za wilayani mwao kama Temeke, Amana, etc...Ukitoka hapo ukawa reffered kwenda Muhimbili utapata hizo advantages za watoto bure na matibabu bei rahisi

2. Huduma ya pili inaitwa Fast Track...Au Private....Hii ni pale unapoamua wewe moja kwa moja kwenda muhimbili bila kupitia rufaa....Hapa sasa ndo kuna balaa......Wana bei sio kawaida....Niliwahi kutonywa na mhasibu mmoja hapo kuwa wanaweka bei kuwa ili kudiscourage tabia ya kwenda muhimbili moja kwa moja.....Yani kwa huduma hii kulipa laki 5 au 6 ni kawaida sana....Tena kwa matibabu ya hovyo balaa.....Mimi kuna mgonjwa wangu alilazwa mwanaye hapo mtoto mchanga, ikabidi na mama mtu wampe kitanda ili aweze kumhudumia mtoto....Walikaa siku tatu tu, mtoto alichajiwa laki 3,na mama laki 3.....matibabu aliyokuwa anapata mama mtoto ni yule daktari wa zamu kupita na kumpima presha tu asubuhi.....

Hiyo ndo muhimbili dadangu
 
mkuu yeye anafikiri bombrider uwanja na ghorofa la tra kijijini ndio maendeleo ndio maendeleo

anasahau huduma muhimu za kijamii wanaishia kupeleka sabuni kama misaada

ila tuvumilie tuu maana ukiuliza unaeza ukaambiwa sio siri kali iliokufanya uumwe
 
Pale muhimbili kuna huduma za namna mbili....
1. Rufaa
Hawa ni wale wagonjwa waliokwenda pale kwa rufaa kutoka hospitali za wilayani mwao kama Temeke, Amana, etc...Ukitoka hapo ukawa reffered kwenda Muhimbili utapata hizo advantages za watoto bure na matibabu bei rahisi

2. Huduma ya pili inaitwa Fast Track...Au Private....Hii ni pale unapoamua wewe moja kwa moja kwenda muhimbili bila kupitia rufaa....Hapa sasa ndo kuna balaa......Wana bei sio kawaida....Niliwahi kutonywa na mhasibu mmoja hapo kuwa wanaweka bei kuwa ili kudiscourage tabia ya kwenda muhimbili moja kwa moja.....Yani kwa huduma hii kulipa laki 5 au 6 ni kawaida sana....Tena kwa matibabu ya hovyo balaa.....Mimi kuna mgonjwa wangu alilazwa mwanaye hapo mtoto mchanga, ikabidi na mama mtu wampe kitanda ili aweze kumhudumia mtoto....Walikaa siku tatu tu, mtoto alichajiwa laki 3,na mama laki 3.....matibabu aliyokuwa anapata mama mtoto ni yule daktari wa zamu kupita na kumpima presha tu asubuhi.....

Hiyo ndo muhimbili dadangu
Asante nimekuelewa mdau
 
Back
Top Bottom