Nauliza: Hivi ile ban ya Mikusanyiko wakati wa SENSA imeisha saa ngapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nauliza: Hivi ile ban ya Mikusanyiko wakati wa SENSA imeisha saa ngapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by S2dak_Jr, Sep 10, 2012.

 1. S2dak_Jr

  S2dak_Jr Senior Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi,


  Kumbukumbu yangu ni kuwa mikusanyiko ya watu, ikiwa na ya siasa ilikatazwa kwa sababu ya Sensa.

  Hii ikiwa ni pamoja na kukatazwa/kusitishwa kwa kazi zote zilizokuwa zikifanywa na chama cha siasa cha CHADEMA.

  Kwa taarifa tu ni kwamba juzi mkusanyiko mkubwa ulifanyika mkoani Tabora kwenye kile kinachoitwa tamasha la Fiesta linaloendeeshwa na Clouds Media.

  Pia kuna tetesi kuwa Mh. Mwigulu Nchemba akishirikiana na Nape Nnauye wamefanya Mkutano wa kisiasa Mjini Igunga.

  Na pia Mh. Mwigulu alikuwa kwenye mkusanyiko wa kisiasa Kiomboi Iramba ikiambatana na zoezi la uchaguzi wa UVCCM wa wiilaya ya Iramba.

  Kama hiyo haitoshi, mpaka muda huu kuna mkusanyiko wa watu unaoendelea mpaka muda huu Mjini Singida kwenye tamasha la Fiesta la Clouds Media na linarushwa moja kwa moja kupitia Clouds Fm tangu mchana wa jana. Na sijajua kibali cha tamasha hili kinaisha muda wake saa ngapi. Kwani mpaka saa saba ya usiku huu tamasha hilo linaendelea Mjini Singida.

  Swali: Je katazo la mikusanyiko ni kwa ajili ya watu fulani au CCM na Clouds Media hao wana exemption kwenye hili katazo?

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. S

  Starn JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sensa ilipoisha
   
 3. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,322
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hili Tangazo/katazo lilikuwa maalum tu kwa CHADEMA kwa vile wao ndo wana historia ya kuvuta watu wengi zaidi kwenye mikutano yao, na uchunguzi wa kipolisi unaonesha wapenzi na wanachama wa CHADEMA huwa wanasafiri kwa pesa zao kwenda umbali mrefu sana tu ili wakasikilize hotuba za makamanda, kwasababu hiyo ilibidi sirikali iwapige ban kwa muda CDM.
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu sensa imeisha, au umelewa mbege ndo ukapost huu uzi?
   
Loading...