Nauliza: Akiondoka Pinda, Bunge laweza kuitishwa kwa ajili ya kumthibitisha Waziri Mkuu mpya?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Nauliza tu ili nipate kujua. Hivi PM akijiuzulu (au akiachishwa kazi) wakati Bunge halikutani inakuwa vipi? Kikao cha Bunge kitaitishwa ili kithibitishe PM Mpya?

Au nafasi ya PM itakaa wazi hadi kikao kijacho cha Bunge?

Nauliza hivi kwa sababu uwezekano wa Pinda sasa hivi kuondoka ktk nafasi hiyo ni mdogo sana kwani Bunge kukutana tena ni zaidi ya mwezi mmoja kutoka sasa. Hivyo Pinda tunaye tu hadi wakati huo.

Nauliza tu jameni.
 
Sijui Katiba inasema vipi. Lakini nadhani bunge la siku moja laweza kuitishwa kum-confirm PM.
 
Nadhani ni lazima bunge liitiswe kumthibitisha, ila sikumbuki vizuri J.Malechele alivyotolewa, nakumbuka tu alipwe Mzee Msuya ila sijui kama bunge lili mthibitisha
 
NDIO.

Lakini kuitisha bunge la dharura kwa ajili ya kura ya kutokuwa na imani na Pinda isingewezekana, kwa mujibu wa madam Makinda.
 
Endapo Rais atavunja baraza la mawaziri atalazimika kumchagua Waziri Mkuu (WM) mwingine ambaye ndani ya siku 14 toka baraza lilipovunjwa ni lazima athibitishwe na bunge. Na hata pale atakapomteua tena WM aliyekuwepo, maadam atakuwa amevunja bunge, basi WM huyo itabidi apigiwe kura na bunge. Hivyo, itabidi liitishwe bunge la dharura.
 
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku
kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua
Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi
anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi
Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge
wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio
wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika
madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa
na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge
walio wengi.
hiki kipengele cha katiba kinaonyesha waziri mkuu hawezi kushika madaraka hadi athibitishwe na bunge kwa hiyo kama baraza lkivunjwa akateuliwa waziri mkuu mpya lazima bunge kuitishwa kumthibitisha

55
.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la

Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada
ya kushauriana na Waziri Mkuu.
 
Nadhani ni lazima bunge liitiswe kumthibitisha, ila sikumbuki vizuri J.Malechele alivyotolewa, nakumbuka tu alipwe Mzee Msuya ila sijui kama bunge lili mthibitisha

Uthibitishwaji wa Waziri Mkuu ulianza 1995 mara baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Mkuu angekuwa na maamuzi sahihi angefutilia mbali baraza wakati wa kikao cha Bunge kilichopita kwa kuacha kwenda kwenye mazishi kule Malawi
 
hivi pinda akijiuzulu halafu mawaziri wale mafisadi wakaachwa nini kitakuwa kimefnyika?
 
Excellent, WM akijiuzulu na mawaziri wote (pamoja na manaibu) wanapoteza nafasi zao! Ndicho kilichotokea baada ya WM Lowassa kujiuzulu. Waziri Mkuu akifa mawaziri wote nao wanapoteza nafasi zao! Huwezi kuwa na baraza la mawaziri bila ya waziri mkuu. Ndio maana wengi wetu tunaamini kitakachotokea ni "major reshuffle" yaani WM haguswi isipokuwa karibu mawaziri wengine wote wanahamishwa, kuondolewa au kuingizwa wapya!
 
Kwa hiyo ndio kusema ili kuepuka mtego wa kuitikishwa kwa bunge la dharura maana yake ni kwamba kitakachotokea ni major reshuffle tu na mtoto wa mkulima ataendelea kupeta tuuu.

Kaazi kweli kweli
 
Sahau,Pinda hana tatizo lolote hawezi ondolewa ata kidogo wenye matatizo ni mawaziri,Pinda ni kiongozi safi na muwajibikaji hana machafu yoyote,tafadhari Mh Mizengo husijeondoka kwa kujiuzulu wala Mh Raisi husijemuondoa huyu jamaa ni kiongozi safi kiuadilifu na kiutendaji!
 
Hivi neno kusuka upya lina maana ya kufanya mabadiliko makubwa bila kumgusa WM? Mimi nilidhani Rais angevunjilia mbali Baraza la Mawaziri na kuanza kusuka upya kuanzia kwa PM kwenda huko chini. Vunja kaa hata wiki moja bila Mawaziri Makatibu wakuu wafanye kazi baada ya wiki teua PM athibitishwe na Bunge mkae chini msuke sasa serikali. Hii ya kusema major reshuffle mimi siiipendi napenda kusuka upya kwa maana ya kuvunjilia mbali baraza la mawaziri.
 
Kwa hiyo ndio kusema ili kuepuka mtego wa kuitikishwa kwa bunge la dharura maana yake ni kwamba kitakachotokea ni major reshuffle tu na mtoto wa mkulima ataendelea kupeta tuuu.

Kaazi kweli kweli
Kuepuka huo mtego anaweza kuwafuta woote kazi aoambakisha waziri mkuu tu wakaanza upya kuuunda serikali ila akimgusa tu PM tujue Bunge la dharura linakuja.

Kuna mtego mwingine hapa: Huyu Mama, Asha Rose Migiro anatajwatajwa sasa yeye ataingiaje kama baraza litaundwa bila kuitisha bunge? Yeye si mbunge na ili uwe waziri unatakiwa uwe Mbunge. Kwa maana hiyo atamteua awe mbunge sawa lakini inabidi aapishwe na spika ja kuapishwa inakuwa kwenye kikao cha bunge. Huu mtego mwingine kama kweli huyu mama anatakiwa awemo kwenye baraza.
 
Yeye kuwemo kwenye baraza sio shida. Kumbuka Rais ana nafasi 10 za kuteua wabunge. nadhani ametumia kama 5 au 6 hivi. Hivyo anaweza kumteua kama mbunge na kisha kumpa uwaziri ila sio uwaziri mkuu. Waziri Mkuu anatakiwa atoke kwenye wabunge wa kuchaguliwa. maana yake kutoka majimboni.
 
Mkuu Maishamapya suala hapa ni kwamba unaweza kuapishwa kuwa waziri bila kuapishwa kwanza kuwa mbunge? Kuteuliwa sawa sina shida ila mbunge anaapishwa kwenye kikao cha bunge. Hivyo kama anamtaka na anasuka uoya serikali kabla ya kikao cha kawaida cha bunge itabidi kiitishwe ili aape ndipo aape kuchukua Uwaziri.
 
Last edited by a moderator:

Nimekupata! Hilo halina shida mkuu. Wabunge huteuliwa ama bunge liko kwenye session au la. Cha kwanza atamteua kama mbunge na kikao kinachompitisha huyo WM ndicho kitakachomwapisha huyo mbunge mpya. Hayo ni mambo ya process tu.
 
Back
Top Bottom