TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,731
- 21,133
Hata kama ni mapendekezo sidhani kama mlifikiria au kuwaza kwa kinagaubaga, huko Anatorglo mnaenda kupaka mafuta ili kung'arisha hiyo nauli na si vinginevyo.
Ukute mmeshaandaa wazungumzaji wenu wa kutetea hiyo nauli na hapo ndiyo watakuwa wengi ukumbini.
--
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu nauli za abiria kwa treni ya njia ya Reli ya Kisasa – ‘Standard Gauge Railway’ (SGR) zitakavyotumika kwa huduma ya usafiri wa treni za abiria.
Kwa mujibu wa Kifungu Na. 21 cha Sheria Na. 3 ya LATRA, 2019 Mamlaka inapaswa kukusanya maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia viwango vya nauli kwa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwemo nauli za treni.
Katika kulitekeleza hilo, Mamlaka imeandaa mkutano wa kupokea maoni ya wadau wa usafirishaji, ikiwa ni pamoja na watoa huduma, watumiaji wa huduma na wananchi kwa ujumla. Mkutano utafanyika tarehe 19 Disemba 2022 jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Anatorglo.
Nauli zinazopendekezwa na TRC ni Kama ifatavyo:
Kutokana na umuhimu wa mkutano huo, LATRA inawaalika wadau wa sekta ya reli na wananchi kwa ujumla kushiriki katika mkutano huo wa kukusanya maoni ya wadau.
Vilevile, wadau wanaweza kuwasilisha maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu kwa maandishi kupitia LATRA Makao Makuu, Mtaa wa Tambuka Reli, Dodoma au ofisi za LATRA zilizopo Makao Makuu ya kila mkoa Tanzania Bara kabla ya tarehe 3 Januari 2023.
Aidha, maoni ya wadau yanaweza kutumwa kwa barua pepe kupitia anuani hizi: info@latra.go.tz na dg@latra.go.tz

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano – LATRA
06 Disemba, 2022