Nauli na mafao ya askari wastaafu kucheleweshwa ni mateso

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Si kila askari alijiandaa kuwa na kitega uchumi akiwa kazini lahasha, lakini sasa kwanini anapostaafu asipewe nauli ya kumrudisha kwao kwa wakati ili aende apambane na mashamba?

Swala hili viongozi na Waziri wa mambo ya ndani alitolea ufafanuzi lakini hamna utekelezaji sijui ni kumbembeleza mtoto kwa pipi au la.

kwa sasa mtu anastaafu nauli yake haiji baada tu ya kustaafu, fuatilieni ni wangapi wapo makambini wanasubiri nauli na wameisha staafu na nauli hizo hazii, watu wamekaa miezi sisi tukiwemo, pensheni ndio usiseme, mfuko wa pensheni PSSSF wanasema Serikali.

Inachelewesha kulipa Michango ya wanachama wake ndio maana na wao wanachelewa kuwalipa pensheni zao, serikali hiyo hiyo ndio inayotoa maagizo watu walipwe mapema, sasa hawa watu wanatuonaje sisi mfano, sasa hapa tunashindwa kuelewa ni kampeni ili wapate kura za wastaafu au ni nini.

Wastaafu kama askari wamekuwa wakitaabika baada ya kustaafu, si nauli ya kurudi kwao si pensheni hamna kitu, huenda NSSF inayokusanya michango ya private sector wana unafuu sana labda, ila PSSSF imetuchosha mno mno.

Sidhani kama kuna huruma yoyote ile kwa wastaafu wa PSSSF.
 
Jifunze kupitia wenzako,
Umeona alistaafu hajalipwa pesa ya nauli(masurufu) wewe weka akiba ili ukistaafu isiwe kadhia kwako au ukiona unakaribia kustaafu omba uhamisho ukastaafu kwenu ambapo hautahitaji nauli kubwa, mfano unafanya kazi Sumbawanga na wewe kwenu Zanzibar hamia hata Dar kabla hujastaafu ili ukistaafu unakuwa upo karibu.

Wananchi wengi hawapendi polisi kwa sababu polisi wamekuwa sio rafiki kwa raia kutokana na matendo yao. Kama wavyokamata boda boda bila mpangilio, kuna boda boda wengi wamekufa kwa sababu ya kukimbizwa na polisi mwishoe inatokea ajali na mtu anaumia, kuna mambo meeengi yanayofanya polisi wasiwe rafiki wa raia.
 
Nyie askari ni watu msiojielewa kabisa. Ndio maana mnakaa kwenye mahema mpaka mnastaafu. Anayewahurumia, hana akili. Subirini 2025 ili muingize kura za kufoji za CCM kwenye vituo vya kura. Hicho ndio mnachoweza. Ndio maana kiongozi wenu anaitwa Zirro.
Hilo povu sio mchezo

Nje ya mada kidogo:
Omusolopagasi maana Ake Ni Nini, Kuna nyimbo ya professor Jay nmeskia ameimba ilo neno pia.
 
Si kila askari alijiandaa kuwa na kitegea uchumi akiwa kazini lahasha, lakini sasa kwann anapostaafu asipewe nauli ya kumrudisha kwao kwa wakati ili aende apambane na mashamba? Swala hili viongozi na Waziri wa mambo ya ndani alitolea ufafanuzi lakini hamna utekelezaji sijui ni kumbembeleza mtoto kwa pipi au la...
Pole port wamekusikia
 
Si kila askari alijiandaa kuwa na kitegea uchumi akiwa kazini lahasha, lakini sasa kwann anapostaafu asipewe nauli ya kumrudisha kwao kwa wakati ili aende apambane na mashamba? Swala hili viongozi na Waziri wa mambo ya ndani alitolea ufafanuzi lakini hamna utekelezaji sijui ni kumbembeleza mtoto kwa pipi au la...
Mwambie avumilie baada ya miezi 6 au saba ivi huenda shimo likatema nasema ivyo kutokana na experience niliyo ishuhudia live kwa ndugu wa karibu

Baada ya kudtaafu aumia sanaa miezi kama 7 iv lkn shimo lilipotema maumivu yote yametoweka .........ila mkumbushe tu huyo afande mstaafu asiketi tu home yampasa afuatilie route za Psssf ziwe nyingi kuliko hata za vikaao vya harusi
 
Mkuu mbona huwapendi police kiasi hicho,hao ni walinzi wa raia na mali zao wakikosekana siku 3 tu utaaona mziki wake ulivyo.
Huwajui police wewe----Badala ya kulinda wanachukua hata kile kidogo ulicho nacho!

Naunga mkono hoja
 
Nyie askari ni watu msiojielewa kabisa. Ndio maana mnakaa kwenye mahema mpaka mnastaafu. Anayewahurumia, hana akili. Subirini 2025 ili muingize kura za kufoji za CCM kwenye vituo vya kura. Hicho ndio mnachoweza. Ndio maana kiongozi wenu anaitwa Zirro. Na tangazo lenu la kazi eti mnataka fomu 4 division 3 na 4 tu!! Yaani katika wasomi wote waliojaa Tanzania, nyie mkaona fomu 4 division 3 ama 4 ndio mtaji wenu!! Lo!! Kweli mtaji wa CCM ni nyie wajinga.
Nimeshangaa sana hilo tangazo.. Yaani 2021 bado sector muhimu kama police wanaprefer division 4? Sijui kwanini hawakuacha wazi watu waombe, wapembue wenyewe huko.. Kuliko kusema wanataka division 4?
 
Back
Top Bottom