Nauli mabasi ya mikoani zimepandishwa habla ya muda waliotangaza LATRA

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,302
5,439
wzururaji-pic-data.jpg

Licha ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) kutangaza kuwa mabadiliko ya bei za nauli za daladala na mabasi zitabadilika kuanzia Mei 14, 2022, asilimia kubwa ya makampuni ya mabasi yalishaanza kutumia bei hizo mpya.

Safari ya Dar es Salaam kwenda Dodoma inatozwa Tsh 26,000 badala ya Tsh 24,000. Nauli ya Dar es Salaam kwenda Morogoro imekuwa Tsh 10,000 badala ya Sh9,000.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema suala la watoa huduma kupewa siku 14 ndiyo waanze kutoza nauli mpya ni la kisheria.

“Sheria inawataka kabla ya kutoza nauli mpya wampe taarifa abiria ndani ya siku 14 na katika kipindi hicho nasi tutachapisha katika Gazeti la Serikali,” alisema.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa tayari imetumwa timu ya watumishi wa LATRA katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli kwa ajili ya kutoa elimu na kudhibiti utozaji wa kiwango hicho cha nauli mpya.
 
Back
Top Bottom