Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,735
- 40,858
Inaonekana sasa tunataka kuwa kama watu wanaocheza michezo ya kombolela! Watu tunanyemeleana na kusubiri mtu haangilii halatu tuje kuwakomboa wengine! Suala la Polepole ni mfano wa jinsi gani katika kutafuta makosa ya Magufuli ndugu zetu wengine wameamua kabisa kukataa kuangalia kwa uyakinifu hoja zao.
Hapa naona watu wanajaribu kutengeneza mlima kutoka kwenye kichuguu! Imewekwa nukuu ya Humphrey Polepole akionesha kuhoji na kupinga nafasi za Ukuu wa Wilaya na Ukuu wa Mkoa. Kwamba kwa hoja zile za wakati Bunge la Katiba basi Polepole asingepaswa au kukubali nafasi ya Ukuu wa Wilaya; Kisa? Ati kwa vile aliupinga kwenye mjadala.
Polepole alikuwa anajadili masuala ya Katiba Mpya, ulikuwa ni mjadala ambao alikuwa na msimamo wake. Kama hoja ya kuwa kilichopendekezwa hakikurudi na watu basi hawatakiwi basi wabunge wote waliotaka serikali tatu hawapaswi kutumikia serikali mbili! Kama maneno ya watu waliyoyatoa kwenye Bunge la Katiba yanatosha kuwa msumari wa wao kutokutumikia popote kinyume na misimamo hiyo basi wengi ambao walisimama kutaka Serikali Tatu na hata wakagoma Bungeni kuonesha msimamo wao hawapaswi kurudi kutumikia Bunge la Serikali mbili au hata kulia kiapo kuilinda Katiba iliyoundwa kusimamia serikali mbili!
Ama walichokuwa wanakisimamia kule Bungeni walikuwa wanamaanisha kweli kweli au ilikuwa porojo; kama walikuwa wanamaanisha kweli kweli basi hawakupaswa kabisa kurudi kwenye Bunge la Serikali Mbili! Lakini sote tunajua kuwa ule ulikuwa ni mjadala ambao walitakiwa kutoa maoni yao na maoni yao hayawezi kuchukuliwa kama kisu cha kuwashikia nacho shingoni!
Kupinga kitu katika mjadala haina maana mtu hawezi au hapaswi kutumikia status quo. Mjadala huu hauna mantiki kwa sababu ukishauchukua na kukubali kigezo hicho kimoja basi huwezi kukomea hapo. Wengine walipinga hata uwepo wa Muungano lakini leo wanatumikia ndani ya Muungano huo huo; wengine walipinga mambo ya Tume ya Uchaguzi lakini hao hao wakaenda kushiriki Uchaguzi chini ya tume ile ile!
Ni lazima tuweze kutofautisha misimamo katika mijadala vingineyo tutajikuta tunafungana wote kwani ukimfunga kamba mwenzio mguu na yeye anatafuta kamba hiyo hiyo kukufunga wewe mkono. Usishtuke tu 'eh kwani lazima na mimi unifunge"?