Natural disasters: TZ how well preparedness are we?. Najua Uwezo Kuzuia Hatuna, Lakini hata communications alert tuu ya what to do tunashindwa?!,

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,351
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,351 2,000
Wanabodi,

Niko mkoani Lindi katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Malaria, ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi, katika uwanja wa Mpilipili.

Maadhimisho haya sasa hivi ndio yameahirishwa on the spot, licha ya taarifa za uwezekano wa Kimbunga kukumba mikoa ya Mtwara na Lindi, kwa nini maadhimisho haya hayakuahirishwa tangu baada ya kupokelewa kwa taahadhari ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kuhusu Kimbunga?.

Tangu juzi tumeingia Lindi, tahadhari iliishatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Maadhimisho haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mgeni rasmi ni Waziri, ambaye alipaswa kufika Lindi jana. Waziri hakufika baada ya kuzuiliwa ile jana, tungekuwa na good disaster communications, jana hiyo hiyo Tangazo la kuahirishwa kwa shughuli hii lingetolewa, leo asubuhi watu tungejidamkia kurejea makwetu.

Wenzetu wazungu wako very serious na taarifa hizi, baada tuu ya kupokea taarifa za kimbunga, Wazungu wa US AID waliondoka Lindi jana hiyo hiyo, hivyo leo asubuhi kwenye mabanda yaa ya maonyesho yalikuwa tupu.

Mamlaka ya Hali ya Hewa, TMA, wamefanya kazi nzuri kwa kutoa tahadhari well ahead in time, Serikali yetu ilipaswa iwe na mfumo wa taarifa za majanga, ilipaswa serikali kuu kutoa taarifa mikoa ya Mtwara na Lindi, na Wakuu wa Mikoa hiyo walipaswa kuitisha Press Conferences immediately kutangaza taarifa hizo na nini cha kufanyika.

Hata hivyo, nimeongea na Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Dr. Leonard Subi, na kumuuliza kwa nini hawakuahirisha toka jana usiku baada ya Waziri wake kuzuiwa kuja Lindi, Dr. Subi ametoa a very good reason ya kutotangaza jana usiku, amesema wangetangaza usiku, kunge send a panic wave, hivyo watu wasingelala usiku kucha kutaka kujiokoa, hivyo kungeweza kusababisha madhara, ndio maana wamesubiri asubuhi na kutangaza, ili angalau movements zifanyike mchana.

Kutokana na kutokuwepo kwa taarifa rasmi, wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara, wame panick, wenye uwezo wa kuhama, wamezikimbia nyumba zao, mabasi yote yako full, makundi makubwa ta watu Stendi ya Mkoa na hakuna mabasi!.

Tulipata Janga la Tetemeko la Ardhi Bukoba, tukashuhudia jinsi tulivyo shangalabaghala kwenye majanga, swali ni how prepared are we kukabiliana na majanga?. Najua uwezo wa kama wenzetu nchi zilizoendelea hatuna, lakini hata utoaji tuu wa taarifa nao ni mpaka Wazungu ndio watusaidie?. Saa hizi wenzetu wazungu wa Mtwara na Lindi, tangu jana wameyakimbia maeneo haya, kwa vile wazungu ni wageni huku sii kwao, wao wako right kukimbia kuelekea maeneo salama, lakini kwa wenyeji ambao Mtwara na Lindi ndio kwao na hawana pa kukimbilia, hakuna utoaji taarifa wowote wa maana hawa wananchi wafanye nini, waende wapi, wachukue tahadhari gani?.

Kwa vile kimbunga hiki kinaweza kuandamana na mvua kubwa yenye upepo mkali na uwezekano wa mafuriko, nilidhani ilikuwa ni busara kwa serikali ya mkoa kuwaelekeza wananchi wa mabondeni wenye nyumba za udongo za mbavu za mbwa, leo wakusanyike maeneo ya milimali, au kwenye mashule ili mafuriko yakipita yasombe tuu nyumba na sio nyumba na maisha ya watu.

Disaster communications ni specialization, kunapotokea majanga, kuna watu wengi wanaathirika kwa kutopata taarifa sahihi, hivi kujifunza kutoa taarifa sahihi za majanga, ni lazima kusubiri kwanza majanga yatokee ndipo tujifunze kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kupunguza athari za majanga hayo?.

Mungu apishilie mbali hili Janga la Kimbunga Mtwara na Lindi. Kabla ya ujio wa wazungu, Mababu zetu walikuwa na utaalamu sio tuu wa kubaini majanga kama haya kabla hayajatokea, bali walikuwa na uwezo wa kuyazuia na hivyo yasilete madhara. Mkama Rumanyika wa Karagwe, alizuia mvua, radi na mafuriko, na ikitokea vita, anawtumia tuu maadui zake mvua ya mawe na kuwatumia radi, ina wakata kata na kuwasambaratisha.

Kwenye kabila langu Wasukuma, watu hawa wapo mpaka kesho, serikali yetu inaweza kuamua kufuangua chuo pale Gamboshi, kama vipi waende tuu wakaombe msaada, mabingwa wa Kisukuma watue leo usiku Pwani ya Mtwara na Lindi na kukizuia hicho kimbunga kiishie kule kule baharini kisifike nchi kavu na kuleta madhara.

Namalizia kwa swali za msingi la uzi huu, Majanga ya Natural Disasters: Tanzania How Well Preparedness Are We?. Najua Uwezo Kuzuia Hatuna, Lakini hata Communications Alert Tuu ya What to Do Tunashindwa?!, Au Na hili pia linahitaji fedha za nchi wafadhili na wahisani watusaidie kuwaeleza tuu wananchi wetu wajiandae vipi kwa majanga fulani fulani?.

Nawatakia Alhamisi Njema.

Paskali
 

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Messages
10,251
Points
2,000

mcubic

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2011
10,251 2,000
"Kabla ya ujio wa wazungu, Mababu zetu walikuwa na utaalamu sio tuu wa kubaini majanga kama haya kabla hayajatokea, bali walikuwa na uwezo wa kuyazuia na hivyo yasilete madhara.

Mkama Rumanyika wa Karagwe, alizuia mvua, radi na mafuriko, na ikitokea vita, anawtumia tuu maadui zake mvua ya mawe na kuwatumia radi, ina wakata kata na kuwasambaratisha"
 

mkafrend

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Messages
3,054
Points
2,000

mkafrend

JF-Expert Member
Joined May 12, 2014
3,054 2,000
Namalizia kwa swali za msingi la uzi huu, Majanga ya Natural Disasters: Tanzania How Well Preparedness Are We?. Najua Uwezo Kuzuia Hatuna, Lakini hata Communications Alert Tuu ya What to Do Tunashindwa?!, Au Na hili pia linahitaji fedha za nchi wafadhili na wahisani watusaidie kuwaeleza tuu wananchi wetu wajiandae vipi kwa majanga fulani fulani?.
Paskali
Paskali, sisi akili zetu lazima zifanyiwe scanning - ukienda TBC huenda ukakuta taarifa za kuuza vitambulisho vya machinga badala ya kutoa elimu kwa wananchi wetu - halafu TBC hiyo ndiyo uikute ikihamasisha watu kuchangia fedha za uokozi kama walivyofanya wakati wa MV Nyerere!

Sisi ni watu wa karne ya 21!
 

Matola

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
40,139
Points
2,000

Matola

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2010
40,139 2,000
Taifa ambalo halikujiandaa na majanga basi ujuwe limejiandaa na msiba.

Wale kina Kimbisa wanapiga tu pesa za red cross wakati red cross inapaswa kuwa na magari yake na helicopter zake na mpaka dakika hii red cross wangekuwa wamepiga kambi huko wapo standbdby kutowa huduma ya uwokozi.

Na usishangae ile ziara yetu ya siku 8 Mbeya ikaendelea kama kawaida.
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Messages
3,557
Points
2,000

Jp Omuga

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2012
3,557 2,000
Sasa Mkuu PASKALI unataka watoe "communication alerts" kwani walipokuwa wanagombea waliahidi watayaleta hayo majanga ya asili..??
Ila muhimu kujua ni kuwa "Mioyoni mwao wanaombea hayo majanga yatokee haraka (na kila mara) ili yatumike kama kiki kisiasa au kuwakomoa watu fulani.."!!
 

wakatanta

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Messages
1,411
Points
2,000

wakatanta

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2018
1,411 2,000
"Kabla ya ujio wa wazungu, Mababu zetu walikuwa na utaalamu sio tuu wa kubaini majanga kama haya kabla hayajatokea, bali walikuwa na uwezo wa kuyazuia na hivyo yasilete madhara.

Mkama Rumanyika wa Karagwe, alizuia mvua, radi na mafuriko, na ikitokea vita, anawtumia tuu maadui zake mvua ya mawe na kuwatumia radi, ina wakata kata na kuwasambaratisha"
Wazungu wameua tamaduni zetu,ngoja tuone hiki kilanga mwisho wake,mungu atuapushe na madhira ya hiki kimbunga
 

Forum statistics

Threads 1,391,509
Members 528,420
Posts 34,083,171
Top