Natumani kwa mtafaruku huu Bungeni, Rais wetu hata tafuta suluhu kwa kukutana na wazee wa Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natumani kwa mtafaruku huu Bungeni, Rais wetu hata tafuta suluhu kwa kukutana na wazee wa Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lyimo, Apr 20, 2012.

 1. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Imekuwa ni mazoea kwa serikali yetu kutatua ama kuzungumzia matatizoyanayolikumba Taifa kwa kuzungumza na wazee wa Dar na kutoa makaripio, vitishona hata kejeli ili wananchi wapate ujumbe kwa namna serikali inavyopenda. Tumeshuhudiamgogoro wa wafanyakazi ulipochukua kasi, na kuona jinsi Rais wetualivyolishughulikia kwa kuzungumza na wazee wa Dar es salaam.

  Vilevile, lichaya mgomo wa madaktari ulivyochukua muda mrefu na kuleta madhara makubwa, Raiswetu alikuja kuongea na Wazee wa Dar na kufikisha ujumbe wake kwa wananchi kamatulivyomsikia.
  Kutokana hali ilivyo tete kwa serikali kutuhumiwa kwa ubadhilifumkubwa unaosababishwa katika ngazi mbalimbali pamoja na viongozi wajuu, bungelilikemea ubadhilifu huo na hata kufikia sasa kuamua kupiga kura ya kutokuwa naimani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusiomamia Mawaziri wake ambao aliwachaguayeye na Mh. Rais.

  Kumekuwa na kelele za chini kwa chini kwamuda mrefu kuhusu kutoridhishwana ufanisi wa viongozi, lakini Rais na Waziri Mkuu hatukuona hatua yoyotestahiki. Sasa imefikia mahali tete ambapo hata Wabunge wa chama tawalawamechoshwa na kutetea serikali ya CCM ambayo imepoteza imani kwa wananchi.

  Tunatumaini sasa Rais na washauri wake watajua ili kumaliza tatizosi kuzungumza propaganda na wazee wa Dar es salaam, ni vema ijifunzekushughulikia tatizo husika kwa kujadiliana na wahusika ama kuchukulia hatua wahusikakwa haraka.

  Kwasasa si rahisi tena kwenda kuzungumza na Wazee wa Dar ilikupotosha jamii juu ya ubadhilifu serikalini na jinsi viongozi tuliowapadhamana kushindwa kusimamia shughuli za serikali kwa uadilifu. Ni hakika sasaRais na washauri wake watabaini kuwa kitendo cha kuongea na wazee wa Dar ilikupotosha jamii na kutishia wahusika si njia sahihi ya kushughulikia matatizoyanayoikumba serikali yetu.
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Akifanya hivyo atakuwa ni rais bomu kuliko wote, suala kama hili si la kuongea na wazee wa Dar.

  Atafute njia mujalabi wa kushughulikia matatizo yetu.
   
Loading...