Natumai mbobezi wa sheria Profesa Kabudi atatudadavulia namna Nusrat Henje alivyotoka jela usiku na asubuhi kuwa mbunge!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,867
141,804
Nikuombea tu Waziri wa katiba na sheria Prof Palamagamba Kabudi utuwekee sawa hili la mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Nusrat Henje namna alivyoupata ubunge.

Hili swala lina utata mwingi na ni doa kubwa kwenye chombo kitukufu kama bunge tena kinachoongozwa na daktari wa sheria Tulia Ackson.

Je, kuna uhusiano gani kati ya CHADEMA na DPP hadi zoezi lile likaweza kukamilika kwa namna ile?

Je, kuna mazingira ya rushwa?

Niishie hapo

Ukinizingua Nakuzingua!
 
Mkuu mbona unamnyang'anya mwenye mhimili Mh Ndugai na kumpa Tulia?

Ila hilo swali wa kulijibu alikuwa Mwigulu huyo ndiyo anajua vifungu vya sheria vilivyotumika pamoja na DPP wake ila huyu DPP sijui kwanini mama hakushuka naye jumlajumla
 
Nikuombe tu Waziri wa katiba na sheria Prof Palamagamba Kabudi utuwekee sawa hili la mbunge wa viti maalumu kupitia Chadema Nusrat Henje namna alivyoupata ubunge.

Hili swala lina utata mwingi na ni doa kubwa kwenye chombo kitukufu kama bunge tena kinachoongozwa na daktari wa sheria Tulia Ackson.

Je, kuna uhusiano gani kati ya Chadema na DPP hadi zoezi lile likaweza kukamilika kwa namna ile?

Je, kuna mazingira ya rushwa?

Niishie hapo

Ukinizingua Nakuzingua!
Kwanza Chadema haina Mbunge wa viti maalum. Pili huyo Nusrat alitolewa kwa amri toka juu( kwa sasa tamka amri toka Chato graveyard). Tatu ni jinsi gani alivyopata Ubunge muulize yule andunje mgonjwa wa safura. Kwaheri
 
Ni kinyonga huyo kama mataga wengine tuu
Kama huyu hapa
IMG-20210407-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom