Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbukiwa na tatizo la kutokwa na makohozi na mate ya utelezi. Tatizo hilo limedumu kwa muda wa miaka 3. Nimeenda hospitali kadhaa lakini sijapata matibabu ya kumaliza tatizo hilo. Kuna daktari mmoja alinieleza kuwa ugonjwa huo unatibika kwa dawa za asili na unajulikana kama Ndimi Mbili. Sina hakika kama jina hilo ni la kitaalam au ni majina yetu ya uswahilini.
Naamini kuwa JF ina watu wanaojua mambo mengi na ninaamini kuwa hata tatizo hili wanalifahamu na wanafahamu tuba yake. Mwenye uelewa mpana juu ya ugonjwa huu atuwekee maelezo ya kutosha na ni vema pia akaainisha na tiba ili isaidie na wengine wanaoteseka pasi na mafanikio
Ahsante
CC. ZEMARCOPOLO