Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 127
Habari zenu wanaJF,
Napenda nitofautiane kidogo na wenzangu kuhusu hili suala la Katiba mpya. Kwangu mimi kipaumbele cha kwanza ni mishahara mikubwa na posho nono wanazopewa wabunge. Kama kweli wabunge wetu ni wazalendo wangeanza na hili na kuhakikisha kabla ya bunge la bajeti 2011/2012 limefanikiwa na kinachobakia kwenye mishahara ikaenda kuongezewa kwa waalimu na wauguzi. Maana watu watakuwa busy kwa miaka mitano kudai katiba mpya huku watoto wetu wakipewa elimu mbovu na huduma mbaya za afya kwakuwa wauguzi na waalimu maslahi yao yamemezwa na waheshimiwa wabunge!
Halafu mwaka 2011 baada ya kikao cha bajeti waanze mchakato wa katiba mpya sambamba na kubadilisha katiba zao za vyama maana hata huko kwenye vyama katiba hazikidhi matakwa ya wengi. Sipendi kutolea mifano ila ipo mingi sana kwenye baadhi ya vyama vyetu kuna uditekta, kujuana na undugu.
Nawakilisha....